Mjengwa katika kampeni za Kikwete 2010?

Wakuu naona we are missing the point hapa.

Jamaa amedeclare katika opening statement kuwa ni "tathmini yake binafsi",... hajajumuisha watanzania wote kwenye huu mtazamo wake. Sasa huku kufoka povu kote
kunatokea wapi?....
Ofcourse he is entitled to his opinion as an individual,...angekua ametujumuisha watz wote kwenye huo mtazamo wake,... tungekua na haki ya kumshambulia.

I dont necessarily share his opinion but still, nahisi we are missing the point kwa kumtolea personnal attacks as if watu mnataka kusettle nae scores za zamani hapa.

Kina Karl Rove wataendelea kuwepo tu, cha kufanya ni kujenga counter hoja za hiyo
mitazamo yao instead of personal character assasinations.

Ni hayo tu wakuu.

What point are we missing?Kwani personal opinion haiwezi kuwa wrong?Na personal opinion ikiwa wrong haiwezi kuwa criticized?I think you are the one missing a point kwa kuzungumzia settling old scores as if there was any!

Baada ya kufungiwa Mwanahalisi,Raia Mwema limebaki kuwa weekly pekee la "kuaminika".Misimamo ya akina Johnson Mbwambo,Ayoub Rioba,Ulimwengu,nk inafahamika vizuri.Mjengwa amekuwa anayumba kimsimamo,na makala zake zinaweza kuonekana out of place.Nakumbuka makala yake ya kumkosoa Ansert Ngurumo kuhusu wananchi walioupopoa mawe msafara wa JK huko Mbeya.Kwa hakika haikuwa na mantiki yoyote zaidi ya kupinga hoja za maana za Ngurumo.

Kwa jinsi 2010 inayokaribia kwa kasi,na namna baadhi ya wanasiasa walivyoamua kuwekeza kwenye magazeti,sitashangaa kuona "mashujaa" wengi wakifuata mkumbo wa akina Mjengwa....kula kwa kupitia kalamu zao
 
Koba,Mtanzania,Mkandara,Kitila,...

..yaani mtu anasafiri na Landcruiser VX toka DSM anafika Chalinze anatembea vichochoroni kwa mita 100 kuelekea nyumbani kwake, tayari tunadai yuko karibu na wananchi, na anafaa kuongoza taifa la watu milioni 37? that is what makala ya Mjengwa amounts to.

..ifike mahali tuwapime viongozi kuangalia juhudi zao za katika kushirikiana na wananchi kutatua matatizo yao, na kuinua viwango vya maisha yao.

..uimara wa chama cha CCM na mtandao wake mpana usitukwaze kuamini kwamba mgombea yeyote wa Uraisi watakayemsimamisha atatufaa. sera za vyama ni mahali pazuri pa kuanzia kuwapima wagombea na vyama vyao. lakini kipimo cha uhakika zaidi ni VISION YA UONGOZI ya mgombea husika. sijui kama ukimuuliza Mjengwa vision ya uongozi ya Kikwete ipi ataweza kukupa jibu lolote la maana.

..wengi tunakubaliana kwamba nchi na uongozi umemshinda Raisi Kikwete. sasa kuna faida gani kumrudisha tena mwaka 2010? zaidi, sisi wa-Tanzania tuna kasoro gani kiasi cha kushindwa kubadili uongozi ambao hatujaridhika nao?
 
Labda anataka apewe shavu

Nakubaliana na wewe kabsaaa maana kule kwenye blog ameshaanza kusema siku nyingi tu kuwa anamaliza mkataba na mwajiri wake, Leo ameweka kuwa amebakisha siku kumi kumaliza mkataba wake so atakuwa free kuajiliwa na mtu yeyote lakini alisisitiza ameshazoea kuishi mikoani so angependelea mwajiri atoke pande hizo hizo
 
What point are we missing?Kwani personal opinion haiwezi kuwa wrong?Na personal opinion ikiwa wrong haiwezi kuwa criticized?I think you are the one missing a point kwa kuzungumzia settling old scores as if there was any!

