Mjengwa ang'atuka KWANZA JAMII | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mjengwa ang'atuka KWANZA JAMII

Discussion in 'Celebrities Forum' started by Sumaku, Jul 28, 2009.

 1. S

  Sumaku Member

  #1
  Jul 28, 2009
  Joined: Feb 17, 2009
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mbwa wa Manzese

  Na Maggid Mjengwa,


  NAKIKUMBUKA kisa alichopata kusimulia Mwalimu Nyerere kunako mwanzoni mwa miaka ya 80. Ilikuwa ni kwenye kilele cha sherehe za Wafanyakazi Duniani, Mei Mosi pale uwanja wa Taifa, Dar Es Salaam.

  Baadhi ya mabango ya wafanyakazi yaliyopita mbele ya Mwalimu siku ile yaliwakilisha ujumbe juu ya hali ngumu ya kimaisha iliyokuwa ikiwakabili wafanyakazi ikiwamo mishahara midogo na mengineyo.

  Wakati huo Serikali chini ya uongozi wa Mwalimu Nyerere ilikataa masharti ya Shirika la Fedha Duniani na Benki ya Dunia pia. Hii ni kwa sababu, licha ya athari nyingine mbaya kwa masharti hayo kwa nchi yetu, uhuru wetu wa kujiamulia mambo yetu nao ulikuwa hatarini.

  Ilipofika wakati wa kutoa hotuba Mwalimu Nyerere alisema;
  “ Ndugu zangu watu wa Dari Salama ebu nisikilizeni; kulikuwa na mbwa wawili, mmoja wa Manzese na mwingine wa Oysterbay. Ikatokea siku moja mbwa wa Manzese akatembea hata akafika Oysterbay.

  Kwenye moja ya nyumba za huko akamwona mbwa mwenzake aliye ndani ya geti. Mbwa yule wa Manzese akasogea getini huku akimshangaa mbwa wa Oysterbay aliyenenepeana na manyoya yanayoteremka machoni. Mbwa wa Oysterbay naye alimshangaa mwenzake wa Manzese aliyekondeana. Mbwa wa Oysterbay kwa mshangao akamwuliza mwenzake wa Manzese;

  “ Hivi nawe ni mbwa kama mimi?!
  - Naam, miye ni mbwa kama wewe.
  - Sasa mbona umekondeana hivyo, njoo humu ndani kwa bwana wangu nawe uwe kama mimi.
  Mbwa wa Manzese akajibu; “ Lakini wewe umefungiwa, mwenzio niko huru!”

  Kisa kile alichosimulia Mwalimu kilikuwa ni cha kifalsafa. Naamini katika alichokisema Mwalimu, nitaendelea kuamini hivyo hata katika muda wangu uliobaki humu duniani. Mwalimu alizungumzia dhana ya uhuru. Neno uhuru lina maana kubwa ingawa ni neno fupi sana. Asiye na uhuru ni mtumwa.

  Leo hii naandika kwa furaha kuwajulisha kuwa nimeng’atuka kufanya shughuli za kiutendaji katika gazeti hili la KWANZA JAMII nililoshiriki kuliongoza tangu mwanzo wake hadi kufikia toleo la 16 juma la jana. Hakuna Jumanne ambalo halikufika mitaani tangu toleo la kwanza. Naam. Ni miezi minne ya kazi ngumu. Umefika wakati wa kuwaachia wengine ili nifanye mengine.

  Nawashukuru kwa dhati kabisa wachangiaji wa makala na habari katika gazeti hili. Wengi wao wamejitolea na wanaendelea kujitolea. Wanaandika bila kulipwa chochote. Wanajitolea kwa jamii yao, kwa nchi yao.

  Hawa ni ‘ wapiganaji’, wanawake kwa wanaume, ambao bila kujitolea kwao, hakika gazeti hili ulisomalo lingekuwa marehemu mwezi mmoja tu baada ya kuanzishwa kwake.

