Mzee wa Gumzo
Senior Member
- Apr 21, 2008
- 197
- 5
Mwanajeshi Dar adaiwa kumuua mkewe kwa kummiminia risasi
2008-07-29 20:47:01
Na Mwanaidi Swedi, Kinondoni
Askari wa Jeshi la Wananchi Kambi ya Lugalo, anadaiwa kumuua mkewe kwa kummiminia risasi kadhaa mwilini, ikiwa ni pamoja na sehemu za kichwani na mkononi.
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni Mark Kalunguyeye, amesema tukio hilo limetokea jana majira ya saa 3:00 usiku katika eneo la Lugalo ambako askari huyo alikuwa kwenye lindo lake.
Kamanda Kalunguyeye amesema kuwa askari huyo aliyefahamika kwa jina la Bw. Festo Benjamin, akiwa lindoni, mkewe aliamua kumfuata kwa mazungumzo yao.
Aidha, Kamanda Kalunguyeye amesema kuwa inasemekana kuwa katika mazungumzo yao hayo, wapendanao hao walishindwa kuelewana na ndipo askari akaamua kumtwanga risasi ya kichwa na mkononi mkewe huyo na kumuua papohapo.
Kamanda Kalunguyeye amesema baada ya kuona kuwa ameemua mkewe, askari huyo aliamua kujisalimisha mwenyewe Polisi ambapo na hadi sasa anashikiliwa kwa mahijiano zaidi kabla ya hatua za kisheria kufuatia.
SOURCE: ALASIRI
Taarifa zinaeleza kuwa kutokuelewana kwao kulitokana na mume kubamba meseji za kimapenzi kwenye simu ya waifu.
Mimi nawashauri wanaume wenzangu tuchukue ushauri kwenye "LONGA MWANAMUME" ITV kila jumatano saa tatu kamili.Kwanini ujisababishie mipresha bure?
Aka mie!