Mjue Frederick De Klerk 1936-2021 Mkombozi wa Afrika Kusini

jerrysonkiria

JF-Expert Member
Sep 5, 2014
2,232
2,884
MJUE FREDERICK DE KLERK 1936-2021

Mkombozi wa Afrika Kusini

Najua wajua lakini acha wanaojua kidogo wajue zaidi.

Ninataka umjue rafiki wa Waafrika weusi kwenye kundi la weupe wachache, watawala fedhuri Makabulu (boers) wa Afrika kusini. Mtu huyo wa ajabu ni Frederick de Klerk rais wa mwisho mzungu wa Afrika kusini.

Wakati wa uongozi P W Botha mtu huyu mzaliwa wa Kenya kwenye mashamba (plantations) ya baba yake alikuwa waziri wa fedha, baraza lenye mawaziri machachari waua watu kama waziri wa mambo ya nje wa Sauzi ya wakati huo Mr Pick Botha.

Hizo ni tarehe za mateso ya akina Nelson Mandela huko gerezani, kuchinjwa kwa vijana kama Steve Bikho na Solomon Maharangu na mauaji ya wanafunzi wa Soweto na ghasia mbalimbali.

Siku mama Winnie Madikizela Mandela akisema anakwenda gerezani kumuona mumewe Mzee Mandela basi ni fujo na si ajabu makumi ya watu wakafa.

Kama ndoto 1989 De Klerk huyu akatwaa uongozi wa serikali ya kidharimu na kutangaza mabadiliko. Akawatembelea wafungwa wa kisiasa magerezani akiwemo Tata Madiba (Mandela) na kutaka meza ya mazungumzo.

Wakuu wa chama kikuu cha ukombozi ANC kikikaa Lusaka enzi hizo akina Oliver Thambo, Govan Mbeki (baba wa rais Thabo Mbeki) na Afred Nzowa walisita kuhudhuria meza hiyo.

Wakihofia je, De Klerk ni mkweli? Vipi waliomzunguuka? Zilihitajika busara za akina Mwl Nyerere na Kenneth Kaunda kuweza kuisoma dhati ya mzungu muapethaid huyu.

Akaanza kuwatoa wafungwa kama akina mzee Walter Sisulu na wengineo na wakaja hapa Dodoma kumuakua Mwl. Nyerere Je mkabulu huyu ni mkweli?

***********************

Hatimaye De KLERK akamtoa na Nelson Mandela baada miaka 29 gerezani. De KLERK Wazungu wenzie walimkosa mara kadhaa kwa risasi na kujaribu kumng'oa kwenye kiti kama yeye mwenyewe alivyomng'oa mtangulizi wake Mr Jan Christian, lakini walishindwa. Na hii ikazidisha shaka kwetu sisi watu weusi vipi wakifaulu kumng'oa?

Sasa De Klerk akaendelea na uamuzi wake na akasema tukae tuzungumze na vyama vya ukombozi virudi Sauzi.

Kuna baadhi ya wapigania Uhuru na viongozi wa ANC waliokuwepo Lusaka kwa woga wa kurudi kule Sauzi wakamteua Mandela kuwa rais wa ANC (cheo kipya), ieleweke kuwa chama cha ANC kilikuwa na vyeo vya juu ambavyo ni Mwenyekiti na katibu tu. Sasa baada ya hapo chama kinakuwa kimerudi rasmi na mazungumzo na De klerk yaanze.

Lakini upande mwingine chama kingine cha PAC kiliapa hakitakaa meza moja na kabulu kuzungumza badala yake ni mtutu tu ndio utaamua ukombozi!

Sharti la De Klerk kubwa ni kuwa tukubaliane kuwa sisi sote ni Wasauzi na kwamba hakuna mgeni kati ya weupe na weusi. Je tukubali ? Nyerere tushauri baba (viongozi wa ukombozi wakimuomba ushauri Mwl.) Ulikuwa mtihani.

Hatimaye tukakubali kuwa Wazungu nao waendelee kuwepo sauzi maana na wao kwao ni palepale Sauzi.

De Klerk anasema kama ndivyo sasa anaitisha uchaguzi wa mtu mmoja kura moja. Anasema hayo huku akijua kuwa idadi yao ni ndogo sana pale. Wao ndio matajiri wenye uchumi na nguvu za kijeshi halafu anakubali hayo. Akachochea chuki kubwa kwa Wazungu wenzie wa ndani na wa nje.

Swali waliojiuliza zaidi je hivi De Klerk ni mkweli?

Mungu akawa upande na hatimaye uchaguzi ulifanyika kwa tume ya uchaguzi aliyoiunda yeye na yeye akiwa mgombea kutoka chama kilicho madarakani. Kura zikahesabiwa kwa haki na mshindi akatangazwa ni Tata Madiba Nelson Mandela.