Baada ya kufungiwa Mwanahalisi,Raia Mwema limebaki kuwa weekly pekee la "kuaminika".Misimamo ya akina Johnson Mbwambo,Ayoub Rioba,Ulimwengu,nk inafahamika vizuri.Mjengwa amekuwa anayumba kimsimamo,na makala zake zinaweza kuonekana out of place.Nakumbuka makala yake ya kumkosoa Ansert Ngurumo kuhusu wananchi walioupopoa mawe msafara wa JK huko Mbeya.Kwa hakika haikuwa na mantiki yoyote zaidi ya kupinga hoja za maana za Ngurumo.

Kwa jinsi 2010 inayokaribia kwa kasi,na namna baadhi ya wanasiasa walivyoamua kuwekeza kwenye magazeti,sitashangaa kuona "mashujaa" wengi wakifuata mkumbo wa akina Mjengwa....kula kwa kupitia kalamu zao


Amakweli you can force a donkey to the river but you cant really force it to drink the water. Siwezi kukusaidia kuelewa nilichoandika... Soma post uelewe kabla ya kukurupuka kujibu. Nimeongelea watu watoe counter hoja badala ya kumfanyia Mjengwa character assasination kwa opinion yake!
 
Jokakuu,

Binafsi simpi sifa Kikwete wala kutetea hoja ya Mjengwa haina maana kuwa naungana na sifa alizompa JK.. isipokuwa swala la Kikwete limekuwa swala la Mjengwa.. Sifa alizopewa Kikwete na Mjengwa hata kama ni pupu, majibu yake (hoja) hayakutakiwa kurudi kama Mjengwa..issue sasa hivi imekuwa Mjengwa na CV yake inatazamwa kama vile yeye ndiye mgombea 2010.

Huyu ni mwandishi tu katoa maoni hata kama yanatokana na mapenzi au kapigwa shavu bado hoja inasimama kuwa Kikwete anarudisha hadhi na heshima aliyopoteza.

Nimesema pia kuwa mimi binafsi sioni sababu kabisa Ya Kikwete kushindwa 2010 kwani sisi kina Ndivyo Tulivyo, hizo sifa za kusafiri na Landcruiser VX ukaliacha barabarani ukapuyanga, ndizo sifa za kiongozi. Utasikia Kikwete bwana, kaliacha gari kisha katembea kwa mguu!...pengine tukifananisha na mkoloni ambaye angebebwa au Mkapa ambaye hakuwahi hata kufika kwao!

Mkuu, sisi hatuna kipimo cha Uongozi bora hata kidogo na itachukua karne nzima watu kuweza kuelimika kwa hilo..kumbuka tu Kikwete alishinda kwa Ujana wake, sura yake na juu ya yote hayo - Muungwana.

Mimi na wewe hatuwezi kuchukua asilimia 50+ ya wadanganyika ambao kutwa nzima wanafurahi kuona Mafisadi wakiswekwa ndani.. Hii sifa pekee haina kipimo kwa Taifa letu maanake haiwahi kutokea na kati yetu sote tumemkubali ktk hilo pamoja na kwamba tuna wasiwasi.

Kifupi ni kwamba Dr. Slaa na Zitto wamemboresha Kikwete ktk Popular vote..Yawezekana madai yao yalikuja wakati mbaya wakidhani kuwa Kikwete hawezi kuchukua hatua ama kwa mapenzi ya nchi yao walishindwa kuachia vitu hivi vikiendelea kuharibu Uchumi wetu.. Pamoja na yote hayo Kikwete amekuwa namuda wa kujiandaa na taratibu anarudisha hadhi ya jina lake..

Na kikubwa zaidi amefuata maagizo ya wataalam kuhusiana na rule of law badala ya rule by law..kiasi kwamba watu hawa wanafikishwa mahakamani... ndio Uungwana wenyewe!

Sasa kama ungeniuliza mimi ningewaweka ndani na mali zao zote kutaifishwa kabla hata ya kufikishwa mahakamani..hiyo ndiyo njia pinzani na hiyo anayotumia Kikwete na ningeonekana mnyama na kiongozi mbaya pengine kufananishwa na Mugabe.

Ni wakati wa Kikwete tumeweza kuona jinsi wahuni hawa walivyotuweka ktk hasara na wakati mgumu jambo ambalo linanipa picha kwamba kuna kila uwezekano Kikwete akachukua tena.

