Mjema atuma salamu zenye maelekezo manne kote nchini

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Jan 12, 2019
328
414
Na Bwanku M Bwanku.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Ndugu Sophia Mjema ameacha ujumbe wenye maelekezo manne wakati wa kuhitimisha ziara ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo na Sekretarieti yake mkoani Singida.

Mjema ameacha ujumbe huo kwenye mkutano mkubwa wa hadhara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo aliyeambatana na Sekretarieti yake na viongozi wengine mbalimbali wa Kitaifa wa vijana na mkoa wa Singida kwenye viwanja vya Bombadia Jana Jumamosi Machi 04, 2023.

Kwanza, Mjema ametoa maelekezo kwa viongozi wote nchini kwamba kwasasa maelekezo ni kuendelea kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua kwa mwendo wa papo kwa papo bila kusubili.

Pili, akasema mambo ambayo wananchi wanaona hawana pa kwenda basi CCM iwe ndio kimbilio la wananchi kote nchini.

Zaidi akasisitiza mikutano ya mashina iendelee kote nchini na ishuke mpaka ngazi za chini kabisa kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua pamoja na kuimarisha uhai wa Chama.

Mwisho, akaendelea kuwasisitiza wanaCCM wote kote nchini kuendelea kukisemea Chama na kueleza mipango na yote makubwa yanayofanywa na Serikali inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

-1147179641.jpg
-692941993.jpg
703522916.jpg
-971804158.jpg
 
..bila kusahau agizo la KM Chongolo kwamba waliomaliza vyuo vikuu waende VETA ili waweze kuajiriwa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom