Mjue Ali Solih, aliyekuwa Rais wa visiwa vya Comoro

Wakala wa majini

Senior Member
Jan 19, 2020
139
137
"I am your god and teacher.I am the devine way,the torch that lights up the dark.There is no god but Ali solih."

Haya ni maneno yake marehemu Ali solih aliyekuwa raisi wa Visiwa vya comoro.Kipindi hicho ndio, mwanzo bara la Africa lilikuwa katika harakati za kutaka kujinasua kutoka katika ukoloni, na Visiwa vya comoro vikiwa miongoni mwa nchi zilizowahi kupata Uhuru wao mapema ukilinganisha na taifa la Afrika kusini.

Pia wakati huu,ulikuwa wakati mgumu mno kwa nchi changa za Africa,Kwa sababu ulikuwa mwanzo kwao kujitawala.Hivyo, mahitaji muhimu kama lishe bora,Elimu na Afya vilikuwa ndoto.Pia enzi hizo, Mapinduzi ya serikali ndio ilikuwa kauli mbiu.Kila mwanasiasa alijiona kuwa ana uwezo wa kuongoza, hii ilipelekea kuwepo kwa Mapinduzi ya mara kwa mara,na hili lilikuwa jambo la kawaida tu.

Wananchi nao hawakuwa na kipingamizi, walizikubali hizo serikali mpya, ambazo zilizidi kuwakandamiza na kufanya hali zao kuwa ngumu zaidi.

Tuendelee na mada yetu.

Visiwa vya Comoro vilipata Uhuru wao mnamo mwaka 1975 July kutoka kwa dola ya france. Ali Solih alionekana mtu wa kawaida tu mara ya kwanza kupindua serikali ikiyo kuwepo na kuchukua hatamu ya uongozi wa visiwa vya Comoro miezi sita baada ya kupata uhuru.

Alikuwa na miaka 39 kipindi hicho na alikuwa na kihara.Alikuwa na wake watatu. Pia alikuwa atheist na mnywaji wa vileo licha ya kuwa alikuwa kalelewa kulingana na misingi ya kiislam.

Kwa kauli zake bila Shaka ungeliamini kuwa Ali Solih alikuwa ni mtu mwenye maono makubwa na alikuwa na nia nzuri ya kutaka kuvinasua visiwa vya comoro na watu wake kutoka katika umaskini,ila hali ilikuwa tofauti. Kumbe angelikuja kupagazwa jina la "mwendawazimu wa Moroni."

Ali Solih alibadilika ghafla mara tu alipochukua uongozi. Baadhi ya watu walidai kuwa ni madawa na tembo ndivyo vilivyo mbadilisha. Wengine walisema kuwa alikuwa mwendawazimu. Ila tatizo lilikuwa ni majukumu ya uraisi yalikuwa yakimlemea.

Ndoto na maono yake vikaanza kufifia.Akawa ni mtu wa anasa. Watu waliokuwa na akili za kufikiria na ujasiri wa kuzungumza waliishia makaburini au jela, mpaka wakabaki ma zebe wa ndio tu. Comoro ikawa kama mfano wa mwana Sesere kwa Ali Solih anaichezea anavyotaka.

Akawafuta kazi members of civil service karibia mia tano, na kuwajaza katika serikali vijana ambao walikuwa ni ma school dropout ambao angelikuwa na uwezo wa kuwapeleka anavyo taka. Akashusha umri wa kupiga kura mpaka miaka kumi na minne na kujitangaza kuwa yeye alikuwa nabii. Akafunga ma hoteli huku akisema "foreign infuence corrupt." Na kutaifisha kila kitu mpaka magari ya teksi na maduka ya kuuza mikate. Akawaleta washauri wa kichina ili waje wamuongoze na ma soldier kutoka Tanzania waje wamlinde. Akatangaza kuwa dini ni laana, na kupiga marufuku wanawake wa kiislamu kuvaa majalbib na mabaibui.

Siku moja alijivurumiza msikitini na kuanza kuwakemea waumini kwa kuwaambia "Endeleeni kumuomba Mungu. Muiteni huyo Mungu muone kama atawajibu maombi yenu."

Akawataliki wake zake na kuanza kuvamia visichana vidogo.

