Mji wa Arusha Vuguvugu la Ukombozi wa Wanyonge Tangu Enzi za Nyerere. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mji wa Arusha Vuguvugu la Ukombozi wa Wanyonge Tangu Enzi za Nyerere.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gosbertgoodluck, Jan 5, 2011.

 1. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #1
  Jan 5, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Wakuu,
  Kinachoendelea Mjini Arusha kinatia uchungu na simanzi kubwa. Pamoja na mapungufu yake makubwa, katiba yetu ipo wazi kuhusu haki ya wananchi ya kuonyesha hisia zao kwa uhuru bila kusababisha uvunjifu wa amani kwa wengine. Uhuru huo wa kikatiba unafinywa na mafisadi kupitia vibaraka wao polisi. Wananchi wanapigwa mabomu ya machozi pasipo kosa lolote.

  Ujumbe wangu kwa jk na viongozi wote walio mstari wa mbele kuvuruga demokrais nchini, wawe makini wanaposhughulikia mikutano ya chadema hususan katika Mji wa Arusha. Wasipoangalia, hatma yao ni Mahakama ya Kimataifa. Arusha ni mji wa vuguvugu la ukombozi kwa wanyonge tangu wakati wa Azimio la Arusha ambapo Mwl. Nyerere aliwatangazia mafisadi wote kurejesha mali zao mikononi mwa wananchi. Kwa hiyo, kucheza na Arusha ni kuchochea ukombozi wa wanyonge. Punde si punde mafisadi watatafuta mahali pengine pa kuishi, siyo Tanzania.

  Mungu tuwezeshe watanzania tupate ukombozi wa kweli.
   
 2. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #2
  Jan 5, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Afrika ni vigumu kuendelea!
   
 3. m

  masaiti Senior Member

  #3
  Jan 6, 2011
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 197
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mbona nchi nyingine za Afrika zimeendelea? Angalia Botswana, Libya, Egypt, Tunisia etc. Hakuna kisichowezekana
   
Loading...