Mjapan: Kwa kasi hii ya maendeleo Rais Magufuli alistahili kuishi Japan maana anaamini katika kazi siyo siasa

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,840
141,765
Injinia mmoja wa kijapan pale Mwenge - Morocco project amemmwagia sifa Rais Magufuli na kusema huyu Dr Magufuli anaamini katika kazi kama wajapan.

Tanzania na Afrika kwa ujumla mna bahati ya kupata kiongozi anayeamini katika kazi na siyo porojo za kisiasa, amesema.

Mjapani ameniuliza kama hawa wanasiasa wa Chadema na CCM ni wafanyaji kazi kweli au wanaishi kwa kutumia mdomo ( kuongea) tu?.....nikamjibu wapo baadhi wana kazi zao hata Kiongozi mkuu wa upinzani ni mfanyabiashara mkubwa tu hapa nchini.

Mwisho mjapan ameniambia maendeleo yanayoletwa na Rais Magufuli yataifanya Tanzania iwe ni nchi ya kupigia mfano, muungeni mkono.

Huyu mjapan tumekuta pale jirani na Maryland nikamdadisi mawili matatu kuhusu ujenzi unaoendelea wa barabara.

Maendeleo hayana vyama
 
Okay okay!!! That nice, Magu Rais wa ujenzi. Makandarasi wanapata malipo yao kwa wakati.
Wanasifu, wataabudu pia
 
Back
Top Bottom