"Hatuwezi kuendelea tena kuipeleka hii nchi jinsi tunavyo ipeleka, nchi inapelekwa na vijana wadogo, watu wanatuona sisi wenda wazimu na taifa lote kwa ujumla limekwama." Siku moja Abbas Jusuf alimwambia Ali Solih. "Nyamaza”, Ali Solih alijibu kwa ukali. "Hivi wewe hutambui kama mimi nina maono-maono makubwa. Huu ndio mustakabali wetu." Akajibu Ali Solih.

Siku iliyofuata mamake Abbas Jusuf alikamatwa na kufungwa bila mashtaka yeyote. Siku moja Ali Solih alioteshwa "maono" makubwa. Aliota mtu na mbwa wake wamemjia na kutaka kumuua. Usiku huo alishtuka kutoka usingizini jasho likimkatika huku akitetemeka. Akamueleza mfanyakazi wake kuhusu ndoto hii. Siku iliyofuata asubuhi, baada ya chajio cha soseji na kinywaji cha brandy, Bwana solih alitoa agizo mbwa wote katika visiwa vya Comoro wauliwe mara moja.

Vijana walipata kazi, order hii ya raisi Ali Solih ilitekelezwa mara moja. Mbwa waliuliwa kwa mapanga na bunduki, wakiwaburuza wengine kwa magari yao.Mbwa waliadimika ghafla.

Nitakomea hapo wapendwa. Nitarudi na muendelezo wa jinsi utawala huu dhalimu wa Ali Solih ulivyopinduliwa.

Karibuni.
 
Muendelezo...

Ali Solih alijisahau hata asijue kama alikuwa kazungukwa na maadui wengi waliokuwa wakipanga ni jinsi gani wataupindua utawala wake.Alikuwepo Bob Debard,mercenary hatari ambaye viongozi na wanasiasa kipindi hicho walikuwa wakimtumia kuua wanasiasa wasumbufu au kupindua serikali.Huyu mercenary alikuwa alikuwa na miaka hamsini na alikuwa akijinaki na kujikaga kuwa alikuwa ni military technician.Ali solih alimtambua vyema Denard,kwa sababu yeye ndiye aliyefanikisha mapinduzi ya hapo mwanzo na kumuwezesha yeye Ali solih kuwa mtawala wa visiwa vya comoro.Ila hakuwa na ufahamu kuwa huyu Denard ndio atakuja kuuangusha utawala wake na kumuua.Wakati wa ujana wake ndio alikuwa kisoi na kwa kulipwa kile kiwango akitakacho basi angeliweza kufanikisha mapinduzi bila hofu.Kipindi hicho,baadhi ya nchi na viongozi wa kiafrika walikuwa wakimchukia gwiji huyu ila yeye hakuonyesha kushtushwa na chuki zao.Alikuwa mfaransa.Naam,mahasimu wa Ali solih walipo pata habari za mercenary huyu hawakusita kuwasiliana nae.Ahmed Abdallah raisi wa kwanza ambaye serikali yake ilipinduliwa na Ali solih na mfanyi biashara maarufu kipindi hicho Mohamed Ahmed waliungana huku serikali ya ufaransa ikitoa ridhaa na sapoti ili waweze kufanikisha mapinduzi haya.Bob Denard alihitaji kiasi cha pesa milioni mbili ili afanikishe kazi hii,na baada ya miezi mitatu Denard alikuwa ashajiandaa vilivyo pamoja na kikosi chake cha watu ishirini na tisa wengi wakiwa wafaransa na wabelgiji ambao nao walikuwa taharari na kutopea kweli katika communications na munitions.

Mnamo mwaka 1978 walisafiri kutoka ulaya hadi argentina kwenda kufanya mineral survey.Hii ilikuwa njama ya kuziba watu macho ili njama zao zisijulikane.Walipofika cape of Good Hope walibadilisha njia na kuingia comoro na kukita kambi katika hoteli ya grande comore,Hoteli kubwa comoro nzima.Ali solih tayari alikuwa ashapata fununu kuhusu kupinduliwa utawala wake,lakini jean Guilsou,mwana mercenery wa kifaransa ambaye hapo mwanzo alikuja comoro na Denard mwaka 1975 na kubaki kuwafunza mabody guard wake Ali solih akamhakikishia kuwa habari hizo zinatoka kisiwa kingine cha Anjouan.Ali solih hakujua kama huu ulikuwa ni mchezo anachezwa.Bila hata kufikiria akatuma kikosi cha majeshi watu wasiopungua 2000 na kuiacha moroni bila walinzi.

