Mji wa Jersey: Vita vikali vyasababisha mauaji ya watu sita

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,001
9,866
Afisa mmoja wa polisi na takriban watu watano wamefariki katika msururu wa makabiliano makali ya risasi katka mji wa Jersy katika jimbo la New Jersy.

Maafisa wawili wa polisi pia walijeruhiwa wakati wa kisa hicho , ambacho kilisababisha ufyatulianaji wa risasi baada ya watu hao waliojihami kujificha ndani ya duka.

Shule kadhaa na biashara zilifungwa kwa muda. Sababu ya kisa hicho haijajulikana. Mamalka inasema haiamini kwamba lilikuwa shambulio la kigaidi.

Mamlaka ilimtambua afisa wa polisi aliyefariki kuwa Joseph Seal mwenye umri wa miaka 39 ambaye alikuwa katika mpango wa kuwapokonya watu silaha haramu katika jimbo la New Jersy.

Akizungumza na ripota , afisa mkuu wa polisi wa mji wa Jersy Mike Kelly alisema kwamba bwana Seal alikuwa akiongoza maafisa wa polisi katika kuondoa bunduki haramu mitaani.

Bwana Kelly alisema kwamba ufyatulianaji wa risasi ulizuka kwa mara ya kwanza katika makaburi ya umma mwendo wa saa sita saa za Marekani.

Inaaminika kwamba bwana Seals aliuawa alipokuwa akiwakaribia washukiwa. Wawili hao walitoroka katika eneo hilo na kujificha katika duka moja la jumla ambapo waliendelea kuwafyatulia risasi maafisa wa polisi.

Makumi ya maafisa wa polisi , ikiwemo wale wa kitengo cha Swat na maafisa wengine walipelekwa katika eneo hilo na kusababisha mauaji ya watu watano katika duka hilo- huku wawili kati yao wakidaiwa kuwa washukiwa hao.


Maafisa wa polisi wanasema kwamba washukiwa hao walikuwa wamejihami na bunduki zenye uwezo mkubwa na walifyatua mamia ya risasi wakati wa kisa hicho.

Bwana Kelly alisema kwamba inaaminika watu watatu katika duka hilo waliuawa na washukiwa hao, na kusisitiza kwamba uchunguzi kamili utafanyika huku majibu yakichukua muda.

Mtu mmoja ambaye alinusurika anaendelea na matibabu , na gari lililotumiwa na washukiwa hao linachunguzwa na wataalamu wa kutegua mabomu.
1576039382905.png
 
Back
Top Bottom