Mji Mdogo Usa-River: Mbio za Uchaguzi Wenyeviti wa Mitaa/Vitongoji Novemba 2012

Emashilla

Senior Member
May 24, 2012
138
26
Baada ya Usa-River kupata hadhi ya kuwa Mji Mdogo, Serikali imepanga kufanya uchaguzi baada ya Wenyeviti waliopo madarakani kumaliza muda wao kisheria.
Kwa hiyo:-
1. Mchakato wa vyama kupata wagombea unaanza leo 04.10.2012 na kukamilika 11.10.2012.
2. Uandikishaji wapiga kura itakuwa ni 17.10.2012 hadi 23.10.2012
3. Kampeni za Wagombea ni kwa siku saba kuanzia 28.10 hadi 03.11.2012
4. Siku ya uchaguzi itakuwa 04.11.2012
Vyama vya siasa vinavyotarajiwa kusimamisha wagombea ni Vyama Nane. AFP, CCM, CHADEMA, DP, NRA, SAU, TLP na UPDP.

CHADEMA NA CCM NANI ZAIDI KATIKA UCHAGUZI HUU?


Source: Ratiba ya Uchaguzi toka Mamlaka ya Mji Mdogo Usa-River
 
Fanyeni Uhamuzi wa busara kama mlivyofanya kwa Kamanda Nassari mpeni watendaji katika ngazi ya chini ili aweze kutekeleza ahadi zake vizuri coz currently watendaji wa CCM wanamkwamisha ili aonekane hakufanya kitu.:poa
 
Ushauri wangu bila kujali itikadi, hamasisheni sana watu kujiandikisha maana kampni huwa hazina maana kama watu hawajajiandikisha. Kampeni kubwa inafanyika katika kuandikisha watu.
 
Ushindi upo kwa CHADEMA. Uchaguzi wa wenyeviti wa Mitaa/Vitongoji utafanyika Novemba 4, mwaka huu 2012. Habari ni kwamba CCM wamekataa kabisa kuchaguliwa. Hivyo, waacheni!

Nasikia kawaida ya CCM ni kutoa rushwa katika chaguzi. Je! CCM watafanikiwa katika njama zao za kununua wapiga kura?
 
Kwani utaratibu wa kuwachagua hao viongozi si unaeleweka? Na kama ccm wamekataa kuchaguliwa wanataka achaguliwe nani tofauti na cdm?
 
Kwani utaratibu wa kuwachagua hao viongozi si unaeleweka? Na kama ccm wamekataa kuchaguliwa wanataka achaguliwe nani tofauti na cdm?

Ndiyo, utaratibu ni watu kujiandikisha kuanzia Jumamosi 13/10/2012 hadi 20/10/2012. Lakini, CCM kukataa kuchaguliwa si kwa kusema bali kwa matendo yao wamepoteza sifa za kuongoza nchi hii katika ngazi zote. Ridhaa walipewa kwa miaka mingi sana, lakini leo wanatuonesha kuwa uongozi ni bidhaa na bei yake ni thamani ya RUSHWA. Nasisitiza, CCM hawataki kuchaguliwa kwa nini tuendelee kuwabembeleza? Waacheni!
 
Ndugu yangu unauliza jibu!! ndio maana yake CHADEMA ni chama DUME! linapiga kotekote! magamba chalii! kifo cha mende! miguu juu!
 
Huo utakuwa mwanzo wa ukombozi kwa watanzania, ushindi unaanzia katika ngazi ya chini yaani mtaa.
 
Back
Top Bottom