Mjengwa:Nimepumzika Kuandikia Rai Mwema | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mjengwa:Nimepumzika Kuandikia Rai Mwema

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by magoma, Mar 5, 2009.

 1. m

  magoma New Member

  #1
  Mar 5, 2009
  Joined: Mar 2, 2009
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii nimeisoma mjengwablog;

  Nimepumzika Kuandikia Raia Mwema
  Kwa wasomaji wa makala zangu,

  Baadhi yenu mmeshangaa kutonisoma kwenye ' Raia Mwema' toleo la jana. Nawajulisha kuwa nimepumzika kuliandikia gazeti la Raia Mwema ili niweze kuwaongoza wenzangu tulioshiriki kuandaa gazeti la Gozi Spoti ( Halipo tena mitaani) kujipanga upya kwa kutumia uzoefu tulioupata.

  Tayari nimeshamjulisha Mhariri wangu ( Raia Mwema) kaka John Bwire juu ya uamuzi wangu huu. Natumia fursa hii kuwashukuru kwa dhati ndugu zangu wa 'Raia Mwema' kwa kunipa fursa ya kuandikia gazeti hilo. Nimekuwa nikiandika bila kukosa tangu toleo la kwanza. 'Raia Mwema', kama ilivyokuwa kwa gazeti la 'Rai', limenisaidia kuifikia jamii pana ya Watanzania. Nimetengeneza mahusiano mema na Watanzania wengi wa ndani na nje ya nchi. Katika muda wangu na ' Raia Mwema', nimejaribu kwa uwezo wangu wote kuitumikia jamii yetu kupitia kalamu yangu. Nami nimejifunza mengi kupitia wasomaji wa gazeti hilo.

  Naam. Nimepumzika. Kwa sasa nitabaki kuwa msomaji wa ' Raia Mwema'.
  /Maggid
   
 2. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #2
  Mar 5, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,573
  Likes Received: 18,468
  Trophy Points: 280
  Uamuzi huo wa Mjengwa si bure, kuna jambo!. Naamini it has something to do with safari ya kuelekea 2010. Kwa mawazo yangu, haiwezekani Mzee wa Makala tangu enzi na enzi akizungumzia mambo ya siasa, uchumi na jamii ghafla akabwaga manyanga eti kisa anataka kuimarisha kijarida cha 'Gozi Spot' ambacho kiko limited kwenye michezo.

  Naamini ama anajipanga kuibukia gazeti jingine, ama dhamira yake itamsuta.

  Mimi ni mmoja kati ya wanunua magazeti kwa ajili ya makala mbalimbali, kwa sisi wasomaji wa makala zake, kutuacha just like that, 'its a betrayor'
   
 3. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #3
  Mar 5, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Hata "Gozi Spoti" alitangaza kwa blogu yake kuwa wameliondoa kutoka orodha ya msajili tarehe 19/02. Hivyo nadhani kama wana jipanga kuanzisha Gazeti kamili litakaloripoti masuala yote (Siasa, biashara nk) na si michezo peke yake.
   
 4. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #4
  Mar 5, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  tumpongezee kwa kujipanga upya kwani huo ndo mwanzo wa kupanuka zaidi kwa kufungua milango mingi...

  maggid natumai bado una nia ya dhati ya kuendelea kuburudisha, kuelimisha na kusasahisha jamii yetu inayojaribu kujenga uwezo wa kupambanua zaidi mambo kwa mustakabali wa taifa hili...

  HONGERAAA...
   
 5. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #5
  Mar 5, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Hongera mjengwa kujiondoa kwa mazuri ni changamoto kwako na kwa wengine pia
   
 6. B

  Baija Bolobi JF-Expert Member

  #6
  Mar 5, 2009
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 931
  Likes Received: 697
  Trophy Points: 180
  Hii ina harufu ya 2010 au makundi ya CCM yanajaribu kuingia Raia Mwema. Kumbuka Afisa Mahusiano wa Richmond (Salva Rweyemamu) alikuwa Rai na Mjengwa. Rai ilipouzwa kwa Rostam, Salva akaenda Ikulu kwa kufanikisha uuzaji wa Rai, na ndipo Mjengwa akahama na Jenerali kwenda Raia Mwema. Hivi sasa JK na kundi lake wanatafuta namna ya kuyapunguza nguvu magazeti "hostile". Linalokataa kununuliwa, ananunuliwa mwandishi. Sisemi Mjengwa amenunuliwa, lakini Tanzania yetu, kila mtu ana bei, na pungufu unaongea mwenyewe!

  Kwa nini hakuwaaga wasomaji wake ndani ya makala ya mwisho anakuja kuaga kupitia blogu?
   
 7. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #7
  Mar 5, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Maggid.
  Yaelekea anayosema huyu ndugu yangu baija bolobi ni kweli. Unaweza kuja hapa kujitetea? Vinginevyo tutaendelea kuamini haya huyu bawana aliyosema maana yanaonekeana yako karibu na ukweli.
   
 8. Companero

  Companero Platinum Member

  #8
  Mar 5, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  - Raia Mwema Hakati Tamaa
  - Raia Mwema Husema Ukweli
  - Raia Mwema Hasaliti watu
  - Raia Mwema Hapokei Rushwa
  - Raia Mwema Haachi Mbachao
   
 9. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #9
  Mar 5, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  2010?
   
 10. The Invincible

  The Invincible JF-Expert Member

  #10
  Mar 5, 2009
  Joined: May 6, 2006
  Messages: 4,722
  Likes Received: 1,212
  Trophy Points: 280
  Au ndio kama yale ya Deodatus Balile kuacha Tanzania Daima? Walau yeye aliaga kwa makala kwenye gazeti alilokuwa anaandikia.
  Mmmmhhhh!
   
 11. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #11
  Mar 5, 2009
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,793
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  ...mmmm, nina wasiwasi na aliyeileta post hii! Post ya kwanza tu habari ya Mjengwa?? Ama ndio wewe mwenyewe????
   
 12. Sasha Fierce

  Sasha Fierce JF-Expert Member

  #12
  Mar 5, 2009
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 362
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  If i remember correct kuna wakati fulani hata mzee Mwanakijiji alishawahi kutangaza kuwa anapumzika kuandika katika gazatte fulani lakini sikumbuki haswa lilikuwa ni gazeti gani fikira zangu zinaniambia ni huyo huyo raia Mwema je na yeye anajiandaa for 2010?
   
 13. B

  Baija Bolobi JF-Expert Member

  #13
  Mar 5, 2009
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 931
  Likes Received: 697
  Trophy Points: 180
  Yeye hakusubiri 2010, alianza baada ya kutangaza na anafanya vizuri kabla hata ya kuchaguliwa.
   
 14. l

  lageneral Member

  #14
  Mar 6, 2009
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mjengwa,
  Umetuangusha wapiganaji wenzako.Nilishaona dalili wapi unaelekea baada ya makala kama iliyokuwa ikimsifia JK kuwa anakatiza mitaani Bagamoyo kwa miguu,kuwa JK mtu wa watu.
  Kama Balile,baadaye tutajua wapi ulipo hata ukitumia jina bandia.Au kasheshe za ngurumo zimekutoa mbio?
   
Loading...