  Kwenu nyote mnaolitakia mema gazeti hili na nchi yetu kwa ujumla, tukae tukijua, kuwa mapambano ya kuipigania Tanzania na hata kulifanya gazeti hili liendelee kuwapo mitaani bado ni magumu sana. Hatuna sababu ya kukata tamaa.Tukishindwa kukimbia tutembee, tukishindwa kutembea tutambae.Na hata tukishindwa kutambaa, tupambane mpaka risasi ya mwisho, mpaka pumzi ya mwisho.

  Ni nani basi anayechukua nafasi yangu?
  Kijana Benedict Sichalwe amechukua rasmi jukumu langu kama mwenza. Sichalwe ana msimamo, hana makundi na anaheshimu maadili ya taaluma yake. Alianzia katika gazeti la Dimba mwaka 1993 na kwa sasa ametokea katika jarida la RAI baada ya kumaliza mkataba wake.

  Binafsi nimejifunza mengi katika kuliongoza gazeti la kada hii ya KWANZA JAMII. Kuna walionisaidia bila kunipa masharti yeyote, nawashukuru sana. Nawashukuru pia hata wale walioonyesha utayari wa kunisaidia ingawa kwa masharti. Niliyakataa masharti yao kwa kutamka huku nikiwatazama usoni, bila kuwaonea haya.

  Anayenifahamu anajua kuwa naweza kukubaliana na kufanya kazi na yeyote yule katika kilicho na maslahi kwa nchi yetu bila kujali itikadi, dini , rangi au kabila la muhusika. Nitafanya hivyo hata kama kwa kujitolea tu.

  Ukweli sina chama, na sijawahi kuwa mwanachama wa chama cha siasa. Sina makundi. Nina marafiki karibu katika vyama vyote vikubwa vya kisiasa hapa nchini. Wakati wa mchakato wa uchaguzi wa 2005, kwa kuandika makala mbili za kumwelezea Dr. Salim Ahmed Salim na nyingine kupinga ubaguzi wa kisiasa uliofanyika dhidi yake, basi, kuna walioamini kuwa nilikuwa mmoja katika kambi ya Dr. Salim.

  Ukweli sikumfahamu Dr. Salim kwa kukutana naye hadi Februari 5 mwaka huu nilipomtembelea na kukutana naye kwa mara ya kwanza ofisini kwake. Azma yangu kuu ilikuwa ni kusalimiana na kufahamiana naye, basi.
  Siku zote naamini, kuwa kama thamani ya mwandishi haijulikani, basi, mwandishi huyo ana thamani kubwa, na kinyume chake. Hakuna anayejua thamani yangu kwa maana ya bei ya kuninunua.

  Nilipoanzisha jarida la michezo la GOZI SPOTI sikuzungumzwa sana. Gozi Spoti lilidumu kwa mwaka mmoja. Ajabu nilipoanzisha gazeti hili la KWANZA JAMII , haraka nikasoma mitandaoni watu wakinijadili. Ikasemwa kuwa KWANZA JAMII linamilikiwa na mafisadi, hivyo basi hata mimi nimenunuliwa na hata kuitwa fisadi.

  Kila mtu ana uhuru wa kikatiba wa kutoa maoni yake. Naheshimu uhuru huo na nitaendelea kuupigania. Hata hivyo, waliozungumza hayo juu yangu ni watu wasionifahamu. Nami sikupoteza hata dakika moja kulumbana na watu wasionifahamu na wala wasiojitambulisha kwa majina yao halisi.

  Baadhi ya wanaonifahamu wanajua nilianzisha na kuendesha gazeti nikiwa kidato cha pili shuleni pale Sekondari ya Tambaza. Niliandika kwa kalamu ya wino na kwa mkono katika karatasi za A-4. Niliweza kubandika kwenye ubao wa matangazo kile nilichoandika, kikasomwa na wanafunzi wenzangu hata walimu . Hiyo ni historia yangu pia.

  Nitafanya nini sasa?

  Nitabaki kuwa mwandishi wa makala kupitia safu hii. Kuna mengi ya kuandika, na nina azma ya kuandika kitabu. Maana, katika miaka yangu ya uandishi, nimekutana na watu wa kada mbali mbali. Mathalan, kuna bwana mmoja mwenye dhamana ya uongozi alipata kuniuliza; hivi wewe unaandika ili kumfurahisha nani?

  Mwezi Novemba, 1996 nilikuwa kijijini Ilula, Rais Mkapa akiwa na mwaka mmoja madarakani alikwenda huko kufungua mradi wa umeme uliokamilika. Kwenye hotuba yake, Mkuu wa Mkoa wa wakati huo, Bw. Nicodemus Banduka alimwambia Mheshimiwa Mkapa kuwa mkoa umemwandalia ng’ombe wawili wa maziwa. Watasafirishwa kwa njia ya gari kwenda Ikulu. Ilikuwa ni zawadi ya ng’ombe si kumfurahisha Mkapa, bali kujipendekeza kwa Mkapa. Nani alimwambia Mkuu wa Mkoa kuwa Rais ana shida ya maziwa?!

  Hivyo basi, swali nililoulizwa na Bwana yule lilikuwa; “hivi wewe unaandika ili kujipendekeza kwa nani? “ Kitabu nitachoandika kitaitwa ‘Ng’ombe wa Ikulu’. Ni mkusanyiko na mwendelezo wa fikra zangu. Natumaini nitaishi kukiandika na kukichapa. Ahsanteni.

  0788 111 765


  CHANZO: http://www.kwanzajamii.com
   
 2. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #2
  Jul 28, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,306
  Likes Received: 5,596
  Trophy Points: 280
  duuu mimi nilijua labda mjengwa umejikomboa umeanzisha gazeti lako.....kama haikuwa hivyo.....basi fikiria hilo kama unafikiriaa utaweza kukusanya nguvu....hapo tuu ndio uhuru wako utatimia...mawazo yangu
   
 3. L

  Lukundo Member

  #3
  Jul 28, 2009
  Joined: Feb 19, 2009
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mjengwa alifanya kazi nzuri sana na raia mwema, na blog yake ile. Aliposema anaacha kutoa gozi sport, nilimwandikia kuwa mwanzo wa kutangatanga ni kukosa mipango ya muda mrefu. Na alisema anaanzisha kitu kizuri zaidi, sasa miezi michache tu,anamwaga manyanga . Sio kitu kizuri hata kidogo, hata hivyo ajue kuwa katika jamii ambayo imejaa wabeuzi, ni vigumu kufanya kitu kionekane kuwa ni kwa maslahi ya wananchi, itasemwa tu kuwa kuna kitu unafaidika nacho. Tusubiri tuone.
   
 4. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #4
  Jul 28, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Mbona sijaona alipo sema anang'atuka?
   
 5. MpigaFilimbi

  MpigaFilimbi JF-Expert Member

  #5
  Jul 28, 2009
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,171
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 133
  ...au umesahau miwani yako mkuu??
   
 6. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #6
  Jul 28, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,644
  Likes Received: 1,470
  Trophy Points: 280

  hahaha dogo ulilala nazo kichwani nini?

  by the way hata mimi nimemshangaa kidogo Maggid....kusema kweli nilidhani kuwa hapa kwanza jamii ndo amefika, na kuacha gazeti baada ya miezi minne tu huwezi kusema eti muda wangu wa kung'atuka umefika...ni lazima kuna vitu vinaendelea nyuma ya pazia ambavyo hatuvijui.
  na labda pengine uamuzi wa kujitoa raia mwema haukuw amzuri sana?

  Kilala heri kwenye uandishi wa kitabu!
   
