Mjane wa Erasto Msuya apandishwa Kizimbani Kisutu

hazipotei mkuu huenda huelewi zipo adhabu zinazoonekana kwenye ulimwengu wa damu na nyama ambazo wewe umekariri ila pia zipo adhabu zinazotolewa na hakimu wa haki ambaye ni Mungu huenda wewe huzijui hizo
Usisahau kwamba hata wauaji wanaungama mbele ya Mungu na wanasamehewa vile vile!
 
Msuya.png


Miriam Stephen Mrita (41), ambaye alikuwa mke wa marehemu Bilionea Msuya, amefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akikabiliwa na shtaka la mauaji ya dada wa bilionea Erasto Msuya, Aneth Msuya.
msuya2.png

Wakili wa Serikali, Diana Lukondo alidai mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Margareth Bankika kuwa Mei 25, 2016 katika eneo la Kibada, Kigamboni jijini Dar es Salaam, mshtakiwa huyo alimuua Aneth.

Baada ya kusomewa shtaka hilo, Miriam hakuruhusiwa kujibu chochote kwa sababu mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi za mauaji.

Upande wa mashtaka ulidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika na iliahirishwa hadi Septemba 6.

Mshitakiwa alirudishwa rumande kwakuwa kesi hiyo haina dhamana.Aneth, ambaye ni dada wa bilionea Erasto Msuya, aliuawa kwa kuchinjwa na watu wasiojulikana Mei 25, 2016 nyumbani kwake Kibada, Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Chanzo: Gazeti la Mwananchi

Maswali:
1. Huyu Miriam Stephen Mrita ni nani?
2. Huyu mama ndiye aliyeshika kisu na kumchinja mtu kweli?
3. Hii haitakuwa kama ile kesi ya Zombe?
4. Nadhani wapelelezi wabadilishe shtaka.
 
Habari ninayokupa ni ya uhakika. Naifahamu familia kwa karibu. Na mkasa wote wa mauaji. Huyo marehemu Anathe kaka yake marehemu Erasto alimuandika jina lake katika mali zake nyingi. Kwahiyo nadhani akawa anamnyima usingizi wifi.
inawezekana ikawa kweli.Maana tunaambiwa during mauaji documents zilikutwa zimevurugwa..meaning kuna kitu walikuwa wanakitafuta hapo.Sad sad...haki itendeke kwakweli
 
Kibongo bongo kutajwa tu inaweza kutosha kabisa.

Si umesikia kuna habari zinasema kuwa eti yule mdada wa kazi ndo alimtaja...

Sasa hapa najiuliza...huyo wifi atakuwa ju.ha kiasi gani kumhusisha mdada wa kazi kwenye mpango wa kutoa uhai wa wifi yake?

Pia, huyo mdada wa kazi anasema ukweli kiasi gani? Manake isije ikawa naye anadanganya ili asiendelee kupata joto ya jiwe.

Anyway, nadhani wengi wetu hatuujui ushahidi walionao polisi...hivyo labda wana zaidi ya tunavyojua sisi.
Binafsi akili inagoma kabisa kukubali kuwa huyu mjane wa Erasto ndio muhusika
 
Nadhani hii inaweza kuwa conclusion ya kijiweni. Sasa kama alikuwa ameandika jina lake kwenye mali hata kama angeuawa isingebadilisha kitu. Tuombe tu upelelezi wa hii kesi usiwe unaongozwa na fedha bali haki.
Kulikuwa na kesi ya mirathi mahakamani, na dada wa marehemu ameandikwa kwenye mali. kwahiyo utaona kwa akili ya kijinga kumuua walidhani ndio itakuwa suluhisho la wao kupata mali zote.
 
Hapo unaongea mambo 2 tofauti...kuna sheria na offiside kumbuka.......huyu marehemu kumbuka alikua anafanya bank na bado mirathi ilikua bado haijakamilika manake mirathi inakamilika namna gani wakati kesi iko mahakamani??
Sio sheria za mirathi. Kama mdogo mtu ni signatory wa account anaweza ku freeze mpaka mirathi imalizike. Tatizo likowapi hapo.
 
Back
Top Bottom