Mji wa Ifakara ni mzuri kuliko Njombe mjini

Sasa mkuu huo Mji si unachangamshwa kibiashara na wageni! Hasa Wasukuma. Ila ukija kwa wenyeji, mambo siyo mepesi hata kidogo.

Nimeishi miaka mingi sana Ifakara. Ila ukiilinganisha na Njombe, naona kama Njombe iko juu zaidi ya Ifakara. Ifakara ingelinganishwa na Mji kama Kilosa vile, hakika Ifakara ingetisha mbaya.
Sawa Mkuu.
 
Kuanzia kibaoni,mjini hadi Lipangalala,mjini ni wa moto sana.
Hata harakati za kibiashara Ifakara ziko juu sana.

Ifakara iwe mkoa alafu wilaya zake ziwe Mlimba,malinyi,Ulanga(mahenge) na Kilombero(kidatu)
Kwanini isiwe mkoa wa kilombero HQ ni ifakara kama ilivyo kagera na bukoba au mara na musoma.
 
Mkuu njoo Ifakara ya leo,mji umejaa wahamiaji harakati za kibiashara zipo juu sana,miundombinu ya barabara ipo mjini hapa,idadi ya watu ni kubwa sana now days
 
Nakubaliana kuanzia mikumi kwenda kilombero, ifakara, mbingu,mgeta,mlimba malinyi kuwe na mkoa na makao makuu yawe pale Ifakara fikiria Kilosa inafika mpaka pale kwenye kiwanda cha sukari kilombero kama nipo sahii
Ndio ndio,yaani kunatakiwa kuwe na mkoa wa IFAKARA uwe na wilaya za Mlimba,Malinyi,Ulanga(Mahenge),wilaya ya Kilombero.
 
Kuna vigezo vinavyoangaliwa ili kupata hadhi ya Mkoa!! Njombe ni Mkoa kwasababu imekidhi vigezo hivyo ; na hapo Ifakara itapokidhi hivyo vigezo nayo itatunukiwa hadhi hiyo!!!
Hakuna vigezo vinavyofatwa,ni Siasa na upuuzi mtupu,Tabora ni kubwa zaidi ya Kagera,Geita,Kwa pamoja.
lakini wachawi wanataka waimege Kagera na Geita kutengeneza Mkoa wa Chato.Sasa sijuhi wataendelea kuigawa hii nchi mpaka lini?jambo la msingi lingekuwa kuunganisha mikoa,Kagera,Mwanza,Shinyanga.
Singida,Dodoma.Morogoro,pwani,Dar.
Lindi,Mtwara.
Tatizo wanasiasa kichwani hakuna kitu,hawana njia mbadala ya kuweka fedha kitaa,njia pekee ni kuongeza maeneo ya kiutawala,watendaji waongezeke,maana yake pesa itafika kitaa kupitia Malipo kwa hao watendaji watakao ongezeka.
 
Hivi inakuaje, Ifakara bado ni wilaya lakini Njombe ni mkoa? Maana Ifakara kuna maendeleo kuliko Njombe mjini.
Kwan huwa wana angaliaga uzuri wa mji ?
Kuna vigezo na moja ya kihezo ni mapato ..sasa kama nyie hukonifakara ni wavivu kutoa kodi mpaka mkabweeeee embu mtulie kwa kuketi mwenyenacho huongezewa, mkono mfupi haurambwi, !!
 
Shida ya ifakara ni moja tu mji umezungukwa na misitu alafu upo mbali sana
Ifakara ya wapi hiyo iliyo zungukwa na misitu! Bora hata ungesema mashamba ya mpunga!

Maana ukitoka nje kidogo tu ya mji, unakutana na mashamba ya mpunga. Au unaifananisha Ifakara na Mang'ula?
 
Ifakara ya wapi hiyo iliyo zungukwa na misitu! Bora hata ungesema mashamba ya mpunga!

Maana ukitoka nje kidogo tu ya mji, unakutana na mashamba ya mpunga. Au unaifananisha Ifakara na Mang'ula?
Wewe inaonekana hujawahi kufika Ifakara,
Ukiimaliza ifakara unaanza kukutana na misitu ya kufa mtu, mpaka maporomoko ya maji yapo yaani kiufupi mji upo msituni alafu ni ardhi ya maji maji (tindiga) hapafai kabisa kuishi huko,

Msimu wa mvua nilishuhudia nyumba zinamezwa na maji

Ukienda Malinyi ndio usiseme hovyo wilaya nzima inazingirwa na maji hakuna kutoka nje ya wilaya hata siku 5
 
Kinachoufanya mji wa IFAKARA kuwa juu ni uwepo wa vitu vifuatvyo

1) Hospital kubwa ya Rufaa ya St.Francis Referral hospital

2) Chuo kikuu cha Afya St.Francis University College of Health and Alied science(SFUCHAS) kwa ngazi ya Udaktari na kozi zingine za Afya.

3) Taasisi ya utafiti (IHI) inayohusika na utafiti wa malaria,HIV ,TB na tafiti zingine kibao.

4) Chuo cha Udaktari kwa ngazi ya clinical officer kinachoitwa TTCIH

5) chuo cha Nersing Edger malanta school of nursing.

6) Hospital kubwa na ya pili kwa kutoa huduma ya kansa ukiachana na Ocean road na hii imefunguliwa mwaka jana wana mashine zote ikiwemo CT scan,Mammography,MRI na huduma zote za wagonjwa kansa, inaitwa GOOD SAMARITAN CANCER HOSPITAL IFAKARA.Ndo mana wagongwa wote wa kansa kwa kanda ya kati na kusini wanalazimika kwenda Ifakara kupata tiba badala ya Ocean Road unless kama mgonjwa ana option ya kwenda Ocean Road kwa sababu ya jina.

7) Chuo cha maendelo ya jamiii kilichopo kibaoni.

8) shule zenye ufaulu mkubwa kwa ngazi ya elimu ya sekondari zinaongoza kimkoa kama hiyo ya wasichana inayoitwa Benignis Sec school iliyopo jimboni mjini hapo..

9) kambi wa wagonjwa wa ukoma (leprosy rehabilitation centre)


Kwa hiyo unapoongelea kwanini Ifakara inakuja juu ni kwa sababu ya mwingiliano mkubwa wa watu kupitia taasisi hizo..

IFAKARA ibadilika kila siku ..ukienda leo na mtu atakayeenda week ijayo mabadiliko ni makubwa sana ..hebu jaribu kutathmini uwepo wa vyuo hivyo pamoja na taasis kubwa kubwa kwa mfano kituo kikubwa cha HIV/malaria kipo ifakara ..

Kule CDC/CDCI wameweka kambi kule...Ndo mana mji unakimbia kwa kasi ya ajabu sana...


WATU WANAZIDI KUWEKEZA KILA KUKICHA, KUMBI NA VIBE ZOTE ZA STAREHE ZIMEFUNGULIWA KULE.

sasa kwa mfano wanachuo wanapopata boom bata yote wanalia Ifakara huoni kwamba mji unachangamka sana kuliko sehemu ambazo hazina vyuo na taasisi hizo...?!!

ALL IN ALL Mji umefikia hadhi ya kuitwa manispaa kwa sababu ya population density pamoja na maendeleo...

MJI HUKUWA KWA KASI KUTOKANA NA HUDUMA ZA JAMII...mji ukikosa taasis au vyuo au shule kubwa kubwa lazima huchoka mapema..

ANgalia mfano wa wilaya ya Mbulu ambayo ndo wiliya ya kwanza kabisa Tz kwani kipindi inakuwa wilaya ndo mji wa mombasa ulipata kuwa mji pia ,lakini ndo wilaya ya mwisho kabisa kwa maendeleo inazidiwa na mji wake mdogo wa Hydom ambapo kuna hospital kubwa ya rufaaa ya Hydom Lutheran Hospital ..

Ukienda Hydom pamechangamka kuliko mbulu mjini hii inatokana na huduma zinazopatikana kule..vyuo vya afya pamoja na hospital ya rufaa zinapafanya hydom pachangamke kuliko mbulu mji...

LIKEWISE IFAKARA ..muda si mrefu inakuwa level za kahama au Babati mji..so uwepo wa huduma hizo unaifanya IFAKARA iwe wilaya ya kwanza kwa maendeleo mkoa mzima wa morogoro ukiachana na manispaa (mjini)...

Soon mkoa wa morogoro unaenda kudolola kama ilivyo kahama ndani ya Shinyanga..

So huhitaji kufanya Ubishi kama hujafika Ifakara these 3 passed years maendeleo ni makubwa sana..
 
Wewe inaonekana hujawahi kufika Ifakara,
Ukiimaliza ifakara unaanza kukutana na misitu ya kufa mtu, mpaka maporomoko ya maji yapo yaani kiufupi mji upo msituni alafu ni ardhi ya maji maji (tindiga) hapafai kabisa kuishi huko,

Msimu wa mvua nilishuhudia nyumba zinamezwa na maji

Ukienda Malinyi ndio usiseme hovyo wilaya nzima inazingirwa na maji hakuna kutoka nje ya wilaya hata siku 5
Nimeishi Ifakara kwa muda wa miaka 18! Nimesoma huko kuanzia darasa la 1 mpaka kidato cha 6! Naifahamu nje ndani.

Ifakara haijazungukwa na misitu. Vile unavyo viona ni vichaka tu vidogo vidogo! Na siyo misitu. Mfano wa misitu ni kama ile iliyopo Wilayani Mufindi Mkoani Iringa (Misitu ya Sao Hill).
 
Back
Top Bottom