 7. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #7
  Jul 28, 2009
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,741
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mjengwa ukingatuka kwenye kila gazeti tunakuchukulia kaka 'quitter' inabidi ujaribu kupigana ukiwa humohumo ndani,ni maoni yangu tu.
   
 8. Mopao Josee

  Mopao Josee JF-Expert Member

  #8
  Jul 28, 2009
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  `LIFE IS NOT A RIHESO`
  Umejipanga???????????/
   
 9. S

  Silas A.K JF-Expert Member

  #9
  Jul 28, 2009
  Joined: Apr 23, 2008
  Messages: 807
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Nimeipenda hii RIHESO (rehearsal).
   
 10. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #10
  Jul 28, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145

  Yeah nilisahau.
  Kama ndo hivyo jamaa amezidi kutanga tanga au ameona halilipi nini?
  Biashara iwa tunaanza kwa hasara baadae inaanza kujilipa yenyewe.
   
 11. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #11
  Jul 28, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Hata hapa JF alishajitoa kitambo...!
   
 12. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #12
  Jul 28, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  Kwahiyo

  All the best Mjengwa M
   
 13. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #13
  Jul 28, 2009
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Tatizo lako Mjengwa Ulianza kwa Kushindwa, hukusoma alama za Nyakati na Ukiwa Bosi wa Kwanza Jamii uliruhusu gazeti lako katika toleo la mwanzo kabisa kuandika UDAKU

  Unaikumbuka hii Mjengwa kutoka Kwanza Jamii?

  Kamati ya Dk. Wilbroad Slaa yalamba posho mara mbili
  12 May 2009 749 views 5 Comments
  Na Mwandishi Wetu

  MAELEZO yalivowahi kutolewa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU), Dk. Edward Hosea, kwamba wapo baadhi ya wabunge wanaopokea posho mara mbili, yamethibitishwa katika ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh.
  Ripoti hiyo ya CAG inathibitisha hali hiyo kutokana na ukaguzi wa hesabu za Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga, mkoani Rukwa, ikidhihirika kuwa malipo yaliyofanywa kupitia vocha ya malipo yenye namba 1/8/066145, yaliyosainiwa na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo yalitumika kulipa wabunge posho.
  Katika hali ya kawaida, wabunge hulipwa posho na ofisi ya Bunge hususan wanapokuwa katika shughuli za kawaida zinazohusiana na kamati za Bunge.
  “Katika ukaguzi tulioufanya tuliweza kubaini matumizi yasiyostahili yenye thamani ya Sh 8,472,200 ambayo yasingeweza stahili kulipwa kwa kutumia fedha za miradi ya TASAF,” anasema CAG kupitia ripoti yake ya ukaguzi kwa mwaka ulioshia Juni 30, mwaka 2008, ripoti ambayo hata hivyo imekwishawasilishwa bungeni.
  Maelezo yaliyotolewa kwa CAG kuhusu malipo hayo yanasema; “Posho kwa ajili ya vikao vya kamati ya Bunge ya hesabu za serikali za mitaa Agosti 7 hadi 16 mwaka 2007 yalikuwa Sh 1,050,000.
  Kutokana na kubainika kwa hali hiyo huenda hadhi ya wajumbe wa kamati hiyo inayoongozwa na Dk. Wilbroad Slaa, Mbunge wa Karatu, ikaingia doa mbele ya umma wa Watanzania.
  Aprili 2, mwaka huu, Dk. Hosea aliwaeleza wabunge waliojaribu kuhoji uhalali wake wa kuiongoza TAKUKURU wakati akiwa anakabiliwa na tuhuma za kusafisha kashfa ya zabuni ya mitambo ya kuzalisha umeme wa dharura ya Richmond, kuwa kama watafanya hivyo basi nao pia wawe tayari kusikia kashfa zao mbele ya umma. Mara baada ya kutoa kitisho hicho kwa wabunge wakati wa semina ya miundombinu ya uadilifu iliyoandaliwa na Takukuru na Chama cha Wabunge wa Afrika (APNAC) na kufanyika kwenye Hoteli ya Whitesands, jijini Dar es salaam, Dk. Hosea alijikuta katika wakati mgumu.
  “Inakuwaje wakati wa mjadala wa Richmond, wewe mkururugenzi wa Takukuru ulikanusha kuwapo rushwa na uchunguzi wa kamati ya Bunge ulibaini kuwepo rushwa ndani ya kampuni hiyo?
  Je ni nani mwenye dhamana ya kukuadhibu wewe na taasisi yako kuhusu rushwa’’ alihoji Mbunge wa Busega, Dk.Raphael Chegeni katika semina hiyo.
  Swali hilo halikutegemewa na Dk Hosea na lilionekana kumuudhi na kulazimika kuchukua kipaza sauti na kusitisha maswali na kuanza kujibu kwa ghadhabu.
  “Hapa siyo jukwaani hivyo tusilete siasa. Nipo hapa kwa ajili ya kufundisha na kama ni suala la Richmond waziri mkuu alishaliongelea na ndiyo mwenye dhamana ya kujibu hilo. Mimi sina jibu kwa hilo na kama mtu hapendi kuvuliwa nguo kwanini umvue mwenzako,” alisema Dk Hosea.
  “Mjadala huu aachiwe Waziri Mkuu Mizengo Pinda na aliyeuliza swali hilo hanitendei haki kwani hakuna hoja nyingine ya maendeleo kwa jamii ambalo inaweza kujadiliwa… mbona mnang’ang’ania kujibu hilo pekee.
  “Najua kuna watu wanatumiwa ili niongee halafu nibabaike katika kujibu na nishindwe kufanya kazi yangu. Mbona mnang’ang’ania jambo hilo tu wakati kuna hoja nyingine za maendeleo kwa jamii. Kuhusu suala la Richmond sijibu ng’o.”
   
