Mjue Alfred Nobel (Muanzilishi wa Tuzo za NOBEL)

Deadbody

JF-Expert Member
May 30, 2015
4,276
6,585
1542442451317.png


ALFRED NOBEL



Utajisikiaje siku utakayo soma taarifa zako mbaya kwenye gazeti ? Nini watu watasema kuhusiana na wewe pindi utakapofariki?

Wakati wewe unafikiria na kuwaza kuwa haiwezani basi hali hii iliwahi kuwezekana kwa Alfred Nobel ambaye alibahatika kupata nafasi ya kusoma kuhusu kifo chake kwenye gazeti.

Hakupenda kabisa kile alichokiona kwenye gazeti

ALFRED NOBEL alikuwa mtu tajiri sana na mwenye mafanikio makubwa mno kwa wakati huo.Alikuwa mwanakemia na mgunduzi wa kemikali kuu tatu zinazohusika katika kufanya mlipuko hasa upande wa mabomu.Na ugunduzi wake huu ulimfanya kuwa moja ya watu tajiri Zaidi wakati huo.

Aligundua kemikali hizi
1.Dynamite
2.Gelignite(hutumika kwenye migodi)
3.Ballistite(bado inaendelea kutumika kwenye rockets)

Kutokana na kuwa na pesa nyingi aliamua kuinunua kampuni ya Bofors inayohusika na kutengeneza bunduki na hivyo kuendelea kuwa na utajiri wa hali ya juu.
Mnamo mwaka 1888,kaka yake na Alfred alifariki akiwa njiani kuelekea UFARANSA .Magazeti ya UFARANSA wakajua aliyefariki ni Alfred Nobel na wakachapisha gazeti lenye kichwa cha habari :

MFANYABISHA YA KUUA WATU AFARIKI
“Dr.Alfred Nobel ,ambaye amekuwa tajiri kwa kazi ya kuua watu kwa haraka sana kuliko kawaida amekutwa amefariki jana ”


Alfred Nobel alipoona gazeti hilo alipata mshangao mkubwa.”Kumbe hivi ndivyo watu wanavyoniongelea?”
“Kwahiyo hii ndio kumbukumbu nitakayoiacha duniani?”


Alfred Nobel wala hakulishitaki gazeti lile wala kushauriana na mtu yeyote kuhusu tukio lile na badala yake akaamua kuishi maisha ya kipekee yatakayomfanya aache kumbukumbu nzuri duniani siku atakayofariki.

Na hapo ndipo alipoamua kutumia utajiri wake kuleta mabadiliko.
Nobel akaanzisha mradi wake wa kwanza kwa $ 250 million kukopesha watu.Kila mwaka aliwashauri watu walifanikiwa kuzalisha na kuweza kusaidia wengine kwa kuwaongezea hela Zaidi.


Nobel akawa maarufu Zaidi.

Nobel akapanua Zaidi zawadi zake na kuwa na vipengele vingi sana kama zawadi za waliofanya vizuri kwenye sayansi,fasihi,na wanaochochea kuleta Amani.

Nobel ndio akafanikiwa kuiteka dunia na kuboresha tena tuzo hizi na kuziita NOBEL PRIZES (Yani tuzo za nobel) ambapo alitotoa kwa watu waliofanya vizuri kwenye sayansi,waandishi bora wa vitabu,wanaharakati ,waleta amani nk.


Tuzo za Nobel zilianzishwa mwaka 1895 na mwaka uliofuata muanzilishi wake akafa.

Tuzo za Nobel zilitimiza hitaji lake;zimeweka kumbukumbu mpya katika maisha yake na anakumbukwa sio kama “MFANYABISHA MUUAJI” Bali kama mtu mashuhuri kipenzi cha watu.

Alfred Nobel ni mfano mkubwa wa kuigwa ambapo anatufundisha kuwa hatujachelewa kabisa kubadili maisha yetu na kusaidia kuifanya dunia kuwa sehemu nzuri ya kuishi.

Deadbody
JamiiForums.
 
Back
Top Bottom