De Klerk alifurahishwa na matokeo na akampa ulinzi wa nguvu Mandela kama rais mteule kuelekea siku ya kuapishwa ambayo siku hiyo ilikuwa mbali kidogo. Maswali yakazidi kuibuka miongoni mwa wasauzi (hivi siku ya kuapishwa Mandela itafika kweli )

Tulisubiri kwa hamu na ghamu.

Hatimaye Mandela akaapishwa na akapishwa Ikulu na mtu huyu. Mandela alimwomba awe msaidizi wake kwa muda na baadae aliondoka Ikulu !!.

Mtu huyu FREDERICK WILlEM DE KLERK amefariki dunia leo Tarehe 11 Nov 2021 akiwa na miaka 85. Kwa kweli RIP mwamba.

Aksanteni kwa kunisikiliza.
Imeandaliwa na
SHIDA S. SADIKI

images-3.jpeg
images-15.jpeg
images-14.jpeg
images-13.jpeg
 
Hapa Hakuna historia ya kwenye vitabu iliyo ongezewa na kupunguzwa mambo, hii imeandaliwa na alieshuhudia siasa ya Afrika Kusini na ukombozi wake.

Pia unaweza kuongeza unayojua kumuhusu De Klerk mkuu.
Mkuu kasome vizuri historia
 
Truth and Reconciliation commission ya mwaka 1995, ilikuja na ripoti ikionyesha kwamba huyu Bwana alihusika na ubaguzi wa rangi "apartheid policy", japo alikataa.Hizo ni propaganda za White's kusafisha uovu wao dhidi ya South Africa. Unyonyaji, unyanganyi, mateso, mauaji ya wasouth yalifanyika chini ya utawala wake, aliona liberation movement ya ANC, ingekuja kuwashinda na vile nchi karibia zote za Africa zilishakombolewa kwahiyo alikuwa hana namna tena, zaidi ya kufanya hivyo.
 
Nisingemwita mkombozi. Lakini alikuwa na busara tosha kuelewa dalili za wakati, alikuwa na utu kiasi ili asijaribu kusimamisha mabadiliko kwa njia za kijeshi; mlinganishe na Mobutu au Gaddhafi, utaona alikuwa na sifa zake pia.
 
Truth and Reconciliation commission ya mwaka 1995, ilikuja na ripoti ikionyesha kwamba huyu Bwana alihusika na ubaguzi wa rangi "apartheid policy", japo alikataa.Hizo ni propaganda za White's kusafisha uovu wao dhidi ya South Africa. Unyonyaji, unyanganyi, mateso, mauaji ya wasouth yalifanyika chini ya utawala wake, aliona liberation movement ya ANC, ingekuja kuwashinda na vile nchi karibia zote za Africa zilishakombolewa kwahiyo alikuwa hana namna tena, zaidi ya kufanya hivyo.
Ajengewe mnara angeamua kutumia jeshi nani angemshinda
 
Sio kweli kabisa hii na ANC hawakukomboa hata 1inch ya S.A. in the battle ground,RIP de Kleck you run your race go and rest peaceful. Unapomchafua binadamu aliyefanya juhudi towards umoja,upendo ni muhimu tukaheshimu hilo.
Truth and Reconciliation commission ya mwaka 1995, ilikuja na ripoti ikionyesha kwamba huyu Bwana alihusika na ubaguzi wa rangi "apartheid policy", japo alikataa.Hizo ni propaganda za White's kusafisha uovu wao dhidi ya South Africa. Unyonyaji, unyanganyi, mateso, mauaji ya wasouth yalifanyika chini ya utawala wake, aliona liberation movement ya ANC, ingekuja kuwashinda na vile nchi karibia zote za Africa zilishakombolewa kwahiyo alikuwa hana namna tena, zaidi ya kufanya hivyo.
 
Busara za mwalimu Nyerere zilikua kubwa kuliko huyo madiba nashangaa eti yeye ndo wazungu wanamtambua kama mpigania uhuru Afrika wana msahau mwl Nyerere hatajwi hata kwa bahati mbaya kuna kitu wanacho muogopa Mwl. watu walikula msoto mwl anajibana kubalance mambo na kuwasaidia nchi mbalimbali mpaka zikajitawala mtu mkweli alikua mgabe tu huyu alikua anawagomea wakisema madiba ndi baba wa ukombozi mugabe yeye alipaza sauti kumtambua mwl Nyerere, sio uyo croned tata wao.
 
Hakuna lolote hapo ni muda ulifika tu! wao waachie ngazi sababu ya ANC na OAU, watake wasitake!! hata km ingewachukua miaka mianne kuikalia south wazungu wangekufa tu!! km siyo kwisha kabisa!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom