Mji wa Dar unahitaji kufungwa CCTV cameras

Mtuflani Official

JF-Expert Member
Dec 31, 2019
1,936
4,347
Waziri wa mambo ya ndani Uganda alipigwa risasi miezi kadhaa nyuma. CCTV cameras zilizofungwa jijini Kampala ziliwawezesha polisi kuweza kuwabaini na kisha kumuua mmoja na kukamata wengine.

Muda si mrefu hapo nyuma kuna mtangazaji wa ITV alikutwa amefariki maeneo ya Mwenge na mwili umetupwa barabarani. Zingekuepo CCTV cameras maeneo yale, mtuhumiwa angepatikana haraka sana.

Kuna msanii wa kundi la The Mafik alikutwa amefariki ametupwa barabarani huko Kunduchi, CCTV cameras zingekuwepo mtuhumiwa angepatikana.

Kuna jamaa mmoja habari yake ilizagaa sana miezi kama miwili nyuma. Alitoka benki na kisha akavamiwa na kupigwa risasi maeneo ya Mbezi Beach. CCTV cameras zingekuepo, watuhumiwa wangepatikana.

Maeneo ya flyover pale Ubungo kama unatokea Mlimani City, kuna uzio umegongwa na gari. CCTV cameras zingekuepo, mtuhumiwa angepatikana na kulipishwa faini.

Cameras hizi pia zingewasaidia trafiki kubaini vyanzo vya ajali mijini. Kuna watu wanagongwa na magari na kisha madereva kukimbia. Suluhu ni CCTV cameras
 
Samahani mtoa maada hivi CCTV camera ikifungwa tuseme kwenye ghorofa floor za juu juu je footages za kwenye barabarani zitaonyesha sura ya muhusika kweli au ndo kwa mbali Sana maana sijui zipo za Aina gani zenye uwezo
 
Back
Top Bottom