Mji mkuu wa Tanzania ni upi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mji mkuu wa Tanzania ni upi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tripo9, Oct 2, 2009.

 1. Tripo9

  Tripo9 JF-Expert Member

  #1
  Oct 2, 2009
  Joined: Sep 9, 2009
  Messages: 2,171
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Jamani Naomba mnifahamishe mji mkuu wa Tanzania yetu ni upi? Watu najua wamegawanyika. Watu wengi kutoka nchi nyingine watakuambia Dar es salaam. Hata mji wa Dodoma hawajui kama una-exist.

  Baadhi yetu tunajua ni Dar, miongoni mwetu tunajua ni Dom. Wengine tunasema miji yote hii miwili ni miji mikuu kama baadhi ya nchi duniani.

  Naombeni jibu la uhakika wakuu.
   
 2. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #2
  Oct 2, 2009
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Capital city = dodoma
  Commercial centre = dar
  Nchi nyingi zina mfumo kama huu. Mfano Marekani:NY na DC; Australia:Canberra na Sydney; Canada:Toronto na Ottawa; NZ:Wellington na Auckland....nk
   
 3. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #3
  Oct 2, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Ndg Mtoto, Samahani sioni similarity hapa, kwa namna fulani. Nijuavyo mimi White House ipo Washington na ndipo Ofisi ya Prezidaa wa US ilipo na amejikita kule. Sijawahi kusikia vinginevyo. Mifano mingine uliyoitoa sina hakika kama kuna similarity. Tanzania kila kitu kipo kinyumenyume, wizara na ikulu ipo Dar, na bila aibu watawala wetu wananadi kuwa Dodoma ndio mji mkuu, na ndio maana kuna ule usemi maarufu 'ONLY IN BONGO'.
   
 4. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #4
  Oct 2, 2009
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  hiyo its in reference to the commercial center of the city na mji mkuu. I guess wa kwetu unatatizo zaidi maana hata rais hathubutu kuishi humo...hahahaha!
   
 5. M

  MchungajiMakini Senior Member

  #5
  Oct 2, 2009
  Joined: Apr 4, 2008
  Messages: 192
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  mji mkuu wa tz ni dar er salam.

  lakini katika kuibiwa pesa nyingi kisiri ili kuujenga mji wa dodoma. sasa hii siri inatatanishwa bila ya kusema ukwele.

  watu walioiba pesa kuujenga mji wa dodoma na pesa hizo kuzitia kibindoni, sasa imekuwa kitatanishi

  lakini mji mkuu halisi ni dar

  suala muhumu wabunge we tu hawajui siasa wala historia
  na wengine wanaogopa kuwasema wakuu wao kwa mslahi yao bila ya kujali kuwa wao wamewekwa pale kwa masla ya wananchi na taifa kwa jumla sio kikundi fulani cha waheshimiwa
   
 6. Consultant

  Consultant JF-Expert Member

  #6
  Oct 2, 2009
  Joined: Jun 15, 2008
  Messages: 5,801
  Likes Received: 6,311
  Trophy Points: 280
  Viongozi wanasema MJI MKUU ni Dar es Salaam na MAKAO MAKUU ya Serikali ni Dodoma.
   
 7. K

  Kimweli JF-Expert Member

  #7
  Apr 9, 2012
  Joined: Oct 4, 2011
  Messages: 865
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 45
  Nimesikitishwa sana na ubovu wa barabara za mji mkuu wetu wa Tanzania-Dodoma, ni mbovu ile hadi aibu. CCM saidieni jamani kuuweka mji huu vizuri nawaomba muufikirie it is shame sana
   
 8. Adoe

  Adoe JF-Expert Member

  #8
  Apr 9, 2012
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 202
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Weka picha mkuu.
   
 9. Pharaoh

  Pharaoh JF-Expert Member

  #9
  May 7, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 843
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Sabah al kheri wazee wakuu.
  Naombeni tujadili hasara nchi hii inapata kwa kutapatapa eti mji mkuu uko Dodoma, hii hali inapotosha mpaka jamuiya ya kimataifa, kwani kwenye webs nyingi utaona mji mkuuu wa Tz ni Dodoma lakini chukulia wewe ni mgeni kabisa, utajaribu online kuangalia hiyo Dom yenyewe kila utakachocheki ni moja ya elfu ukilinganisha na miji kama Nairobi, kwa maana hiyo tunaoneka nchi iliyoko miaka elfu nyuma ya kenya ndugu zetu ambao sasa tunalingana tu kiuchumi.
  Pia hasara ya gharama za bunge na vikao vya serikali nzima kuhama kila mara na asilimia karibu yote ya wanasiasa wanaishi Dar
   
 10. mansakankanmusa

  mansakankanmusa JF-Expert Member

  #10
  May 7, 2012
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 4,093
  Likes Received: 603
  Trophy Points: 280
  JB Unalo nani aende mavumbini
   
 11. chakii

  chakii JF-Expert Member

  #11
  Jun 11, 2014
  Joined: Sep 15, 2013
  Messages: 16,471
  Likes Received: 14,165
  Trophy Points: 280
  Habari wana Jamii Forums,.