Usiku huo Ali solih alikuwa katika nyumba yake ya kifahari kama kawaida yake alikuwa akijivinjari na mabinti wawili pamoja na wakala flani wa kutoka ufaransa aliyejialika kuja kupiga gumzo na raisi.Wakati huu Bob denard alikuwa yupo ufuoni pamoja na wenzake wakisubiria simu.Haukupita muda Denard alipigiwa simu na kuarifiwa kuwa Ali solih alikuwa tayari keshalala.Kile kikundi cha ma mercenery kigajigawa vikundi vitatu.Kimoja kikatembea kwa miguu wakitumia bara bara ya ufuoni.Wengine wakaingia mtaa mpaka ilipo nyumba ya Ali solih.Na kikundi cha tatu kikaenda moja kwa moja hadi ilipo kambi,walimokuwa walinzi wa Ali solih.Baada ya muda mfupi wa kubadilishana risasi wale walinzi waliuawa.Kiufupi shughuli yote hii ilichukua masaa matatu na tayari taifa likawa lishatekwa na utawala wa Ali solih kupinduliwa.Ali solih akakamatwa.Wacomoro walilifurahia sana hili.watu walikuwa wakicheza na kuimba mitaani.Wiki mbili baadae,baada ya kurudi Abdulla visiwani comoro na kukaribishwa kwa mlahaka mkubwa,Solih alipigwa risasi na Denard ambaye alidai kuwa alikuwa akijaribu kutoroka.Kisha denard akuchukua mfu wa Ali solih na kuuweka nyuma ya land rover yake na kuisafirisha hadi kharthala alipokuwa akiishi mama yake.Mama yake na dada yake fatime walikuwa wakiusubiria mwili wake.Denard alipofika aliuburuta kutoka katika ile landrover yake na kuuacha uanguke chini.

Hiyo ndio iliyokuwa Hatima ya Ali solih,aliyekuwa raisi wa pili wa visiwa vya comoro.Ntakomea hapo wakuu karibuni muchangie.
 
Makala Safi kbs ila Ally Soilin alikuwa Rais wa Tatu wa Comoro. Baada Ahmed Abdallah kupinduliwa, urais ulishikwa na Sayyid Mohamed Jaffer El Amjad kuanzia Agosti 1975 hadi Januari 1976 alipopinduliwa na Ali Soilin...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Viongozi wa Nchi za Africa wana historia za kusisimua sn hasa baada ya nchi zao kupata uhuru wengi walijifanya miungu watu na kufanya ukatili wa kutisha kuliko hata wakoloni.............majuzi nimesoma historia ya Sheikh Abeid Amani Karume ilinisikitisha sana....m
Wa kwetu kajificha hapo chattel....
 
Makala Safi kbs ila Ally Soilin alikuwa Rais wa Tatu wa Comoro. Baada Ahmed Abdallah kupinduliwa, urais ulishikwa na Sayyid Mohamed Jaffer El Amjad kuanzia Agosti 1975 hadi Januari 1976 alipopinduliwa na Ali Soilin...

Sent using Jamii Forums mobile app
Raisi watatu mkuu,sijawahi mjua huyo sayyed mohamed labda itakuwa ni kwa sababu ya huo muda aliongoza,mwaka mmoja sio.
 
Viongozi wa Nchi za Africa wana historia za kusisimua sn hasa baada ya nchi zao kupata uhuru wengi walijifanya miungu watu na kufanya ukatili wa kutisha kuliko hata wakoloni.............majuzi nimesoma historia ya Sheikh Abeid Amani Karume ilinisikitisha sana....m
Wa kwetu kajificha hapo chattel....
Ahahaa,viongozi wetu Mkuu sijui wapi wanakwama mpaka sasa.Labda itakuwa ni ulimbukeni wa uongozi
 
Back
Top Bottom