Mjengwa - aanika njia mbalimbali sumu kumwingia mtu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mjengwa - aanika njia mbalimbali sumu kumwingia mtu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Njele, Feb 19, 2012.

 1. N

  Njele JF-Expert Member

  #1
  Feb 19, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 275
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Watanzania, tuna blog nyingi na zinazidi kuchupuka, lakini ni chache zenye kujenga taswira ya kujali zaidi maisha ya wananchi wa Tanzania na kutoa elimu bila woga wala upendeleo. Hii ni sifa kubwa ya Mjengwa, na hapa katika pitapita zangu nimekutana na tahadhari hii kuhusu mbinu za kuwekewa sumu mtu. Vema tukazijua kwa tahadhari ingawa si wote wanaojali. Habari nimeifupisha kuchukua mazitomazito zaidi.

  [​IMG]

  Wakati tukijiandaa kwa mlo ulio mbele yenu ningependa kuwaeleza mafupi juu ya sumu na jinsi sumu inavyoweza kuingia kwenye mwili wako na hatimaye kukudhuru. Na bila shaka wote mnajua kuwa sumu inaua.


  Ni hivi; unaweza kuwekewa sumu. Usipoiona na ukaiacha, basi, utakuwa umepona. Ndio, kama kuna sumu imewekwa usiichukue. Kwa mantiki hiyo hiyo, jiadhari, unaweza ukashikishwa sumu.

  • Kuwa makini na wanaokupa mikono ya heri, mingine ni mikono ya kifo. Yumkini anayekupa mkono amevaa glovu yenye sumu.
  • Ndugu yangu, unaweza pia ukagusishwa sumu. Kuwa makini na unayecheza nae muziki baada ya mlo huu. Kumbatio la muziki tulivu laweza kugeuka kuwa ni kumbatio la kifo.
  • Sumu inaweza pia kukuingia mwilini kwa kulishwa. Uwe makini na anayekulisha kipande cha keki ya harusi. Na kama waweza kulishwa sumu hivyo hivyo waweza ’ kujilisha’ mwenyewe sumu. Chunga sana na anayekupa kipande cha nyama choma. Ukakipokea na hatimaye kukitia mdomoni.
  • Kama ilivyo kwa kulishwa na kujilisha sumu. Yawezekana pia sumu ikaingia mwilini mwako kwa kunyweshwa au kujinywesha. Chunga sana na unayekaa karibu naye. Jichunge mwenyewe pia. Ukinywa vodka nyingi ni sawa na ’ kujinywisha’ mwenyewe sumu.
  • Sumu yaweza pia kukuingia mwilini kwa kumwagiwa. Kaa mbali sana na atakayefungua champeini isije kilichomo kikawa ni sumu. Na wengine hamfahamu, kuwa sumu yaweza pia kukuingia kwa kupuliziwa. Sahani yako ya chakula yaweza kuwa imepuliziwa sumu…

  Ndugu zangu,
  kuna njia nyingi sana za sumu kuingia mwilini mwako. Naam. Habari kubwa katika siku mbili hizi ni kadhia ya Dr. Mwakyembe na madai ya sumu kuingizwa mwilini mwake na wabaya wake. Na kama mlivyoona hapo juu, bado haijawa wazi kama Mwakyembe kalishwa, kawekewa, kanyweshwa au kagusishwa sumu.
  Jitihada za Jeshi la Polisi juzi kutaka kutuambia WaTanzania ukweli juu ya kadhia hii zinaonekana kugonga mwamba kwa kupingwa vikali na Mwakyembe mwenyewe. Tumesoma kwenye magazeti ya leo.

  Maggid Mjengwa,
  Dar es Salaam.
  Jumapili, Februari 19, 2012.
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Feb 19, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Sa mbona thread hii ipo hapa JF, na ndio kwanza imepandishwa na yeye mwenyewe Maggid, kwanini unaikopi na kupaste?..TUCHANGIE IPI SASA?
   
 3. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #3
  Feb 19, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  labda haukuiona maana vyanzo ni vingi
   
 4. Thomas Odera

  Thomas Odera Verified User

  #4
  Feb 19, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 644
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Kama ndivyo ilivyo basi kuepuka sumu iko kazi maana hizo njia ulizotaja ni ambazo tunatumia katk maisha ya kila siku
   
 5. Mkereketwa_Huyu

  Mkereketwa_Huyu JF-Expert Member

  #5
  Feb 19, 2012
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 5,115
  Likes Received: 1,206
  Trophy Points: 280
  Huyu Mjengwa namfagilia sana kwani he has the best news always as opposed to some blogger wanna bees whom I do not wish to mention their names. Pia namsikitikia kwani uwazi wake waweza kumfanya yeye mwenyewe kulishwa sumu na mashushushu wa kibongo. Si mnajua Bongo watu hawapendi kuambiwa ukweli bali wanataka kuendekeza uozo Wa kudanganyana na kubezana bila sababu. Mjengwa, jichunge na sumu!
   
Loading...