Mje mnishauri ninaweza kumwacha mtoto wa mtu kwenye mataa

Niambie Tu

Senior Member
May 29, 2022
162
272
Wakuu.

Mimi naona mapenzi yaenda kunishinda.

Kuna mwanamke ilitokea nilimpa ujauzito mwaka jana nikamwambia usitoe mimi ntalea kipindi hiko niko nae mkoa yeye alikuja kunisalmia na sikujiandaa kuwa na mtoto kwa wakati huo japo nilikuwa nafanya kazi isiyokidhi mahitaji.

Mwaka huohuo mimi nikapata kazi mjini, ikabidi nimwache aendelee na miradi ambayo nilimfungulia kabla sijaondoka. Baada hali ya ujauzito kumsumbua sana ikabidi nimwambie nae aje mjini aachane na miradi tutakuja kufanya huku japo ilikuwa haijasimama.

Baada ya kuendelea kuishi nae nikamfungulia duka na mimi nikaendelea na kazi, Mungu amesaidia Kujifungua tumepata mtoto ila kiukweli kilichonileta hapa Jf huyu binti wakuu hayupo kabisa moyoni naona najiforce kumpenda na hatuachi kugombana leo kesho.

Wazazi wake sijui hata wako upande gani maana tangia ajifungue hawajawahi kukanyaga hapa alipo wao wanaulizia mahali nitatoa lini wakati wanaelewa hali halisi ya uchumi wangu nilitoa barua.

Natamani nimwache tu, anilelee watoto wangu tu maana mimi malengo ya maisha yangu sijafukia hata Robo na ninaona uwezo wake ni mdogo wa mimi kuendelea kuwa nae.

Hiko hivi nilimwambia asitoe mimba kiukweli mimi niliweka nadhiri mwanamke akipata mimba yangu sitaitoa, huyu dada nilikuwa nae kwenye mahusiano ila sio seriously maana ilipita muda kila mtu akawa na mishe zake.

Mwaka jana tulirudisha mawasiliano akatoroka kazini kwake na kuja kwangu na mwisho akijikuta amekaa kwangu mwezi, kiukweli sikujiandaa kabisa kwa hili.

Sasa nina hasira nae na tunagombana muda wote na mambo yangu naona hayaendi tu.
 
Sawa. Assume wewe ni mzazi, una mtoto wa kike ambae amepewa ujauzito. Aliempa huo ujauzito amemwambia asitoe. Binti akatii, akajifungua salama alafu jamaa anasema binti hayuko moyoni kwake kabisaaaa, anataka amuache!

Usinipe jibu ngedere wewe. Baki nalo!

Alafu kesho kutwa urudi hapa kuwatukana single maza. Laana nyingine huwa mnajitakia tu. Kiukweli baada ya kusoma uzi wako, nimeanza kubadili mawazo kuhusu single maza!
 
Wewe nadhani umeanza kupata vihela na sasa unadhani huyo binti siyo wa level yako. Sasa unataka pisi kali a.k.a samaki wa mapambo (ambao kamwe hawaliwi!).

Go on mwache tu maana kuishi na mtu ambaye umeshaacha kumpenda napo ni sawa na kuishi kifungoni. Lakini angalau hakikisha unaendelea kuhudumia hicho kimalaika kisicho na hatia mlichoamua kukileta hapa duniani.

Kwa upande wako wewe Karma itakushughulikia maana dunia ni hii hii na maisha ni haya haya. Siku moja utakaa na kumkumbuka sana huyo binti kuwa pengine ndiye binti pekee aliyewahi kukupenda kikweli hapa duniani.

Kwa sasa mwache aende akateseke huko huku akichekwa na kudhihakiwa na jamii kwa kuwa singo maza.

Mungu na Akusaidie 🙏🏿🙏🏿🙏🏿
 
Wakuu.

Mimi naona mapenzi yaenda kunishinda.

Kuna mwanamke ilitokea nilimpa ujauzito mwaka jana nikamwambia usitoe mimi ntalea kipindi hiko niko nae mkoa yeye alikuja kunisalmia na sikujiandaa kuwa na mtoto kwa wakati huo japo nilikuwa nafanya kazi isiyokidhi mahitaji.

Mwaka huohuo mimi nikapata kazi mjini ,ikabidi nimwache aendelee na miradi ambayo nilimfungulia kabla sijaondoka baada hali ya ujauzito kumsumbua sana ikabidi nimwambie nae aje mjini aachane na miradi tutakuja kufanya huku japo ilikuwa haijasimama.

