Mjane wa Daudi Mwangosi akanusha vikali habari za Dr Slaa kutelekeza ahadi yake kwa familia hiyo

Mbunge msigwa baada ya habari ya ukweli kuhusu ahadi ya slaa amefuatwa na kulambishwa sukari halafu palepale anatakiwa azikanushe hizo habari kwani walijua zinamchafua kwa kiasi kikubwa dk slaa sasa jiulize kama kweli amekanusha bila shinikizo lolote toka chadema ni kwa nini azikanushe akiwa na mbunge wa chadema mh.msigwa?ama kweli mama mwangosi umekuwa kama mpira wa kona kila mwanasiasa anayetafuta umaarufu anakuja kwako kupata ujiko wa kisiasa.
 
Wanasheria mpo wapi?
Ni nafac ya huyo mama kudai fidia kwa kuchafuliwa jina lake..
 
  • Thanks
Reactions: MTK
Kizungumkuti!

Hakuna kuzungumkuti hapo, ukweli ndio huo, mjane hakusema hayo yalioandikwa kwenye gazeti la habari leo.
Halafu watu wengi sana pamoja na wewe mkatetea uongo ule bila aibu !!
Shame on you wote mliotetea oungo wa Kimbunga na habari leo.
 
Mjane wa Marehemu Daudi Mwangosi amekanusha vikali habari zilizochapishwa na gazeti la habari Leo kuwa eti yeye alimshutumu Katibu Mkuu wa CDM Dr Wilbroad Slaa kuhusu rambirambi za mumewe.Akiongea na Mbunge wa Iringa mjini Peter Msigwa amesema kwa uchungu mkubwa kuwa amesikitishwa sana kuwa habari hizo hazina ukweli wowote na ni aibu kubwa chombo kikubwa cha habari kama Habari Leo kutoa habari ya uongo kwa viwango hivyo. Mjane huyo amesema kama angekuwa na Shida na Dr Slaa angemtafuta mbunge wa Iringa mjini Peter Msigwa ambaye ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CDM na kwa hapa Iringa yeye na Msigwa ni majirani. Mjane huyo ameendelea kusema kitendo hicho kilichofanywa na gazeti hilo kimeamsha Msiba upya kwake kwani kina lengo la kutaka Jamii imdharau. Anaomba watanzania kuupuza habari hizo na ameshanga ni maadili gani haya ya uandishi na hajui kwa hali hii Taifa linakwenda wapi.
Magamba yamevuliwa mpaka sasa yanataka yamchune mama mwangosi ee Mungu angalia viumbe wako wasio na hatia wanavyoteswa na huyu pepo wa kijani
 
Kitu nacho kifurahia ni hiki; "Hili gazeti la Habari leo na ile TBCCM wasomaji na waangailji wake ni wachache sana, wadau wengi wa habari wanajua habari za vyombo hivyo nyingi ni za kupikwa" kwa minajiri hiyo basi, hiyo habari wala haijasambaa sana!
 
Nilijua tu nii mangumashi za magamba , magamba mtateseka sana mwaka huu atudanganyiki
 
Mbunge msigwa baada ya habari ya ukweli kuhusu ahadi ya slaa amefuatwa na kulambishwa sukari halafu palepale anatakiwa azikanushe hizo habari kwani walijua zinamchafua kwa kiasi kikubwa dk slaa sasa jiulize kama kweli amekanusha bila shinikizo lolote toka chadema ni kwa nini azikanushe akiwa na mbunge wa chadema mh.msigwa?ama kweli mama mwangosi umekuwa kama mpira wa kona kila mwanasiasa anayetafuta umaarufu anakuja kwako kupata ujiko wa kisiasa.

Haya kaka umeshaingiza siku kapokee ujirawako kwa nape
 
msigwa bwana,nenda kasome kilichosemwa kina ukweli ndani yake,yatafahamika tu
siamini kama kigoma kuna watu wenye kuchangia uharo kama wewe KIGOMA KWETU. naomba ubadili hiyo username maana unadhalilisha mkoa kwa manufaa ya kipuuzi. ningekuwa siogopi ban ningekwambia yaliyo mengi ila basi tu! unaweza kuamini ujinga unaoandikwa na habari leo na kuushadadia?
 
Last edited by a moderator:
Mjane wa Mwangosi amewakosea nini CCM hadi wamandame kiasi hicho? Jeshi la polisi ambalo liko chini ya serikali ya CCM limemuuwa mume wake kwa kumpiga bomu wakati yuko kazini, mwezi mmoja baadae gazeti la CCM linamgeuza huyu mama kuwa 'kitega uchumi'! Why?

Hivi mhariri wa Habari Leo anaelewa madhara ya huu mkakate wake kwa huyu mjane na watoto wa marehemu Mwangosi? She is still trying to come to terms with the brutal killing of her husband, sasa anaamka asubuhi anajikuta kaingizwa kwenye malumbano kwa sababu watu wanataka kuuza magezeti? Huu ni uonevu wa hali ya juu.
 
Mungu wetu aliye sirini ndiye ajua nini kilicho katikati.mama Mungu akusaidie na akutie nguvu maana yeyeni mme wa wajane na ni mfariji wawajane
 
Mjane wa Marehemu Daudi Mwangosi amekanusha vikali habari zilizochapishwa na gazeti la habari Leo kuwa eti yeye alimshutumu Katibu Mkuu wa CDM Dr Wilbroad Slaa kuhusu rambirambi za mumewe.

Akiongea na Mbunge wa Iringa mjini Peter Msigwa amesema kwa uchungu mkubwa kuwa amesikitishwa sana kuwa habari hizo hazina ukweli wowote na ni aibu kubwa chombo kikubwa cha habari kama Habari Leo kutoa habari ya uongo kwa viwango hivyo.

Mjane huyo amesema kama angekuwa na Shida na Dr Slaa angemtafuta mbunge wa Iringa mjini Peter Msigwa ambaye ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CDM na kwa hapa Iringa yeye na Msigwa ni majirani.

Mjane huyo ameendelea kusema kitendo hicho kilichofanywa na gazeti hilo kimeamsha Msiba upya kwake kwani kina lengo la kutaka Jamii imdharau.

Anaomba watanzania kuupuza habari hizo na ameshanga ni maadili gani haya ya uandishi na hajui kwa hali hii Taifa linakwenda wapi.

Baba yao yuko Canada anatembezwa na farasi,magamba bwana!
 
Nayashangaa sana magazeti ya namna hii, waandishi wa habar wengine wanaonekana hawana maadili kbs mna aibisha nchi yetu na taifa kwa ujumla pole sana mama.
 
Mjane wa Marehemu Daudi Mwangosi amekanusha vikali habari zilizochapishwa na gazeti la habari Leo kuwa eti yeye alimshutumu Katibu Mkuu wa CDM Dr Wilbroad Slaa kuhusu rambirambi za mumewe.

Akiongea na Mbunge wa Iringa mjini Peter Msigwa amesema kwa uchungu mkubwa kuwa amesikitishwa sana kuwa habari hizo hazina ukweli wowote na ni aibu kubwa chombo kikubwa cha habari kama Habari Leo kutoa habari ya uongo kwa viwango hivyo.

Mjane huyo amesema kama angekuwa na Shida na Dr Slaa angemtafuta mbunge wa Iringa mjini Peter Msigwa ambaye ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CDM na kwa hapa Iringa yeye na Msigwa ni majirani.

Mjane huyo ameendelea kusema kitendo hicho kilichofanywa na gazeti hilo kimeamsha Msiba upya kwake kwani kina lengo la kutaka Jamii imdharau.

Anaomba watanzania kuupuza habari hizo na ameshanga ni maadili gani haya ya uandishi na hajui kwa hali hii Taifa linakwenda wapi.

Pole sana Mama Mwangosi, habari leo ni kijarida cha magamba ya CCM ambao vikaragosi vyake ndio vilivyokatisha uhai wa Mume wako! wapuuze, Mungu atakuponya vidonda vyako vya roho, akili na mwili. Kuna siku utapata faraja ya kudumu.
 
Wako wapi akina Ritz, Mafilili, Kimbunga, na wengineo ??
Vipi wana JF ??
Hapo vipi ??
 
Mbunge msigwa baada ya habari ya ukweli kuhusu ahadi ya slaa amefuatwa na kulambishwa sukari halafu palepale anatakiwa azikanushe hizo habari kwani walijua zinamchafua kwa kiasi kikubwa dk slaa sasa jiulize kama kweli amekanusha bila shinikizo lolote toka chadema ni kwa nini azikanushe akiwa na mbunge wa chadema mh.msigwa?ama kweli mama mwangosi umekuwa kama mpira wa kona kila mwanasiasa anayetafuta umaarufu anakuja kwako kupata ujiko wa kisiasa.

A typical case ya akili ndogo kujaribu kushawishi akili kubwa!! lol. shame be upon you.
 
Ama kweli ukistaajabu ya mussa utaona....gazeti kubwa na makini kama habari leo linaonekana kutaka kufukia madhambi ya serikali kwa mgongo wa CDM
 
serikali ya magamba inaweweseka damu ya mwangosi inalia ole wenu magamba, mliomwaga damu isiyo na hatia!!
 
Habari zingine siyo za kuzitilia maanani.Hivi kweli nikiasi gani ambacho dr.slaa au viongozi wa cdm wanaweza kushindwa kutoa kwa mjane kama siyo kutaka kufunika kombe mwanaharam apite!
 
Back
Top Bottom