Mjue Bi Fatma Abdalla (Toti), Mwanamke jasiri aliyekuwa chimbuko la kuazishwa kwa CUF

Kakke

JF-Expert Member
Dec 4, 2010
1,886
2,000

Ndani ya jamii yetu ya Zanzibar kuna wananawake mbali mbali ambao miongoni mwao wengine ni vigumu kuweza kusahaulika kirahisi aidha kutokana na umahiri wao wa kazi zao mbali mbali ndani ya jamii.

Leo hii tumeamua kumzungumzia mwanamke ambaye aliwahi na ataendelea kuwa historia ndani ya Zanzibar na Taifa kwa ujumla,mwanamke huyu ni Bi Fatma Abdalla (toti) aliekuwa mkaazi wa shehia ya kokoni jimbo la mji mkongwe.

Mama huyu ni miongoni mwa mwanamke aliekuwa jasiri kutokana na kupewa upeo mkubwa wa kipaji cha kuwa no moyo wa kutumikia chama cha wananchi CUF,historia zinasema chimbuko hasa la CUF limetokana na mchango mkubwa sana wa mama huyu.

Mnamo tarehe 25/5/1992 Bi Fatma alitumia nyumba yake ilioko kokoni kwa ajili ya mkutano wa siri uliokuwa na lengo la kuzaliwa kwa chama cha wananchi CUF,mkutano huo uliovikutanisha vyama viwili kwa wakati huo ambavyo vilikuwa ni CCW (chama cha wananchi) kilichotokea bara ambacho muasisi wake alikuwa Jams mapalala,pamoja na chama cha ''Kama huru '' ambacho kilitokea upande wa Zanzibar na lengo lake ni kuteta haki na uhuru wa wazanzibar.

Kuwepo kwa mkutano huu ambao ulifanyika kwa siri kubwa kipindi hicho huku serikali iliyokuwepo ikiongozwa na Dkt Salmin Amour kupitia jeshi la Polisi waliendelea kufanya doria mji mzima wa Unguja kuhakikisha kwamba mkutano huu haufanyiki lakini hali haikuwa hivo badala yake mkutano huo uliweza kufanyika kama ilivopangwa ingawa ulikuwa ni wasiri kubwa.

Siku hii ya tarehe 25/5/1992 mara tu baada ya kumalizika makubaliano yaliyotokana na mkutano huu kulianzishwa chama kipya ambacho kilitokana na muungano wa vyama hivi viwili na kiliitwa chama cha wananchi (CUF)miongoni mwa waliotia saini makubaliano hayo ni Shaban Khamis Mloo kwa upande wa Zanzibar ambae alitokea chama cha ''kama huru'' na kwa upande wa chama cha ''CCW''alietia saini ni Jams Mapalala alietokea Tanzania Bara,kutokana na makubaliano haya ya utiwaji huu wa saini kwa uwazinshwaji wa chama kipya ni wazi kabisa kwamba chama cha wananchi CUF kilianzishwa mnamo tarehe 25/5/1992 nyumbani kwa ''Bifatma Toti'' kokoni ambae kwa sasa ni marehemu mwenyezimungu amlaze mahali pema peponi.

Kama ilivyo kawaida kwa jambo kubwa kama hili ni lazima kuwe na mashahidi walioshuhudia utiaji huu wa saini hizi za uanzishwajwi wa chama hichi nilipotaka kujua ni nani waliokuwa mashahidi nijibiwa hivi '' kwa upande wa chama cha '' CCW '' walimteuwa Jams B Mashime kuwa shahidi nambari moja na mwengine alikuwa ni Dkt Alex Chaponda,kuea shahidi nambari mbili,ama kwa upande wa Zanzibar walioshuhudia walikuwa ni Mzee Ali Hajji Pandu pamoja na Faki Pandu Makame.

Kuanzia hapa chama hichi kiliendeleza harakati zake kwa njia ya siri.

Mnamo tarehe 17/8/1993 chama cha wananchi CUF kiliweza kupata usajili wa muda na kuanza kutambulika zaidi nchi nzima kama chama pekee cha upinzani kilichoanzishwa kwa muda mfupi na kuwa na nguvu ya kupata wananchama wapya wengi mno kikiongozwa chini ya Mwenyekiti wake Jams Mapalala.

