Mji wa Ifakara ni mzuri kuliko Njombe mjini

Na ukienda Ifakara msimu wa kung'olelea mpunga (march mpaka Mei) aisee huwa kunapooza sana!

Yaani mishe mishe na kuchangamka ni wakati wa mavuno na kiangazi (Juni mpaka Disemba)! Mfano ukienda leo Ifakara, ni lazima utafurahia zile mishe mishe za watu. Ila baada ya hapo, kunadorora tena!
IMG_20211105_232337_413.jpg


Hii picha nilipiga msimu wa mvua
Kama kweli wewe umekulia Ifakara
Je hii mashine unaifahamu?
 
Wabunge wenu wachachamae ama sivyo CHATO itakuwa Mkoa kabla yenu!!! Kama mmekidhi masharti lazima mpewe haki yenu!
ifakala pale kuweka mkoa kwa sasa itakuwa hatari kwa bonde la mto kilombero
 
Chato kupata mkoa watulie labda wangekuwa wanatoka mkoa wa kigoma sababu zinazofanya wanyimwe mkoa ni sababubu za ubinafsi wa kamati ya mkoa wa kagera ndizo pia zilitokea shinyanga kahama kunyimwa mkoa lakini kahama ingekuwa ni sehemu ya tabora wangeshapewa mkoa ila kwa sababu wako shinyanga watulie tu
 
Kwan huwa wana angaliaga uzuri wa mji ?
Kuna vigezo na moja ya kihezo ni mapato ..sasa kama nyie hukonifakara ni wavivu kutoa kodi mpaka mkabweeeee embu mtulie kwa kuketi mwenyenacho huongezewa, mkono mfupi haurambwi, !!
Mkuu,Ifakara inaingiza mapato makubwa sana kwenye ushuru wa mazao ya chakula
 
Ifakara hii kumbe kuna watu wanaiona ipo juu mimi linaniudhi hili vumbi la ifakara na masaa karibu saba kutoka ifakara to morogoro mjini and vice versa
Hata Mbeya mjini kuna vumbi la poda lakini maisha yanaenda tu.

Vumbi ni sehemu ya nchi yetu
 
Wewe inaonekana hujawahi kufika Ifakara,
Ukiimaliza ifakara unaanza kukutana na misitu ya kufa mtu, mpaka maporomoko ya maji yapo yaani kiufupi mji upo msituni alafu ni ardhi ya maji maji (tindiga) hapafai kabisa kuishi huko,

Msimu wa mvua nilishuhudia nyumba zinamezwa na maji

Ukienda Malinyi ndio usiseme hovyo wilaya nzima inazingirwa na maji hakuna kutoka nje ya wilaya hata siku 5
Kule Marekani kuna majimbo ya Missisippi,Luisiana majimbo hayo kwa sehemu kubwa yamezungukwa na maji ya mto Misissippi na maisha yanaenda poa tu,mafuriko ni sehemu ya maisha ya binadamu.

Hata jangwani,Kigogo,Magomeni huwa kuna jaa maji
 
Kinachoufanya mji wa IFAKARA kuwa juu ni uwepo wa vitu vifuatvyo

1) Hospital kubwa ya Rufaa ya St.Francis Referral hospital

2) Chuo kikuu cha Afya St.Francis University College of Health and Alied science(SFUCHAS) kwa ngazi ya Udaktari na kozi zingine za Afya.

3) Taasisi ya utafiti (IHI) inayohusika na utafiti wa malaria,HIV ,TB na tafiti zingine kibao.

4) Chuo cha Udaktari kwa ngazi ya clinical officer kinachoitwa TTCIH

5) chuo cha Nersing Edger malanta school of nursing.

6) Hospital kubwa na ya pili kwa kutoa huduma ya kansa ukiachana na Ocean road na hii imefunguliwa mwaka jana wana mashine zote ikiwemo CT scan,Mammography,MRI na huduma zote za wagonjwa kansa, inaitwa GOOD SAMARITAN CANCER HOSPITAL IFAKARA.Ndo mana wagongwa wote wa kansa kwa kanda ya kati na kusini wanalazimika kwenda Ifakara kupata tiba badala ya Ocean Road unless kama mgonjwa ana option ya kwenda Ocean Road kwa sababu ya jina.

7) Chuo cha maendelo ya jamiii kilichopo kibaoni.

8) shule zenye ufaulu mkubwa kwa ngazi ya elimu ya sekondari zinaongoza kimkoa kama hiyo ya wasichana inayoitwa Benignis Sec school iliyopo jimboni mjini hapo..

9) kambi wa wagonjwa wa ukoma (leprosy rehabilitation centre)


Kwa hiyo unapoongelea kwanini Ifakara inakuja juu ni kwa sababu ya mwingiliano mkubwa wa watu kupitia taasisi hizo..

IFAKARA ibadilika kila siku ..ukienda leo na mtu atakayeenda week ijayo mabadiliko ni makubwa sana ..hebu jaribu kutathmini uwepo wa vyuo hivyo pamoja na taasis kubwa kubwa kwa mfano kituo kikubwa cha HIV/malaria kipo ifakara ..

Kule CDC/CDCI wameweka kambi kule...Ndo mana mji unakimbia kwa kasi ya ajabu sana...


WATU WANAZIDI KUWEKEZA KILA KUKICHA, KUMBI NA VIBE ZOTE ZA STAREHE ZIMEFUNGULIWA KULE.

sasa kwa mfano wanachuo wanapopata boom bata yote wanalia Ifakara huoni kwamba mji unachangamka sana kuliko sehemu ambazo hazina vyuo na taasisi hizo...?!!

ALL IN ALL Mji umefikia hadhi ya kuitwa manispaa kwa sababu ya population density pamoja na maendeleo...

MJI HUKUWA KWA KASI KUTOKANA NA HUDUMA ZA JAMII...mji ukikosa taasis au vyuo au shule kubwa kubwa lazima huchoka mapema..

ANgalia mfano wa wilaya ya Mbulu ambayo ndo wiliya ya kwanza kabisa Tz kwani kipindi inakuwa wilaya ndo mji wa mombasa ulipata kuwa mji pia ,lakini ndo wilaya ya mwisho kabisa kwa maendeleo inazidiwa na mji wake mdogo wa Hydom ambapo kuna hospital kubwa ya rufaaa ya Hydom Lutheran Hospital ..

Ukienda Hydom pamechangamka kuliko mbulu mjini hii inatokana na huduma zinazopatikana kule..vyuo vya afya pamoja na hospital ya rufaa zinapafanya hydom pachangamke kuliko mbulu mji...

LIKEWISE IFAKARA ..muda si mrefu inakuwa level za kahama au Babati mji..so uwepo wa huduma hizo unaifanya IFAKARA iwe wilaya ya kwanza kwa maendeleo mkoa mzima wa morogoro ukiachana na manispaa (mjini)...

Soon mkoa wa morogoro unaenda kudolola kama ilivyo kahama ndani ya Shinyanga..

So huhitaji kufanya Ubishi kama hujafika Ifakara these 3 passed years maendeleo ni makubwa sana..
Mkuu umeeleza vizuri sana.

Watu wengi ukiizungumza Ifakara hawajui Ifakara ni namna gani ilivyokubwa na ina ubora kiasi gani
 
Back
Top Bottom