Mjane wa Daudi Mwangosi akanusha vikali habari za Dr Slaa kutelekeza ahadi yake kwa familia hiyo

Kwani Habari Leo au Tazama ni magazeti ua nepi za mafisadi? Kule wamejaa machangudoa wa kimaadili wakiuza huduma yao wasijue kesho watalia na kusaga meno watakapopigwa teke kama ganda na chungwa. May they perish!
 
A typical case ya akili ndogo kujaribu kushawishi akili kubwa!! lol. shame be upon you.

najua umeupata ukweli halisi ila kajifunze kiingereza hata cha darasa la tatu halafu ndo uanze kujibu kwa kutumia hiyo lugha
 
Hiyo story atakuwa ameituma Magid, maana alishadadia sana huo msiba na ni mtu wa kujipendekeza kwa magamba.
 
Ifikie wakati itungwe sheria ya kuvichukulia hatua vyombo vya habari viongo. Sasa hii ndio nini? Gazeti limeshasambaa hadi mbali huko, mwenyewe kakanusha sasa kinachofuata?

Ubovu wa serikali yetu inapenda vyombo mufilisi kama hivi huku vinafungia magazeti muhimu kama mwanahalisi. Ila poa 2015 sio mbali tuombe mungu.
 
Huu uandishi wa namna hii ndo unaozidi kuporomosha heshima ya waandishi wa habari, hii fani imevamiwa na makanjanja!!!!
 
Hivi magazeti kama Habari Leo, Uhuru na Mtanzania, yapo kwa masilahi yapi? Yabadilike magazeti haya. Si wote tunapenda Propaganda hizi zisizokukwa na mashiko kwa maendeleo ya taifa hili.
Kuna radio moja binafsi, haya magazeti ndio huwa inayapitia tu asubuhi vichwa vyake. Huwa naisikilza maana kuna maeneo inapatikana hiyo tu, lakini ikianza habari za magazeti, nazima kwanza.
 
Mkuu, nimecopy na kupaste ili great thinkers waangalie pande zote mbili za shilingi, bado najipendekeza kwa Chadema? Nashukuru pia kwa matusi yako.

Aweda na wewe vipi? Mtu anakutukana bado unamwita mkuu! Huyo ni M.W.E.H.U.
 
Back
Top Bottom