Miezi kadhaa badae baada ya chama kupata usajili wa muda ilipofika tarehe 21/1/1993 Chama kiliweza kupata usajilli wake rasmi na kilianza kutambulika kitaifa na kimataifa kama ni chama cha mwanzo halali cha kidemokrasia ndani ya Zanzibar.

Mara tu baada ya kupata usajili huo wa kudumu chama kiliendeleza harakati zake kila sehemu Tanzania nzima ili kujitangaza,baadae kiliamua kuitangaza siku ya tarehe 31/1/1993 kuwa ni siku maalumu ya kupachika bendera ya chama hicho ndani ya matawi yote Unguja na Pemba.

Hatua hii ya upachikaji wa bendera kwa matawi yote katika kipindi hicho ilifanyika ingawa kwa upande mwengine iliweza kuibua vilio na msiba kutokana na Kijana aliejulikana kwa jina la Omar Hajji Ali mkaazi wa shumba wilaya ya Micheweni mkoa wa kaskazini Pemba kufariki dunia kwa kupigwa risasi na polisi ambao walipewa amri ya kuzuia upachikaji huo wa bendera za chama na aliekuwa mkuu wa mkoa kaskazini Pemba kipindi hicho Bwana ''Ramadhan Khamis Feruzi,mtu mwengine ambae alipigwa risasi katika tukio hilo na kujeruhiwa vibaya ni Ali Juma Msuka mkaazi wa Shumba.

Kutokana na tukio hili historia zinatufunza kuwa kijana huyu aleuwawa ndio mtu wa mwanzo kabisa kufa kwa ajili ya kuitetea haki ndani ya visiwa hivi kupitia chama cha wananchi CUF,binafsi namuomba mwenyezimungu amlaze mahali pema peponi yeye na wengine wote,Amee.

Namailiza kwa kutoa shukrani zangu za dhati kwa walionisaidia kufanikisha kuandika makala hii ndogo,Asante sana Mh,Ismail Jussa,asante sana Mh,Salim Bimani kwa ushirikiano wenu.
 
Kakke

JF-Expert Member
Dec 4, 2010
1,886
2,000
Mh Mbowe aliposema sisi ni wanzilishi wa Chadema na tumetoka mbali kukisimamicha chama hichi mpaka kikasimama,sio leo wanatoka watu fulani fulani tu wameshahongwa na ccm wanakuja kukivuruga chama na kutaka kukigawa kwa misingi yaUkanda,ukabila na Udini ,Hatotokuwa tayari kuwalea watu hao tulowagaribisha kipindi kifupi tu katika chama.

Mh Mbowe yuko right angalia cuf wameweza kumfukuza Mapalala na Hamadi Rashid ambae ni Ndugu yake Seif itakuwa Zitto na kundilake la virus vya ccm?.

Lengo la zito nikutaka kukigawa chama kwa kutumia kikanda,udini na hatari kwa Taifa hili tulilo nalo,na kumvumilia mtu huyo sio jambo jema,nikulea marazi.

Funzo jengine Juzi korea ya Kaskazini imemnyonga Mjomba wa Raisi wa nchi hio kutokana na Usaliti wa kutumiliwa na western country.

Bonyeza uone
swahilivilla: Mjomba wa kiongozi wa Korea ya Kaskazini, Jang Song-Taek anyongwa
 
CHAMVIGA

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
7,689
2,000
Ndani ya jamii yetu ya Zanzibar kuna wananawake mbali mbali ambao miongoni mwao wengine ni vigumu kuweza kusahaulika kirahisi aidha kutokana na umahiri wao wa kazi zao mbali mbali ndani ya jamii.

Leo hii tumeamua kumzungumzia mwanamke ambaye aliwahi na ataendelea kuwa historia ndani ya Zanzibar na Taifa kwa ujumla,mwanamke huyu ni Bi Fatma Abdalla (toti) aliekuwa mkaazi wa shehia ya kokoni jimbo la mji mkongwe.

