Mji wa Luanda Angola Ndio Mji Wenye Maisha Ghali Afrika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mji wa Luanda Angola Ndio Mji Wenye Maisha Ghali Afrika

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Jul 1, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jul 1, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,611
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Mji wa Luanda nchini Angola Wednesday, June 30, 2010 12:36 AM
  Mji wa Luanda nchini Angola ndio mji ambao gharama za maisha ni kubwa kuliko miji yote barani Afrika, kwa duniani mji huo unashika nafasi ya tatu baada ya miji ya Tokyo, Japan na Oslo, Norway. Kwa mujibu wa takwimu za gharama za maisha katika miji mbalimbali duniani kwa mwaka huu wa 2010 zilizotolewa na ECA International, mji wa Luanda nchini Angola unashika nafasi ya tatu duniani kwa gharama za maisha.

  Katika takwimu za mwaka jana, mji wa Luanda ndio uliokuwa ukishika nafasi ya kwanza mbele ya miji mingi mikubwa duniani.

  Katika takwimu za mwaka huu, mji wa Tokyo Japan unashika nafasi ya kwanza ukifuatiwa na mji wa Oslo, Norway.

  Mjini Luanda nchini Angola, chakula cha mchana katika mgahawa wa saizi ya kati, kinagharimu dola 47, kopo moja la bia ni dola 1.62, kilo moja ya mchele ni dola 4.73 na dazani moja ya mayai hugharimu dola 4.75. Ukitaka kwenda sinema na mpenzi wako basi jiandae kutoa dola 13 kwa kichwa kimoja.

  ECA imetoa listi ya miji 65 duniani ambayo ndiyo inayoonekana ina gharama kubwa za maisha kwa kuangalia gharama za chakula, nguo, vifaa vya umeme na burudani.

  Katika listi ya miji 65 iliyolewa mji wa New York unashika nafasi ya 29 wakati jiji la Dar es Salaam limeshindwa kuingia kwenye orodha hiyo.

  Chini ni orodha ya miji iliyomo kwenye top 10.

  1:Tokyo
  2:Oslo
  3:Luanda
  4:Nagoya
  5:Yokohama
  6:Stavanger
  7:Kobe
  8:Copenhagen
  9:Geneva
  10:Zurich

  Chanzo NIFAHAMISHE Tanzania news portal .: Habari za Tanzania :.

  Kumbe Bongo Maisha Rahisi? Babu kubwa.
   
 2. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #2
  Jul 1, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Uchunguzi huo umeangalia hata vipato vya wakazi wa miji hiyo na nchi hizo?
   
 3. mfianchi

  mfianchi JF-Expert Member

  #3
  Jul 1, 2010
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 7,940
  Likes Received: 1,498
  Trophy Points: 280
  Usisahau kaka na kupata visa ya Angola ni sawa na ngamia kuingia kwenye tundu la sindano,utapata visa kiurahisi ya kwenda Uingereza au States lakini sio Angola na balaa zaidi ukiwa na jina la Kiislamu,pia jamaa wanachukia ngozi nyeusi kwani kule kwao mulato ndio everything.
  Yaani hawa watu tulio wasaidia kwa hali,mali na kumwaga damu zetu ukienda pale ubalozini kwao wanatuona kama takataka vile.
  Pia hata Sudan Kusini maisha yako juu sana na kila kitu kwa dola ,ndio maana Bongo naiona tambalale sana kimaisha tatizo ni hawa wanasiasa ndio wamekosa maono na ndio wanatupeleka pabaya,kazi yao nwanawaza kuongeza bei kwenye soda,bia ,sigara eti kwa kufanya hivyo ndio uchumi utakuwa ,huku wakiacha kilimo(Kilimo Kwanza ni pororjo za kisiaa)madini na rushwa teeelee,kisa mfadhili wa CCM.

  SERIKALI INAYOSHINDWA KUKUSANYA USHURU NI CORRUPT!NA HAIWEZI KUWALETEA MAENDELEO WANANCHI WAKE
   
 4. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #4
  Jul 1, 2010
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Sasa wewe ulitaka yawe magumu?
   
Loading...