Kuhusu chama na sera zake mkuu hilo bado kabisa wakati wake..asilimia 80 ya Wadanganyika hawajui tofauti kati ya mirengo na sera bila jina la mtu..sera bila viongozi makini tumeona matokeo yake..
 
What point are we missing?Kwani personal opinion haiwezi kuwa wrong?Na personal opinion ikiwa wrong haiwezi kuwa criticized?I think you are the one missing a point kwa kuzungumzia settling old scores as if there was any!

Baada ya kufungiwa Mwanahalisi,Raia Mwema limebaki kuwa weekly pekee la "kuaminika".Misimamo ya akina Johnson Mbwambo,Ayoub Rioba,Ulimwengu,nk inafahamika vizuri.Mjengwa amekuwa anayumba kimsimamo,na makala zake zinaweza kuonekana out of place.Nakumbuka makala yake ya kumkosoa Ansert Ngurumo kuhusu wananchi walioupopoa mawe msafara wa JK huko Mbeya.Kwa hakika haikuwa na mantiki yoyote zaidi ya kupinga hoja za maana za Ngurumo.

Kwa jinsi 2010 inayokaribia kwa kasi,na namna baadhi ya wanasiasa walivyoamua kuwekeza kwenye magazeti,sitashangaa kuona "mashujaa" wengi wakifuata mkumbo wa akina Mjengwa....kula kwa kupitia kalamu zao
I think some members wanadhani wanajua sana.laiti wangekuwa na madaraka wangekuwa madikteta kila mmoja anazo opinion zake toa zakwako tukuunge au kukupinga.huu ubishi wa ki-mujahidina haufai.toa hoja kaka
 
mjengwa_maggid.jpg

mjengwa akiwa shambani.....mjengwa na Salva wana tofauti?
 
Huyu dogo si kwamba kaanza , bali anaendeleza mambo haya alianza way back kabla ya JK hajaukwaa .Mjengwa ni opportunist kama wengine ambao wako kwenye NGO ambazo hawawezi kwenda bila ya longo longo zao.Yeye ana asili ya kujipendekeza hata anaweza kuona mema lakini lazima akamilishe tabia yake.Ni kigeugeu sana lakini kwa JK naona ka stick kiasi fulani .Mjengwa ni wa kupuuzwa maana yeye kila siku analeta picha wananchi wakiwa choka mbaya ghafla JK amekuwa karibu na watu tena ?

Kuna nafasi ya mwandishi wa habari za Raisi kusaidiana na January Makamba....
 
..naona Mjengwa ameanza kampeni za Uraisi za Kikwete 2010.

..tatizo ni kwamba hawezi hata kutaja achievement moja ya Kikwete tangu hajaingia madarakani, na mpaka sasa hivi 3 years as the President.

..Mjengwa ameishia kumsifa Kikwete kwa kuwa "karibu" na wananchi kwasababu hutembea kwa miguu kwenye viuchochoro vya Bagamoyo.

..Kikwete yuko karibu na wananchi kwa namna gani wakati aliitelekeza shule yake ya msingi aliposomea? shule hiyo ilionyeshwa ktk gazeti la Uhuru wakati wa kampeni za 2005 ikiwa na hali mbaya imechoka mithili ya zizi la ng'ombe.

..halafu kidogo kidogo Mjengwa anachombeza kuhusu hizi kesi mbuzi zilizofunguliwa majuzi na serikali. inavyoelekea zimempa imani kubwa sana na utawala wa Kikwete.

..Mjengwa anasahau kwamba Kikwete alimteua Chenge kuwa waziri wa afrika mashariki, baadaye akafanya mabadiliko na kumpeleka miundo mbinu. Kikwete huyo huyo alimteua Basili Mramba mara mbili ktk baraza lake la mawaziri. Baada ya Dr.Msabaha kuvuruga Nishati, Kikwete akajaribu kumficha wizara ya afrika mashariki. zaidi, kulifanyika mabadiliko mawili ya makatibu wakuu na yote hayakumgusa Gray Mgonja.

..sasa hii imani ya Majid Mjengwa kwa uongozi wa Raisi Kikwete inatoka wapi?

..Watanzania kwanini tunakumbukumbu fupi namna hii?
Mjengwa Kikwete is abig time manipulator huu sio wakati wa kutumia sura kupata kura, wakati kikwete alipochaguliwa kuwa rais alitembelea hospitali ya Muhimbili kuonyesha he is down to earth watu wakasema yes huyu ndio kweli raisi hawakujua ni mswahili na mjanja anajua watanzania majority hawajui ku analyse issues critically, akikumbatia wagonjwa hata kama wataendelea kulala wawili au watatu kitanda kimoja wataona tu raisi huyu ndiyo mwenyewe.

Kikwete ameleta mabadiliko gani toka atembelee muhimbili wagonjwa bado wana sota huduma za afya bado ni zorota. YOTE ANAYOFANYA NIKU MDANGANYA MWANANCHI WA CHINI. Amkeni usingizini kikwete bishoo huyu fuateni mfano wa marekani We need change. Akiacha safari yake moja tu pesa hiyo itatosha kuleta mabadiliko muhimbili.

Kiongozi anaefikiria wananchi wake hawezi kubadilisha magari kama nguo, anatakiwa aseme pesa hii nisipoitumia ialeta maendeleo gani kwa watu wa tanzania hasa katika elimu na afya lakini yeye kila siku kiguu na njia anajifanya anafichua mafisadi kudanganya toto, uongozi cosmetic huo anokana mzuri usoni ndani kumejaa ufisadi wakichichini.

Kikwete twambie wannchi wako umefanya nini?
 
Hii ni kweli tukae tuangalie kwa makinI WHAT ARE HIS ACHIEVEMENTS Tulimteuwa kwa sababu gani hali za wnanchi hazijabadilika hata kidogo, Watanzania wajiulize kila mmoja Je kuna lolote limebadilika kwa mtanzania wa kawaida? Au ni criteria gani itatumika kumpigia kura huyu bwana mkubwa !!!!!!!! kutembelea watu na kuwacha masikini siyo solution Wake up Tanzanians this is a critical moment. We want actions not empty hand visits
 
1.Jamaa amedeclare katika opening statement kuwa ni "tathmini yake binafsi",...

2.hajajumuisha watanzania wote kwenye huu mtazamo wake. Sasa huku kufoka povu kote kunatokea wapi?....

3. Ofcourse he is entitled to his opinion as an individual,...angekua ametujumuisha watz wote kwenye huo mtazamo wake,... tungekua na haki ya kumshambulia.

4.I dont necessarily share his opinion but still, nahisi we are missing the point kwa kumtolea personnal attacks

5.cha kufanya ni kujenga counter hoja za hiyo mitazamo yao instead of personal character assasinations.

- Mkuu hapa tupo ukurasa mmoja,ni muhimu sana kwa demokrasia kuheshimu mawazo ya wananchi wote na hata yasiyokuwa kama yetu, cha muhimu sana ni kujenga hoja against hoja za wale tusiokubaliana nao.

However:-

- Huyu bwana Mjengwa simfahamu, lakini kwa haya mawazo yake anaonekana kuwa a naive person, infact hana hoja nzito kabisaa na kama Muungwana anategemea watu kama hawa kumfagilia basi ndio maana Lowassa na kundi lake huko in private wanadai Lowassa atarudi tu 2010, maana wao ndio waliompa urais Muungwana, huenda wana point maana hoja ya kumrudisha urais Muungwana haiwezi kuwa ni kuongea na wananchi kijijini na kupita vichochoroni tu basi, that is pathetic thinking!

- Unajua hoja zingine zinaudhi na ni too shallow hata zina-justifiy kumshambulia mtoa hoja as of this case hapa!
 
Field Marshall,

Mkuu binafsi sikubaliani na mawazo ya kumshambulia Mjengwa.. Hata kama mawazo yake ni finyu ama potofu..

Swali moja tu Kikwete aliweza vipi kushinda 2005 wakati waliomchagua kwa kura zaidi ya asilimia 80 sio Lowassa na kundi lake. Na hakuna mahala popote kunaonyesha mchango wa Lowassa ktk ushindi wa Kikwete (uchaguzi mkuu)isipokuwa Ushindi wa Lowassa unatokana na Kikwete..Je, aliweza kushinda kwa sifa zipi! si hizi hizi za kihuni tu na kumbuka sisi wengine tuliosema Salim tulionekana hatuna akili...

