Mjini tumeingizwa kwa pilau, pombe na kanga

mfereji maringo

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
1,037
250
MJINI TUMEINGIZWA KWA PILAU, POMBE NA KANGA
Wanakula na kusaza
Huku njaa watulaza
Siku nyingi mi nawaza
Lini twakoma ukilaza
Mjini tumeingizwa kwa pilau, pombe na kanga

Kura zetu waziwaza
Madaraka zawaingiza
Tumaini twapoteza
Maisha yanatukwaza
Mjini tumeingizwa kwa pilau, pombe na kanga

Mafisadi bongo wanatuliza
Mali zetu wanapuliza
Dhiki zetu wanapuuza
Utajiri kwao waukuza
Mjini tumeingizwa kwa pilau, pombe na kanga

Moyo nani atantuliza
Imani yangu kuisogeza
Iwe katika hili baraza
Uamerika au Uingereza
Mjini tumeingizwa kwa pilau, pombe na kanga
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom