Amani ya Bwana Mungu iwe nanyi wapendwa.
Katika maisha kujitambua na kufikiria kuwa unahitaji kuwa nani huwa inasaidia sana na haswa ukiwaza uzao wako unataka uwaje kimaisha.
Niwaombe radhi ambao kwa namna moja au nyingine huwa hawapendi sana kujadili taswira za maisha yao baadae au baada ya uzee.
Wapendwa huu ni msimu wa mvua karibia mikoa yote Tanzania na kila mkoa kuna kila aina ya fulsa ambazo nyingi bado hatujaziona na kama tumeziona basi hatujaamua kuzikimbilia huenda kwa kuzitambua au kutozitambua. Mfano, vijana wenzangu tunaotokea mikoa ya Iringa, Njombe, Tanga, Arusha, Mbeya nk. Mikoa tajwa inafulsa za kilimo cha miti, ndizi, mahindi nk na ardhi iwe ya urithi au ya kununua inapatikana.
Ombi langu vijana kama unafanya kazi omba ruhusa au chukua likizo msimu huu nenda kalime, kapande miti, kapande migomba ya kutosha au zao linalopatikana kwenye eneo ambalo upo familia nalo, panda mazao ya mda mfupi na pia panda mazao ya mda mrefu na hakikisha unayatunza na kuyalinda kwa gharama yoyote ile.
Vijana huu ndo mda wa kuuandaa uzee wako huko mbeleni uweje. Tuache tabia za kuangalia mali za wazazi bali tutafute mali zetu kwa bidii na Mungu atabariki mazao ya mashamba yetu, tuache kuchukua likizo au ruhusa za misimu ambayo haina uzalishaji na kuishia kuuza sura tu kula kulala.
Mwisho ombeni sana kuwa na afya na tujitunze ila tusisahau kuwa wewe ni baba wewe ni mama je unatamani uje uishi maisha gani na familia yako au uzeeni mwako.
Mda ndo huu jiulize unataka uje uishi maisha gani huko mbeleni??? Tumia afya yako sasa kutafuta neema ya uzeeni.
Mungu awabariki sana kwa kila wazo jema ambalo unahitaji kulifanya mkono wa Bwana usikupungukie.