Mjengwablog Iliibua Kashfa Ya Pan African Energy Siku Tatu Kabla Ya Hotuba Ya Ngeleja! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mjengwablog Iliibua Kashfa Ya Pan African Energy Siku Tatu Kabla Ya Hotuba Ya Ngeleja!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by maggid, Nov 19, 2011.

 1. m

  maggid Verified User

  #1
  Nov 19, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Ndugu zangu,
  Nafurahi kuwajulisha, kuwa Mjengwablog. com ndio iliyoibua kwa mara ya kwanza kashfa ya mradi wa gesi unaouhusisha kampuni ya Kisweden ya Pan African Energy , Tanesco na Wizara ya Nishati na Madini.

  Habari kuhusu kashfa hiyo ziliripotiwa kwa mara ya kwanza hapa nchini na blogu hii Ijumaa ya Julai 15, 2011. Ni siku tatu kabla ya Waziri Ngeleja kuwasilisha bajeti ya Wizara ya Nishati Na Madini. Bila shaka yeyote, habari hiyo ilichangia kwenye kuongeza nguvu ya mjadala bungeni. Hapa chini ni habari husika niliyoiposti hapa globuni na kwenye mitandao mingine kama vile Global Publishers, Jamii Forums na Wanabidii. Pichani juu Waziri Ngeleja akipongezwa na wabunge wenzake wa CCM baada ya bajeti ya wizara yake kupitishwa. Ilikwamishwa ilipowasilishwa kwa mara ya kwanza.
  Mheshimiwa Ngeleja, Sweden Kuna Kashfa Ya Nishati Yetu

  Ndugu zangu,

  Waziri wa Nishati na Madini Mheshimiwa William Ngeleja leo anawasilisha bajeti ya wizara yake huku kashfa ya nishati yetu ikiwa ni moja ya ajenda ya shirika la Misaada la Kimataifa la Action Aid lenye tawi lake nchini Sweden.

  Shirika hili linaishinikiza Serikali ya Sweden kuacha kufadhili kwa kuyapa mitaji ya kuwekeza makampuni yenye kukwepa kodi kama ilivyo kwa kampuni ya Pan African Energy.

  Kampuni hii Pan African Energy iliyosajiliwa kwenye visiwa viwili; Mauritius na Jersey inavuna gesi ya Songosongo huku ikiwa imeingia mkataba wa miaka 25 na TANESCO kupitia Shirika la Nishati ina Madini la Taifa TPDC. Ni mkataba wenye kuifanya kampuni hiyo kutokulipa kodi ya faida ya mapato wanayopata kutokana na mauzo ya umeme unaotokana na gesi asilia wanayovuna Songo Songo.

  Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Action Aid iliyotolewa mwezi Mei mwaka huu, tangu Pan African Energy waanze kuvuna gesi asilia kule Songo Songo mwaka 2004, kampuni hiyo imevuna faida ya zaidi ya dola za Kimarekani milioni 60. Nusu ya faida hiyo ilipatikana mwaka 2009 na kampuni hiyo ilitarajiwa kuongeza uzalishaji. Hivyo, kuvuna zaidi gesi yetu asilia ya Songosongo.

  Mpaka kufikia sasa, Pan African Energy imefanikiwa kukwepa kodi inayokadiriwa kufikia dola za Kimarekani milioni 40. Hiki ni kiasi cha fedha kinachotosha kusomesha watoto wa Kitanzania 175,000 ( Laki moja na sabin ina tano elfu) kwa mwaka kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Action Aid.

  Kwa kifupi tu, ripoti hii inadhihirisha namna ufisadi unavyochangia kutuacha Watanzania tukiwa katika hali ya giza linalotokana na mgawo wa umeme. Tukiwa katika hali ya uzalishaji duni kutokana na uhaba wa nishati ya umeme. Ufisadi umetuletea giza na umasikini.

  Kampuni hii ya Pan African Energy inanufaika na 'mkataba wa kifisadi' usiotanguliza maslahi ya taifa.
  Ni wakati sasa wa Waheshimimiwa wabunge wetu ' kumweka kikaangoni' Waziri wa Nishati na Madini Mh. William Ngeleja ili atoe maelezo ya kina juu ya kashfa hii ya Pan African Energy. Na atwambie, ni hatua gani zitachukuliwa na lini kwa wote waliochangia kutufikisha kwenye kashfa hii. Hivyo basi, waliochangia kutufikisha katika giza hili tunalolishuhudia sasa kwa kukosa nishati hii muhimu kwa maana ya umeme.

  Kama Mheshimiwa Waziri atashindwa kutoa majibu ya kuridhisha, basi, aombwe akae pembeni kupisha Watanzania wengine wenye uwezo wa kushika Wizara hiyo nyeti kwa taifa.

  Nawasilisha.

  Maggid
  Knivsta, Sweden
  Ijumaa, Julai 15, 2011
  http://mjengwa.blogspot.com

  ( Unaweza kusoma ripoti ya Action Aid kwenye; http://www.actionaid.se)
   
 2. M

  Madcheda JF-Expert Member

  #2
  Nov 19, 2011
  Joined: Feb 18, 2009
  Messages: 416
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  safi sana majjid tunahitaji watu kama nyie milioni 5 hivi ili hii nchi isonge aise
   
 3. jamii01

  jamii01 JF-Expert Member

  #3
  Nov 19, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 1,836
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  ila wewe ni mmoja ya watu wanafaki sana Tanzania na Blog yako.
   
 4. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #4
  Nov 19, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,701
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  safiii,safi sana,fichua mengine zaidi ya hayo.Nalog off
   
 5. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #5
  Nov 19, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Sasa kama wewe ndiye uliyeliibua kwa mara ya kwanza kuandika hivyo maana yake nini au ili kiwe nini? Ruhusu watu wengine wakusifu usipende kujitengenezea misifa/kujisifu. Utazidi kudharaulika.
   
 6. T

  The Priest JF-Expert Member

  #6
  Nov 19, 2011
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 1,026
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Hivi ile blog yako kumbe bado ipo?
   
 7. Kibukuasili

  Kibukuasili JF-Expert Member

  #7
  Nov 19, 2011
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 858
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Halafu?
   
 8. tz1

  tz1 JF-Expert Member

  #8
  Nov 20, 2011
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 2,118
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  Mbona una mwonea mzungu
   
 9. M

  Mpambanaji K Member

  #9
  Nov 20, 2011
  Joined: Dec 29, 2008
  Messages: 84
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Big up Maggid. Unastahili pongezi kwa ku-whistleblow ufisadi was Pan African Energy. One thing though ile website uliyotuelekeza kupata report yote imeandikwa kiswede. do you have any idea on how one can access english version of the report?

  Much thanks
   
 10. M

  Mpambanaji K Member

  #10
  Nov 20, 2011
  Joined: Dec 29, 2008
  Messages: 84
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Hongera Maggid. you and your blog deserve kudos for revealing what has come to be a topical issue today-ufisadi. website uliotuonyesha ni ya kiswede. can you assist on how to access the english version?
   
 11. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #11
  Nov 20, 2011
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,083
  Likes Received: 4,032
  Trophy Points: 280
  Si umesoma pia toka Action Aid? Kwanini unapenda sifa wewe ulipo-translate kitabu cha Obama ukadai umekiandika na sasa umesoma na kutranslate ulichosoma sasa unadai hiyo habari yako! Lini utajifunza ku-acknowledge the sources? Wewe kama wewe huna uwezo wa kuwa na detailed information za TPDC, Pan Africa na Wizara ya Nishati na Madini haswa za hapa Tanzania kwa ukiritimba wa mikataba kwa jinsi inavyofichwa! Anyway at least umeitaja Action Aid
   
 12. gango2

  gango2 JF-Expert Member

  #12
  Nov 20, 2011
  Joined: Aug 31, 2011
  Messages: 1,237
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180

  okey sasa unatujulisha ili iweje?? mbona hujiamini na kazi yako kaka???? always watu ndo wataodetermine kuwa ur blog is best not u

  so usitangaze this kama matangazo ya biashara/??
   
 13. kirumonjeta

  kirumonjeta JF-Expert Member

  #13
  Nov 20, 2011
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 3,095
  Likes Received: 502
  Trophy Points: 280
  At least Bw.Mjengwa blog yako inaendelea vizuri mi nilishaachaga kuitembelea maana kila siku ilikuwa ni mstori tuuuuuuu hazina kichwa wala miguu.Kwa hili nakupongeza ila usimfuate mwenzio kushabikia MAGAMBA TUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUU.
   
Loading...