 14. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #14
  Jul 28, 2009
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  huyu jamaa anakipaji sema naona amekosa msimamo.
   
 15. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #15
  Jul 28, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  Siku hizi pia namwona hata afya pia inaonyesha amepata matatizo fulani hivi siri yake
   
 16. Ochu

  Ochu JF-Expert Member

  #16
  Jul 28, 2009
  Joined: May 13, 2008
  Messages: 972
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  mJEngwa ulishindwa kuwa makini kwa toleo la kwanza tu!!! matokea yake ndiyo haya. you are a QUITER!!!!!
   
 17. Mlalahoi

  Mlalahoi JF-Expert Member

  #17
  Jul 28, 2009
  Joined: Aug 31, 2006
  Messages: 2,065
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Huyu Mjengwa vipi?Mbona anatapatapa?

  Huyo Sichwale ni kijana wa Rostam Aziz.Trick iliyotumika hapo ni nyepesi tu:Gazeti kaanzisha Mjengwa,kisha kalikabidhi kwa Sichwale (angekuwa na msimamo kama anavyotuaminisha Mjengwa basi huyo Sichwale asingedumu hapo RAI hadi "mkataba umalizike"),na Sichwale ni kijana wa Rostam.
   
 18. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #18
  Jul 28, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Wacha Nongwa wewe! Toka lini umekuwa daktari?
   
 19. Mambo Jambo

  Mambo Jambo JF-Expert Member

  #19
  Jul 29, 2009
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 1,100
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  kwikwikwikwi!!!! kama dada Sara wa Alaska.....
   
 20. Mambo Jambo

  Mambo Jambo JF-Expert Member

  #20
  Jul 29, 2009
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 1,100
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Hivi kwa nini vyombo vingi vya habari hivi sasa lazima viishie na neno JAMII au vianze na neno JAMII?..au ni kwa sababu ya JF
   
Loading...