Baada ya kuendelea kuishi nae nikamfunfungulia duka na mimi nikaendelea na kazi, Mungu amesaidia Kujifungua tumepata mtoto ila kiukweli kilichonileta hapa Jf .

Huyu binti wakuu hayupo kabisa moyoni naona najiforce kumpenda na hatuachi kugombana leo kesho.

Wazazi wake sijui hata wako upande gani?maana tangia Ajifungue hawajawahi kukanyaga hapa alipo wao wanaulizia mahali nitatoa lini wakati wanaelewa hali halisi ya uchumi wangu nilitoa barua.

Natamani nimwache tu,anilelee watoto wangu tu maana mimi malengo ya maisha yangu sijafukia hata Robo na nina ona uwezo wake ni mdogo wa mimi kuendelea kuwa nae.
Aiseh yani sijui nkuite mjinga au zombie.
Hapa ndani kila siku wanaume wanawatukana na kuwabeza single maza ooh sijui nin na nin, Wakati hao single mother wamepatikana kwa namna hii.
Nafikilia ety mdg angu anafanyiwa hivi mhhh lbd nisijue.
 
Kwanini ulitaka "asitie mimba" huku huna mpango nae?

To yeye njoo uone akili za "Future husband" wenu.

Braza sorry, ila una fuvu kubwa limejaa mchanga wa kuharibu maisha ya binti za watu.

#YNWA
Brother! Mi Mungu anikomboe....nione tu nacomment ujinga humu but Nina hasira na wanaume balaa....Mume wangu aje atoke kwa Bwana...amfunge kilakitu kitakachomfanya asikate tamaa juu yangu.Mi ni mwanamke bora tu ila nilishaharibiwa kichwa na mwanaume aliyenipa mimba na baadae kusema nitoe na kunikimbia saivi analilia mtoto.Teh! Mi mvumilivu sana ila nikiingiza chuki sivumilii hata nusu ya kosa.Nina jazba natamani badala ya kuandika comment mngeniona ninavyoongea kwa sauti huku nikivuja kamasi za hasira😭😭😭😡😡😡😠😠
 
Wakuu.

Mimi naona mapenzi yaenda kunishinda.

Kuna mwanamke ilitokea nilimpa ujauzito mwaka jana nikamwambia usitoe mimi ntalea kipindi hiko niko nae mkoa yeye alikuja kunisalmia na sikujiandaa kuwa na mtoto kwa wakati huo japo nilikuwa nafanya kazi isiyokidhi mahitaji.

Mwaka huohuo mimi nikapata kazi mjini ,ikabidi nimwache aendelee na miradi ambayo nilimfungulia kabla sijaondoka baada hali ya ujauzito kumsumbua sana ikabidi nimwambie nae aje mjini aachane na miradi tutakuja kufanya huku japo ilikuwa haijasimama.

Baada ya kuendelea kuishi nae nikamfunfungulia duka na mimi nikaendelea na kazi, Mungu amesaidia Kujifungua tumepata mtoto ila kiukweli kilichonileta hapa Jf .

Huyu binti wakuu hayupo kabisa moyoni naona najiforce kumpenda na hatuachi kugombana leo kesho.

Wazazi wake sijui hata wako upande gani?maana tangia Ajifungue hawajawahi kukanyaga hapa alipo wao wanaulizia mahali nitatoa lini wakati wanaelewa hali halisi ya uchumi wangu nilitoa barua.

Natamani nimwache tu,anilelee watoto wangu tu maana mimi malengo ya maisha yangu sijafukia hata Robo na nina ona uwezo wake ni mdogo wa mimi kuendelea kuwa nae.
Kwa sababu ulisema Niambie Tu naimani wadau washa kuambia.
 
Brother! Mi Mungu anikomboe....nione tu nacomment ujinga humu but Nina hasira na wanaume balaa....Mume wangu aje atoke kwa Bwana...amfunge kilakitu kitakachomfanya asikate tamaa juu yangu.Mi ni mwanamke bora tu ila nilishaharibiwa kichwa na mwanaume aliyenipa mimba na baadae kusema nitoe na kunikimbia saivi analilia mtoto.Teh! Mi mvumilivu sana ila nikiingiza chuki sivumilii hata nusu ya kosa.Nina jazba natamani badala ya kuandika comment mngeniona ninavyoongea kwa sauti huku nikivuja kamasi za hasira
Una hasira halfu unataka mume atoke kwa bwana.
 
Back
Top Bottom