Mama huyu ni miongoni mwa mwanamke aliekuwa jasiri kutokana na kupewa upeo mkubwa wa kipaji cha kuwa no moyo wa kutumikia chama cha wananchi CUF,historia zinasema chimbuko hasa la CUF limetokana na mchango mkubwa sana wa mama huyu.

Mnamo tarehe 25/5/1992 Bi Fatma alitumia nyumba yake ilioko kokoni kwa ajili ya mkutano wa siri uliokuwa na lengo la kuzaliwa kwa chama cha wananchi CUF,mkutano huo uliovikutanisha vyama viwili kwa wakati huo ambavyo vilikuwa ni CCW (chama cha wananchi) kilichotokea bara ambacho muasisi wake alikuwa Jams mapalala,pamoja na chama cha ''Kama huru '' ambacho kilitokea upande wa Zanzibar na lengo lake ni kuteta haki na uhuru wa wazanzibar.

Kuwepo kwa mkutano huu ambao ulifanyika kwa siri kubwa kipindi hicho huku serikali iliyokuwepo ikiongozwa na Dkt Salmin Amour kupitia jeshi la Polisi waliendelea kufanya doria mji mzima wa Unguja kuhakikisha kwamba mkutano huu haufanyiki lakini hali haikuwa hivo badala yake mkutano huo uliweza kufanyika kama ilivopangwa ingawa ulikuwa ni wasiri kubwa.

Siku hii ya tarehe 25/5/1992 mara tu baada ya kumalizika makubaliano yaliyotokana na mkutano huu kulianzishwa chama kipya ambacho kilitokana na muungano wa vyama hivi viwili na kiliitwa chama cha wananchi (CUF)miongoni mwa waliotia saini makubaliano hayo ni Shaban Khamis Mloo kwa upande wa Zanzibar ambae alitokea chama cha ''kama huru'' na kwa upande wa chama cha ''CCW''alietia saini ni Jams Mapalala alietokea Tanzania Bara,kutokana na makubaliano haya ya utiwaji huu wa saini kwa uwazinshwaji wa chama kipya ni wazi kabisa kwamba chama cha wananchi CUF kilianzishwa mnamo tarehe 25/5/1992 nyumbani kwa ''Bifatma Toti'' kokoni ambae kwa sasa ni marehemu mwenyezimungu amlaze mahali pema peponi.

Kama ilivyo kawaida kwa jambo kubwa kama hili ni lazima kuwe na mashahidi walioshuhudia utiaji huu wa saini hizi za uanzishwajwi wa chama hichi nilipotaka kujua ni nani waliokuwa mashahidi nijibiwa hivi '' kwa upande wa chama cha '' CCW '' walimteuwa Jams B Mashime kuwa shahidi nambari moja na mwengine alikuwa ni Dkt Alex Chaponda,kuea shahidi nambari mbili,ama kwa upande wa Zanzibar walioshuhudia walikuwa ni Mzee Ali Hajji Pandu pamoja na Faki Pandu Makame.

Kuanzia hapa chama hichi kiliendeleza harakati zake kwa njia ya siri.

Mnamo tarehe 17/8/1993 chama cha wananchi CUF kiliweza kupata usajili wa muda na kuanza kutambulika zaidi nchi nzima kama chama pekee cha upinzani kilichoanzishwa kwa muda mfupi na kuwa na nguvu ya kupata wananchama wapya wengi mno kikiongozwa chini ya Mwenyekiti wake Jams Mapalala.

Miezi kadhaa badae baada ya chama kupata usajili wa muda ilipofika tarehe 21/1/1993 Chama kiliweza kupata usajilli wake rasmi na kilianza kutambulika kitaifa na kimataifa kama ni chama cha mwanzo halali cha kidemokrasia ndani ya Zanzibar.

Mara tu baada ya kupata usajili huo wa kudumu chama kiliendeleza harakati zake kila sehemu Tanzania nzima ili kujitangaza,baadae kiliamua kuitangaza siku ya tarehe 31/1/1993 kuwa ni siku maalumu ya kupachika bendera ya chama hicho ndani ya matawi yote Unguja na Pemba.