  Dodoma ilitangazwa kuwa Mji mkuu wa Tanzania mwaka 1973 , Pia ni makao makuu ya Chama Tawala CCM.

  Mji huu umepakana na mikoa ya Manyara, Morogoro, Iringa na Singida.

  Idadi ya watu kwa mwaka 2012 ilikuwa 2,083,588, Kiuchumi ni kilimo cha karanga, maharagwe, alizeti pamoja na ufugaji wa mifugo na kuku.

  Hali halisi ya makao ya kikazi ya Serikali ya Tanzania yako Dar Es Salaam pia Ikulu ya Rais.

  Lakini bunge hukutana Dodoma na Sehemu za ofisi za wizara kadhaa zimepelekwa Dodoma.

  My Take: Pamoja Na Mkoa Huu Wa Dodoma Kupewa Heshima Ya Kuwa Mji Mkuu Wa Tanzania Bado Maisha Ya Wakazi Wa Mji Wa Dodoma Yamebakia Kuwa Duni Miaka Nenda Rudi Huku Suala La Maji Likiendelea Kuwa Lulu Kwani Upatikanaji Wa Maji Umekuwa Suala Gumu Pia Lililokosa Suluhisho,.

  Serikali Inatakiwa Kufanya Kazi Ya Ziada Pamoja Na Kuanzisha Vitega Uchumi Na Kuhamasisha Uwekezaji Katika Mkoa Huu!!
   
 12. kabanga

  kabanga JF-Expert Member

  #12
  Jun 11, 2014
  Joined: Dec 12, 2011
  Messages: 29,807
  Likes Received: 3,702
  Trophy Points: 280
  Mkuu umepima vipi kuona maisha duni ya wakazi wa dom, maana mji wa dom ni ghali nao sasa....
   
 13. Excel

  Excel JF-Expert Member

  #13
  Jun 11, 2014
  Joined: Jul 8, 2011
  Messages: 18,888
  Likes Received: 565
  Trophy Points: 280
  Hivi ingekuwa vipi kama Bunge lisingekuwa linafanyikia Dodoma?
   
 14. m

  musami JF-Expert Member

  #14
  Jun 11, 2014
  Joined: Sep 16, 2011
  Messages: 1,420
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Hivi kwanini rais asiamie Dodoma,kwani tatizo ni nini?
   
 15. Kijana leo

  Kijana leo JF-Expert Member

  #15
  Jun 11, 2014
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 2,872
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 145
  nisaidie ni viashiria gani vinaonesha dodoma kuwa watu wake ni duni na umesahulika? halafu ndio nitatoa mchango zaidi, kwa sababu mimi ninaujua mkoa huo sana.
   
 16. mrangi

  mrangi JF-Expert Member

  #16
  Jun 11, 2014
  Joined: Feb 19, 2014
  Messages: 22,017
  Likes Received: 9,306
  Trophy Points: 280
  kwwli kabisa mleta uzi sana sana ukienda dodoma vijijini ndiyo balaaaaa maishaaa yako chini sana maji tabu n.k
   
 17. SPANISH CP

  SPANISH CP JF-Expert Member

  #17
  Jul 11, 2014
  Joined: Apr 5, 2014
  Messages: 466
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Dodoma h mji mkuu wa Tanganyika,leo ndio wamefanya sherehe za uzinduzi wa taa za kuongozea magari.
   
 18. Makamee

  Makamee JF-Expert Member

  #18
  Jul 11, 2014
  Joined: Nov 29, 2013
  Messages: 2,005
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 145
  Inawezekana ikawa ndio sababu za mawaziri kukataa kuishi huko?
   
 19. Heaven on Earth

  Heaven on Earth JF-Expert Member

  #19
  Jul 11, 2014
  Joined: Mar 21, 2013
  Messages: 37,073
  Likes Received: 4,741
  Trophy Points: 280
  mji mkuu wa Tanganyika au Tanzania???
   
 20. kabanga

  kabanga JF-Expert Member

  #20
  Jul 11, 2014
  Joined: Dec 12, 2011
  Messages: 29,807
  Likes Received: 3,702
  Trophy Points: 280
  yeah..najamaa wanasimania mbaya...
   
Loading...