Wewe na mimi tunaweza kuziona hoja za huyu jamaa too shallow lakini ndio maji Wadanganyika wengi wanaweza kuyaoga!..

Na ukitaka kuamini, jaribu kufanya survey waulize Wadanganyika 1000 kuhusu Kiongozi bora (rais) sikiliza majibu yao - Utachoka...Tazama magazeti yetu, yasome na uangalie upupu unaoandikwa lakini ndio yananunuliwa utafikiria watu hawana akili..

Zamani tulikuwa tukiwacheka Zanzibar kwa Taarifa za habari wakizungumzia mtu kaibiwa kandambili msikitini, siku hizi Bara habari kama hiyo ndio breaking news tena zinachukua front page..
 
Kusahau na kukumbuka kote sawa tu kwa Tanzania. Mjengwa anatumia uelewa huu kuandika...Watanzania hawajui kukumbuka, siku wakijua haitakuwa Tanzania tena
 
WENYE kupanga mikakati ya kivita wanajua, kuwa matokeo ya ushindi wa kivita hufahamika kabla risasi ya kwanza kupigwa. Inahusu matayarisho, malengo, mbinu na mikakati.


Ninapoandika haya, zimebaki siku 30 kabla ya Watanzania wenye sifa za kupiga kura hawajapanga foleni ya kwenda kupiga kura, nchi nzima. Kuchagua madiwani, wabunge na Rais.

Zilipobaki siku 45 kabla ya Oktoba 31, 2010 nikaandika; " Kama Uchaguzi Mkuu Ungefanyika leo…" . Ilikuwa ni tathmini yangu kutokana na uzoefu wangu wa chaguzi zetu na hali halisi ninayoiona. Nikathubutu kuandika, kuwa mgombea wa kiti cha Urais kutoka Chama Cha Mapinduzi, Bw. Mrisho Jakaya Kikwete, angeibuka kuwa mshindi, na kwamba CCM ingepata wabunge wengi na madiwani. Kwamba Dr Wilbrod Slaa, mgombea urais kutoka CHADEMA angechukua nafasi ya pili. Kwamba Chadema ingekuwa ya pili pia kwa idadi ya wabunge na madiwani kutoka bara. Nikabainisha, kuwa Profesa Ibrahim Lipumba, mgombea Urais kutoka CUF angechukua nafasi ya tatu.

Leo, zikiwa zimebaki wiki nne kabla ya siku ya uchaguzi naiona hali iliyobadilika katika uwanja huu wa mapambano ya kisiasa. Naiona hali ifuatayo kama uchaguzi ungefanyika kesho.

Mgombea wa CCM, Jakaya Kikwete angeibuka kuwa mshindi. Profesa Ibrahim Lipumba angeshika nafasi ya pili na huku Dr Wilbroad Slaa angetoka akiwa mshindi wa tatu. Vivyo hivyo, CCM ingetoa wabunge na madiwani wengi ikifuatiwa na CUF na CHADEMA. Kwamba CUF ndio ingekuwa chama kikubwa cha upinzani bungeni na hivyo basi, kutoa kiongozi wa upinzani bungeni kama ilivyokuwa katika bunge lililopita.

Nafahamu kuwa hii ni tathmini itakayowakera baadhi humu mtandaoni, lakini najisikia huru na kuona umuhimu wa kuandika tathmini yangu hii kwa madhumuni ya kuchochea mjadala na kujifunza pia. Ni ukweli, kuwa ukweli mwingine unahuzunisha, lakini ni lazima usemwe. Maana, ukweli ni uhuru pia.

Ni nini basi tafsiri ya nilichokiandika? Kama tungekuwa na uchaguzi mkuu kesho, Jakaya Mrisho Kikwete angeunda Serikali huku yeye na chama chake wakikabiliwa na changamoto kama nilizozielezea katika makala yangu yaliyopita. Kwamba changamoto kubwa itatokana na upinzani utakaokuwa umeongezeka nguvu ndani na nje ya bunge kutokana na ujio wa Dr Slaa kama mgombea Urais katika uchaguzi wa mwaka huu. Na ziada hapo, ni kuibuka kwa CUF bara kama chama chenye wabunge kati ya 10 na 15 na idadi ya kutia moyo ya madiwani.

Huko nyuma nilibainisha, kuwa viashria vya jamii inayotaka mabadiliko vimeshaonekana. CCM itakuwa na mawili ya kuchagua; kuchukua jukumu la kuyaongoza mabadiliko hayo au kusubiri kuzamishwa na mkondo wa maji ya mabadiliko hayo.

Historia ni mwalimu mzuri. Matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa 2005 na uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa Oktoba mwaka jana yanaiweka CCM na mgombea wake Urais mahali pazuri zaidi kiushindi kulinganisha na CUF na Chadema. Angalia taarifa hii; Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika Oktoba mwaka jana ulimalizika kwa kukipa ushindi mnono Chama Cha Mapinduzi. Chama hicho kilipata ushindi wa asilimia 91.71 za kura, kikifuatiwa kwa mbali na CUF iliyopata asilimia 3.94 na Chadema asilimia 2.76.

Katika Mkoa wa Dar es Salaam pekee, Chama hicho tawala kiliibuka na ushindi mnono kwa kupata viti 402 kati ya 448, sawa na asilimia 91, huku wapinzani wakiambulia viti 40, sawa na asilimia tisa tu. Katika mkoa wa Iringa ninakoishi, CHADEMA, ilifanikiwa kushinda mtaa mmoja wa Kihesa Kilolo "B",. Ni kwenye Kata ya Mtwivila Manispaa ya Iringa.

Katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005. CCM na mgombea wake Urais waliibuka washindi. Jakaya Kikwete alipata zaidi ya kura milioni 9.2 . Alifuatiwa na Profesa Lipumba aliyepata kura milioni 1.3 na huku mgombea wa CHADEMA , Freeman Mbowe akiambulia kura laki 7.
Pamoja na Profesa Lipumba na chama chake cha CUF kuwa cha pili, hakikupata mbunge wa kuchaguliwa huku CHADEMA ikipata nafasi hiyo ya kuwa na wabunge wa kuchaguliwa zaidi ya watano katika Bunge la Jamhuri ya Muungano.

Kwa hali ilivyo kwa sasa, CCM bado wanajivunia:

Kuwa ni chama kikongwe, kikubwa na kilichotawala kwa muda mrefu. Na nilibainisha huko nyuma, kuwa kuna hata wanaokipigia kura chama hicho ' Kwa mazoea tu'. Na katika nchi zetu hizi; kukiondoa chama kilicho madarakani, Chama kilichopigania uhuru au kinachotokana na chama kilichopigania uhuru ni kazi ngumu sana. Kwa anayetaka kufanikiwa katika hilo, anahitaji kwenda ilipo mizizi ya chama hicho. Ni vijijini. Na huko vijijini kwa leo hii chama wanachokijua ni CCM. Naam. Ndio ' Zimwi' wanalolijua. Mwanakijiji atatembea kwa miguu kilomita kumi kwenda kuhudhuria mkutano wa CCM. Atakwambia amepewa taarifa ya mkutano na Balozi wake wa Nyumba Kumi. Hivyo basi, CCM wanajivunia mtandao wao wa kichama kuanzia ngazi ya Balozi wa Nyumba Kumi, shina, tawi na kuendelea. Na hata mtandao wa Kiserikali.

Nyongeza ya Udhaifu wa CCM:
Kwamba CCM inajivunia ‘K' zake tatu; Chama Kikongwe, Kikubwa na Kinachotawala, basi, kuna baadhi ya watendaji ndani ya Chama hicho walioshindwa kusoma alama za nyakati. Wanafanya kazi zao kwa mazoea. Jambo hilo limeigharimu CCM muda na rasilimali katika jitihada za kuziba mashimo. Matokeo ya Uchaguzi wa Oktoba 31 hayataiacha CCM na mfumo mzima wa uendeshaji nchi katika hali iliyozoeleka. Subirini, mtaona.

Mama Salma Kikwete na Ridhiwani Kikwete:

Wawili hawa wamekuwa kiini cha mijadala itakayoendelea huenda hata baada ya uchaguzi kwisha. Tangu Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005 uliomwingiza madarakani Jakaya Kikwete, Tanzania imeshuhudia aina mpya ya harakati na kampeni za kisiasa zenye kuhusisha mke wa mgombea na hata wana familia ya karibu kama hili la mke na mwana wa Rais, Ridhiwani Kikwete.

Inaonekana sasa, kuwa zama za ' First Lady' kuwa ' Mama wa nyumbani' Ikulu zimepita. Ni dhahiri, kuwa kwa mgombea wa CCM, Jakaya Kikwete, amenufaika sana na ushiriki wa karibu wa mkewe na mwanawe Ridhiwani. Na si kwa Jakaya Kikwete tu, CCM kama chama, wagombea ubunge wake wananufaika kwa kiasi kikubwa na uwepo wa Mama Salma Kikwete na Ridhiwani kwenye kampeni.

Wote wawili, Salma Kikwete na Ridhiwani Kikwete wana mvuto wa kisiasa unaoongezewa nguvu na wao kuwa wanafamilia ya Rais aliye madarakani na ambaye bado, kiukweli, ana mvuto kwa Watanzania walio wengi.

Katika mazingira ya sasa, Salma Kikwete na Ridhiwani Kikwete wanafanya kile ambacho Jakaya Kikwete hawezi kukifanya kwa urahisi kwenye kampeni kutokana na kubanwa na itifaki. Mama Salma Kikwete anaweza kufanya mikutano ya ndani Lindi, Mtwara na kwingineko akiongea na kundi kubwa la wapiga kura, wanawake, kwa lugha yao. Amefanya hivyo 2005 na sasa ana uzoefu zaidi. Anaongeza kura za JK.

Vivyo hivyo kwa Ridhiwani Kikwete, naye ana ametokea kwenye Chipukizi wa CCM na kuingia kwenye Umoja wa Vijana wa Chama hicho na kushika nafasi za uongozi. Ridhiwani ana mtandao mpana wa kichama ndani ya jumuiya hiyo na hata nje. Ni karata muhimu kisiasa. Ingekuwa ajabu kama asingezunguka kumtafutia kura zaidi mgombea wa chama chao ambaye pia ni baba yake.

CHADEMA:

Ujio wa Dr Slaa:

Niliandika, kuwa ujio wa Slaa, sio tu umewashangaza CCM na mgombea wake urais, bali pia unaonekana kuwashangaza CHADEMA wenyewe wanaoonekana kutokujiandaa na namna Dr Slaa alivyopokewa na wananchi. Dr Slaa ameongeza msisimko kwenye siasa za nchi yetu. Watu wengi wana shauku ya kumsikiliza, kama ilivyokuwa kwenye uchaguzi wa 1995 uliomwibua Augustino Mrema. Akijipanga vema, hata baada ya uchaguzi huu. Akafanya kazi ya CHADEMA nje ya Bunge na kutembea nchi nzima, basi, Dr Slaa anaweza kuwa tishio kwa ye yote ndani ya CCM atakayekuja kupambana nae.

Udhaifu wa CHADEMA
Unajidhihirisha kwenye eneo la oganaizesheni na kifedha. Hilo nililibainisha katika makala yangu yaliyopita. Bado CHADEMA haina uwakilishi mpana katika ngazi za mashina na matawi. Niliandika, kuwa Dr Slaa anaweza kutua na helikopta Pawaga Iringa, lakini mara ile akiruka, huku nyuma hakuna watendaji wa CHADEMA wa kufanya kazi ya CHADEMA. Kuna taarifa pia za wagombea wake ubunge na udiwani kukosa nguvu za kifedha kuendesha kampeni .

Zitto Kabwe bado ni kitendawili:

Niliandika, kuwa Zitto Kabwe n i kada nyota ndani ya CHADEMA, lakini ‘sarakasi' zake za kisiasa huenda zinachangia kukidhohofisha chama chake kuliko kukipa nguvu. Alipata kulipotiwa na magazeti kutamka hadharani kuwa anajiandaa kugombea urais 2015. Zitto Kabwe alituachia maswali; Kulikoni ndani ya CHADEMA? Je, Dr Slaa ni mgombea wa ‘msimu' tu? Au ndio sababu Zitto Kabwe hakuhudhuria Mkutano wa ufunguzi wa kampeni za CHADEMA? Niliandika, kuwa kuna watakaouliza. Na maswali yanaongezeka.

Inachojivunia CHADEMA:

Bado ni chama kinachoonyesha kuwa na mvuto kama kitajipanga vema. Kuna vijana wengi na hususan wasomi wenye kuvutiwa na CHADEMA. Hizi ni dalili njema kwa CHADEMA kwa siku zijazo, endapo zitabaini mtaji huo , kuuwekeza na kuutumia vema mbele ya safari.

CUF: CHAMA CHA WANANCHI
Leo naweza kukiri, kuwa nilikosea, nilipoandika, kuwa CUF ( Bara) safari hii kinaonekana zaidi kuwa ' jokeli' katika karata za kisiasa. Kwa hali ilivyo sasa, CUF bado ni chama chenye nguvu na kilicho na mizizi kwenye baadhi ya maeneo ya nchi. Na kwa hakika, Profesa Ibrahim Lipumba bado anaonekana kuwa na nguvu katika kanda ya pwani na mikoa ya kusini.

Mathalan, kama Uchaguzi Mkuu utafanyika kesho, CUF ina hakika ya kunyakua kati ya viti 8 hadi 10 kutoka mikoa ya Kusini pekee; Lindi, Mtwara na Ruvuma. CUF ina nafasi ya kushinda viti vingi vya madiwani kutoka mikoa hiyo na hata kuweza kuongoza halmashauri moja au mbili. Tunduru ni moja ya majimbo ambayo CUF ina nafasi kubwa ya kutoa mbunge na madiwani.

Ndio, Profesa Ibrahim Lipumba bado ni tishio. Ana uzoefu na anautumia. Na siku ile CHADEMA na CUF watakapokubaliana kuunganisha nguvu na kutoa mgombea mmoja wa Urais, basi, CCM itakuwa shakani. Lakini si kwa sasa, zikiwa zimebaki siku 30 kabla ya Oktoba 31. Ninapoandika fikra hizi huru.

Maggid
Iringa, Oktoba 1, 2010.
mjengwa
 
Maggid

Nadhani umerudia yale yale ya wiki mbili zilizopita na hakuna jipya japo una uhuru wa ku-recyle mawazo yako kila wakati.

Kigezo chako cha uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi wa 2005 ni weak mno kwa sasa. Kuna mambo mengi yamebadilika ikiwamo chemistry ya siasa za uchaguzi. Fikiria haya:
-JK kudai miaka 5 ya kwanza alikuwa anajifunza kazi, sasa anaomba ili afanye kazi ni tamko la hatari. Watu walichagua rais kufanya kazi si kufanya mazoezi.
-CCM ilikuwa moja na imara wakati wa uchaguzi wa 2005 kuliko ilivyo sasa. Kuna wana CCM wengi watakaopigia upinzani kuliko idadi ya wapinzani wenyewe. Ushindi wa Kikwete 2005 ulichangiwa na kura za wapinzani kuliko unavyoweza kutegemea sasa.
-JK aliridhi uchumi mzuri kutoka Ben kuliko hali ya uchumi tuliyo nayo sasa.
-Kampeini za uchaguzi wa 2005 zilifanywa na mtandao plus chama - hizi za sasa zinafanywa na familia -JK, Salma, Ridhiwani na Miraji. Jioni hii JK amemuita Makamba kulalamika kuwa kuna maeneo hayana mabango na anahitaji maelezo. Hii si kazi ya mgombea wa chama kikubwa!

Chemistry ya namna hii, haina nafasi katika matundu ya uchambuzi wako uliolalia "mazoea" na theory iitwayo "Makambaism".
 
Nafahamu kuwa hii ni tathmini itakayowakera baadhi humu mtandaoni, lakini najisikia huru na kuona umuhimu wa kuandika tathmini yangu hii kwa madhumuni ya kuchochea mjadala na kujifunza pia. Ni ukweli, kuwa ukweli mwingine unahuzunisha, lakini ni lazima usemwe. Maana, ukweli ni uhuru pia.

Maggid mark my words, matokeo ya ucahaguzi huu yatakushangaza sana kama tathmini yako ndiyo hiyo!!!!!!!! Kwa uhuru huo huo unaouzungumzia, this is my prediction

Wa kwanza Dr. Slaa, wa pili JK na wa tatu Lipumba.......... haha ahaha ahahah
 
Back
Top Bottom