Hatua hii ya upachikaji wa bendera kwa matawi yote katika kipindi hicho ilifanyika ingawa kwa upande mwengine iliweza kuibua vilio na msiba kutokana na Kijana aliejulikana kwa jina la Omar Hajji Ali mkaazi wa shumba wilaya ya Micheweni mkoa wa kaskazini Pemba kufariki dunia kwa kupigwa risasi na polisi ambao walipewa amri ya kuzuia upachikaji huo wa bendera za chama na aliekuwa mkuu wa mkoa kaskazini Pemba kipindi hicho Bwana ''Ramadhan Khamis Feruzi,mtu mwengine ambae alipigwa risasi katika tukio hilo na kujeruhiwa vibaya ni Ali Juma Msuka mkaazi wa Shumba.

Kutokana na tukio hili historia zinatufunza kuwa kijana huyu aleuwawa ndio mtu wa mwanzo kabisa kufa kwa ajili ya kuitetea haki ndani ya visiwa hivi kupitia chama cha wananchi CUF,binafsi namuomba mwenyezimungu amlaze mahali pema peponi yeye na wengine wote,Amee.
na HEMEDI MAZRUI.
 
kibwengomfupi

JF-Expert Member
Jul 21, 2016
689
1,000

Ndani ya jamii yetu ya Zanzibar kuna wananawake mbali mbali ambao miongoni mwao wengine ni vigumu kuweza kusahaulika kirahisi aidha kutokana na umahiri wao wa kazi zao mbali mbali ndani ya jamii.

Leo hii tumeamua kumzungumzia mwanamke ambaye aliwahi na ataendelea kuwa historia ndani ya Zanzibar na Taifa kwa ujumla,mwanamke huyu ni Bi Fatma Abdalla (toti) aliekuwa mkaazi wa shehia ya kokoni jimbo la mji mkongwe.

Mama huyu ni miongoni mwa mwanamke aliekuwa jasiri kutokana na kupewa upeo mkubwa wa kipaji cha kuwa no moyo wa kutumikia chama cha wananchi CUF,historia zinasema chimbuko hasa la CUF limetokana na mchango mkubwa sana wa mama huyu.

Mnamo tarehe 25/5/1992 Bi Fatma alitumia nyumba yake ilioko kokoni kwa ajili ya mkutano wa siri uliokuwa na lengo la kuzaliwa kwa chama cha wananchi CUF,mkutano huo uliovikutanisha vyama viwili kwa wakati huo ambavyo vilikuwa ni CCW (chama cha wananchi) kilichotokea bara ambacho muasisi wake alikuwa Jams mapalala,pamoja na chama cha &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];'Kama huru &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];' ambacho kilitokea upande wa Zanzibar na lengo lake ni kuteta haki na uhuru wa wazanzibar.

Kuwepo kwa mkutano huu ambao ulifanyika kwa siri kubwa kipindi hicho huku serikali iliyokuwepo ikiongozwa na Dkt Salmin Amour kupitia jeshi la Polisi waliendelea kufanya doria mji mzima wa Unguja kuhakikisha kwamba mkutano huu haufanyiki lakini hali haikuwa hivo badala yake mkutano huo uliweza kufanyika kama ilivopangwa ingawa ulikuwa ni wasiri kubwa.

Siku hii ya tarehe 25/5/1992 mara tu baada ya kumalizika makubaliano yaliyotokana na mkutano huu kulianzishwa chama kipya ambacho kilitokana na muungano wa vyama hivi viwili na kiliitwa chama cha wananchi (CUF)miongoni mwa waliotia saini makubaliano hayo ni Shaban Khamis Mloo kwa upande wa Zanzibar ambae alitokea chama cha &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];'kama huru'' na kwa upande wa chama cha &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];'CCW''alietia saini ni Jams Mapalala alietokea Tanzania Bara,kutokana na makubaliano haya ya utiwaji huu wa saini kwa uwazinshwaji wa chama kipya ni wazi kabisa kwamba chama cha wananchi CUF kilianzishwa mnamo tarehe 25/5/1992 nyumbani kwa &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];'Bifatma Toti'' kokoni ambae kwa sasa ni marehemu mwenyezimungu amlaze mahali pema peponi.

Kama ilivyo kawaida kwa jambo kubwa kama hili ni lazima kuwe na mashahidi walioshuhudia utiaji huu wa saini hizi za uanzishwajwi wa chama hichi nilipotaka kujua ni nani waliokuwa mashahidi nijibiwa hivi &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];' kwa upande wa chama cha &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];' CCW '' walimteuwa Jams B Mashime kuwa shahidi nambari moja na mwengine alikuwa ni Dkt Alex Chaponda,kuea shahidi nambari mbili,ama kwa upande wa Zanzibar walioshuhudia walikuwa ni Mzee Ali Hajji Pandu pamoja na Faki Pandu Makame.

Kuanzia hapa chama hichi kiliendeleza harakati zake kwa njia ya siri.

Mnamo tarehe 17/8/1993 chama cha wananchi CUF kiliweza kupata usajili wa muda na kuanza kutambulika zaidi nchi nzima kama chama pekee cha upinzani kilichoanzishwa kwa muda mfupi na kuwa na nguvu ya kupata wananchama wapya wengi mno kikiongozwa chini ya Mwenyekiti wake Jams Mapalala.

Miezi kadhaa badae baada ya chama kupata usajili wa muda ilipofika tarehe 21/1/1993 Chama kiliweza kupata usajilli wake rasmi na kilianza kutambulika kitaifa na kimataifa kama ni chama cha mwanzo halali cha kidemokrasia ndani ya Zanzibar.

Mara tu baada ya kupata usajili huo wa kudumu chama kiliendeleza harakati zake kila sehemu Tanzania nzima ili kujitangaza,baadae kiliamua kuitangaza siku ya tarehe 31/1/1993 kuwa ni siku maalumu ya kupachika bendera ya chama hicho ndani ya matawi yote Unguja na Pemba.

Hatua hii ya upachikaji wa bendera kwa matawi yote katika kipindi hicho ilifanyika ingawa kwa upande mwengine iliweza kuibua vilio na msiba kutokana na Kijana aliejulikana kwa jina la Omar Hajji Ali mkaazi wa shumba wilaya ya Micheweni mkoa wa kaskazini Pemba kufariki dunia kwa kupigwa risasi na polisi ambao walipewa amri ya kuzuia upachikaji huo wa bendera za chama na aliekuwa mkuu wa mkoa kaskazini Pemba kipindi hicho Bwana &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];'Ramadhan Khamis Feruzi,mtu mwengine ambae alipigwa risasi katika tukio hilo na kujeruhiwa vibaya ni Ali Juma Msuka mkaazi wa Shumba.

Kutokana na tukio hili historia zinatufunza kuwa kijana huyu aleuwawa ndio mtu wa mwanzo kabisa kufa kwa ajili ya kuitetea haki ndani ya visiwa hivi kupitia chama cha wananchi CUF,binafsi namuomba mwenyezimungu amlaze mahali pema peponi yeye na wengine wote,Amee.

Namailiza kwa kutoa shukrani zangu za dhati kwa walionisaidia kufanikisha kuandika makala hii ndogo,Asante sana Mh,Ismail Jussa,asante sana Mh,Salim Bimani kwa ushirikiano wenu.

Ahsne Kakke kwa kutujuvya chimbuko la CUF. N pahala pazuri pa kuanzia kwa wale wanaopenda siasa znz. Nakumbuka sana jinsi ya huyo mhanga wa kwanza wa CUF jinsi alivyopigwa risasi na Policcm kule Pemba. Wahanga wengine 45 walifuata mwaka 2001 baada ya kuandamana.
 
mbandeon

JF-Expert Member
Aug 27, 2014
1,399
2,000
Seif alikuwa wapi mda huo, na uwache unafiki unawezaje kumkumbuka Toti ushinde kumpa heshima hiyo Mapalala au kwa sababu alikuwa mboya teh teh teh.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom