Mjomba Muhidin Maalim Gurumo ni Mgonjwa;

Mwawado

JF-Expert Member
Nov 2, 2006
993
252
Mzee Muhidini Maalim Gurumo ni mgonjwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Wodi ya Mwaisela,wodi No.5.Mzee Gurumo ni mmoja wa wakongwe wa Muziki alianza Muziki mwaka 1960 akiwa na Bendi ya NUTA.

Muhidini anasumbuliwa na kujaa maji katika mapafu.Wapenda Muziki,Ndugu na Jamaa tupite Hospitali kumfariji.Sala na maombi yetu yaelekezwa kwake,Ili apate nafuu na kurudi katika shughuli zake za kawaida.
 
Dah! Mjomba anaumwa?!!!!!!......SAD!
Mungu amjalie nguvu na mpe ulinzi.
 
Nimesikia hata yule daktari wa muziki Remmy Ongala naye kalazwa anasumbuliwa na kisukari,tumwombee kwa Mola amjalie afya nzuri.
 
Amefanya kazi nzuri isiyo na kifani toka 1960. Hakuisaliti fani amepitia mabonde na milima, umri hauna huruma namuombea Mungu amtazame kwa karibu yuko mioyoni nwetu
 
Mwenyezi Mungu Amjalie apone haraka Gwiji wetu wa muziki wa Dansi
Mmenikumbusha wimbo wake wa 'Tunawapongeza Wakulima wetu' wa miaka ya sitini
 
Mwenyezi Mungu Amjalie apone haraka Gwiji wetu wa muziki wa Dansi
Mmenikumbusha wimbo wake wa 'Tunawapongeza Wakulima wetu' wa miaka ya sitini



Dah, wewe Mkuu mwenzangu umenikumbusha mbali sana. Tuburudike pamoja basi.




'Tunawapongeza wakulima wetu leo,


Kazi yao kubwa wanayofanya mashambani
toka asubuhi jembe liko mkononi,
Tunawapongezaa.

Wafanyakazi twawategemea wao.
Wakishalima mazao tununue,
Tushiriki nao adui njaa tumuue hapa Tanzaniaa x2

(chorus)

Tuwape misaada yote oo waendelee,
Nafaka ziwe nyingi ee na wingi wa mazao,
Tushirikiane na wakulima adui njaa aende x2
 
Apone haraka Uncle Gulumo Mungu amjalie,

Utavamia wanfunzi wa mapenzi waikaange roho yako inyauke kama mti,malingo binti malingo nitakukumbuka daima. enheeee twende vipande vya uncle Gulumo
 
Tuache maneno ohooo ananikumbusha sijui nini, Mungu amjalie, pls wana jamii hospital ni gharama mnaeno hayasaidii tufanikishe hata mchango wa fedha za matibabu zimsaidie mzee wetu.

nawakilisha
 
"Cha cha mateso, nikufariki baba na mama, nimekuwa mkiwa, mbele ya ndugu zangu"

Hapo akiwa na marehemu TX, Suleiman Mbwembwe na wengineo katika wimbo "ukiona na mtu mzima analia" Mungu amjaze afya huyu mwamba.
 
Toka miaka ya 60 kweli mzee kapitia milima na mabonde katika kazi yake ya muziki. Mwenyezi Mungu amjalie afya njema.
 
Back
Top Bottom