Mji mkuu wa Burundi, Bujumbura umefanana na mji gani hapa Tanzania?

Drone Camera

JF-Expert Member
Jul 25, 2017
14,007
13,797
Habari wakuu,

Kama kichwa kinavyojieleza ningependa kufahamu jiji la Bujumbura limefanana na mji au jiji gani hapa kwetu.

Kuna ripoti naiandaa hivyo kwa wale wenye uzoefu na huko ningependa kusikia kutoka kwenu.

Ningependa kufahamu kiuchumi, miundombinu, majengo, vitu kama shopping centers na mambo mengine jiji hilo limefanana na mji au jiji gani huku kwetu.

NB: Kama umetembelea Bujumbura na mji/jiji utakalotaja kwa siku za karibuni itapendeza zaidi.

Regards.
==================
Updates
Mmoja kaniambia Mwanza jiji
Mwingine Sengerema
Mwingine kasema Dodoma
Ila wengi wamesema Kahama
Ripoti naiandika kesho saa tatu hivyo naendelea kusikiliza ushauri wenu kwangu.
Asanteni.
==============
Final updates:
Asanteni wakuu kwa michango yenu.Nimeamua kuchagua Mwanza japo inaweza kuwa mbele kiuchumi ila kuna vitu vimematch jambo ambalo ni tofauti na hiyo miji mingine.
Shukrani sana kwa michango yenu.
Bujumbura

2417447_Bujumbura.jpg

1558224_MwanzaCity-29.jpg

Mwanza
 
Naam

Bujumbura zamani ikifahamika kama Usumbura ni mji mkuu na jiji lililokuwa bora lenye kuhodhi makao makuu ya nchi. Jiji hili ni sawa na Mwanza kwa asilimia 92%

Bujumbura iliyojengeka kijiografia analalia upande wa Ziwa Tanganyika (Magharibi) jiji hili linayo bandari salama ya ziwa na huduma nyingi za kuingiza zikitoka Tanzania.

Shughuli za kiuchumi ndani ya Bujumbura ni zao la kahawa, uchakataji karatasi, madini ya ore, viwanda vya kemikali na mazao mbalimbali, sabuni na mavazi.

Uwapo Bujumbura hutojuta maana kwa asilimia kubwa raia wa Bujumbura huzungumza KiSwahili na Kifaransa pia Kiingeleza.

Hii ndio Bujumbura
 
Nilisahau kukutag mkuu! Shukrani sana
 
Mmoja kaniambia Mwanza jiji
Mwingine Sengerema
Mwingine kasema Dodoma
Ila wengi wamesema Kahama
Ripoti naiandika kesho saa tatu hivyo naendelea kusikiliza ushauri wenu kwangu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom