Mji wa moshi

Ng'wale

JF-Expert Member
Nov 24, 2011
4,688
3,395
Kwa wale wenyeji wa Mji huu tafadhari, nimetembelea Moshi na ningependa weekend nipate sehemu ambapo naweza kupata moja baridi na moja moto mida ya jioni. Hii ni ktk kupeana ufahamu mpana wa mji na kuzijua sehemu ambazo hata ukitoka unasema nilifika Moshi. Asanteni.
 
pub alberto aisee kuna watoto nyololo nyololo sana,hapa utasuuza sana sii kupiga moja moto moja baridi
 
makao makuu ya ccm

Wewe kila kitu ni ccm tuu,inaelekea upo tayari hata kumtoa mkeo kwa makada wa kware wa ccm kama wakina Kapuya na wenzake.Sasa Mji wa Moshi na Makao makuu ya ccm yameingiaje,au lumumba mmeiamishia Moshi siku hizi?Shame on you.
 
Mkuu kama wewe ni Mpenzi wa kujirusha viwanja vipo vingi tuu Moshi,kuanzia Pub Alberto,Malindi,La liga,Avencha,Glaciers nk.Na kama ni Mpenzi wa mvurugo nenda zako pale mitaa ya Kiusa stand ya Maili sita ukale mvurugo wa uhakika. Na kama ni mpenzi wa Mbuzi Katoliki panda zako KCMC au Kibolironi,na kama unapenda mambo yetu yaleeeeeee,ukiweka kambi mitaa ya Malindi na Pub Alberto utang'oa mpaka wazungu kirahisi kabisa but make sure salio linasoma mfukoni kwa ajili ya Savanah,maana hapo kuna watoto wa MUCCoBS,KCMC,Mwenge na Masoka.
 
Njoo huku marangu kuna hoteli za kumwaga kuna marangu hot, caprico n, kibo hotel, na nyingine nyingi mwananchi kina yule mbuzi ktlk anapatikana bila kusahau kinuka mori wallah hutajutia hela yako
 
makao makuu ya ccm

hivi mbona hueleweki? Umeulizwa eneo zuri lenye kubeba sura nzuri ya mji wa Moshi ili akasimulie kwao wewe unamjibu aende makao makuu ya ccm. Hivi yalishahama dodoma? Au unashabikia ccm usiyoijua hata yalipo makao yake makuu?
Umevurugwa vibaya kiukweli. Kwa namna ya avatar yako (M23) yaonesha ni mtu wa vurugu sana na hata wewe binafsi unajivuruga! Nakushauri uende hospitali uonane na psychologist akusaidie kwani waelekea kubaya sasa.
Vinginevyo badilika kwani unafanya exhibition ya mind yako hapa kuwa huna kitu upstair.!
 
East african pub, kuna varieties za vyakula na vinywaji, kama unataka sehemu ya tofauti kidogo malindi si mbaya,pia kuna pub alberto night club na cool bar pembeni ake, makumba bay, Glaciers si mbaya pia. Ukitaka disco kuna club la liga kwakweli si mbaya utafurahi...karibu Moshi.
 
Wakuu shukrani wote kwa maelekezo mazuri, sasa hivi nipo Makumba bay nimepata mchemsho wa kuku. Kwa mtu ambaye anaelekeza kwenye ofisi za vyama, itabidi kumsamehe kwani lengo langu si kuchukua kadi ya uanachama, labda kama alimaanisha vinginevyo. Wengi 99.99% michango yenu nimeipokea na nitaifanyia kazi. JF ni uwanja wa elimu, tuzidi kuelimishana.
 
Mkuu kama wewe ni Mpenzi wa kujirusha viwanja vipo vingi tuu Moshi,kuanzia Pub Alberto,Malindi,La liga,Avencha,Glaciers nk.Na kama ni Mpenzi wa mvurugo nenda zako pale mitaa ya Kiusa stand ya Maili sita ukale mvurugo wa uhakika. Na kama ni mpenzi wa Mbuzi Katoliki panda zako KCMC au Kibolironi,na kama unapenda mambo yetu yaleeeeeee,ukiweka kambi mitaa ya Malindi na Pub Alberto utang'oa mpaka wazungu kirahisi kabisa but make sure salio linasoma mfukoni kwa ajili ya Savanah,maana hapo kuna watoto wa MUCCoBS,KCMC,Mwenge na Masoka.

Malindi imetajwa sana, panafaa kufika hapo angalau kwa kuanzia Kuburudisha macho kwanza, taratibu mengine yatajipa.
 
Malindi imetajwa sana, panafaa kufika hapo angalau kwa kuanzia Kuburudisha macho kwanza, taratibu mengine yatajipa.

Naikumbuka Moshi,

Kinywaji unapata Kindoroko Hotel halafu mbavu unapeleka Uhuru Hostel kwa raha na amani. Hivi Uhuru Hostel bado ipo?
 
Nami nimefika leo naona mzee wa Fresh Coach anaboresha pale round about mkabala na kahawa house. Juice matunda saafi,milo nk
 
Wakuu shukrani wote kwa maelekezo mazuri, sasa hivi nipo Makumba bay nimepata mchemsho wa kuku. Kwa mtu ambaye anaelekeza kwenye ofisi za vyama, itabidi kumsamehe kwani lengo langu si kuchukua kadi ya uanachama, labda kama alimaanisha vinginevyo. Wengi 99.99% michango yenu nimeipokea na nitaifanyia kazi. JF ni uwanja wa elimu, tuzidi kuelimishana.

Mkuu ameshindwa kujieleza tu huyo wa ccm. Nadhani alimaanisha karibu na stand ya maili sita. Pale pana kiwanja. Msameheni bure
 
Back
Top Bottom