Mjane wa Daudi Mwangosi akanusha vikali habari za Dr Slaa kutelekeza ahadi yake kwa familia hiyo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mjane wa Daudi Mwangosi akanusha vikali habari za Dr Slaa kutelekeza ahadi yake kwa familia hiyo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mikael P Aweda, Oct 5, 2012.

 1. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #1
  Oct 5, 2012
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Habari hii nimeichukua ktk facebook wall ya mchungaji Peter Msigwa na nimecopy na kupaste.

  Mjane wa Mwangosi amekanusha vikali habari zilizochapishwa na gazeti la habari Leo kuwa eti yeye alilia rambirambi za Slaa. Akiongea alipokuwa nyumbani kwangu kwa uchungu amesikitishwa sana kuwa habari hizo hazina ukweli wowote na Kama angekuwa na Shida na Dr Slaa angenitafuta Mimi.

  Kwanza ni jirani yake na pili anajua ukaribu wangu na Dr. Anasema kitendo hicho kimeamsha Msiba kwani kina lengo la kutaka Jamii imdharau. Anaomba watanzania kuupuza habari hizo na ameshangaa ni maadili gani haya ya uwandishi. Naomaba kuwasilisha

  Haya ni maelezo niliyochukua kutoka ktk uzi aliouanzisha msemaji wa Chadema Molemo + picha  My take;
  Kama gazeti la habari leo linaweza kupotosha umma namna hii kwa kutumia kodi zetu, basi kazi tunayo kama nchi.
   
 2. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #2
  Oct 5, 2012
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Watani hawataki mchezo ni uzushi tuuu kwenda mbele!!
   
 3. k

  kibali JF-Expert Member

  #3
  Oct 5, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 315
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  bongo bana kila kitu siasa tu!
   
 4. k

  kibali JF-Expert Member

  #4
  Oct 5, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 315
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Leo gazeti limeuza sana kisa hii habari..........Waandishi wetu uchwara sana kama ile ya "watoto wa wasiza wajiunga chadema"
   
 5. Mtego wa Noti

  Mtego wa Noti JF-Expert Member

  #5
  Oct 5, 2012
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 2,231
  Likes Received: 136
  Trophy Points: 160
  hilo gazeti nalo lifungiwe
   
 6. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #6
  Oct 5, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Hilo gazeti lina haja ya kuchunguzwa kwa kina sana!

  Hauwezi kuwaandikia umma mambo kama haya yaliyona ukweli hata chembe!

  Halipendezi hata kidogo!
   
 7. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #7
  Oct 5, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,481
  Likes Received: 5,861
  Trophy Points: 280
  At least hilo la hao watoto wasiza (whatever this means..itake it watoto wa Wassira) lina ukweli
   
 8. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #8
  Oct 5, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,540
  Likes Received: 10,467
  Trophy Points: 280
  Kizungumkuti!
   
 9. Bartazar

  Bartazar JF-Expert Member

  #9
  Oct 5, 2012
  Joined: Oct 4, 2011
  Messages: 805
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 45
  Sasa hapa tulipofika hata kama ni siasa baaaasi, enough is enough...
   
 10. Victoire

  Victoire JF-Expert Member

  #10
  Oct 5, 2012
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 10,453
  Likes Received: 7,219
  Trophy Points: 280
  jamani wamwache mama wa watu aomboleze,Mme wake kaondoka bila kutegemea,hana kazi ana watoto.Wamwache wasimfanye mtaji wa kuuzia magazeti yao
   
 11. M

  Molemo JF-Expert Member

  #11
  Oct 5, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Mjane wa Marehemu Daudi Mwangosi amekanusha vikali habari zilizochapishwa na gazeti la habari Leo kuwa eti yeye alimshutumu Katibu Mkuu wa CDM Dr Wilbroad Slaa kuhusu rambirambi za mumewe.

  Akiongea na Mbunge wa Iringa mjini Peter Msigwa amesema kwa uchungu mkubwa kuwa amesikitishwa sana kuwa habari hizo hazina ukweli wowote na ni aibu kubwa chombo kikubwa cha habari kama Habari Leo kutoa habari ya uongo kwa viwango hivyo.

  Mjane huyo amesema kama angekuwa na Shida na Dr Slaa angemtafuta mbunge wa Iringa mjini Peter Msigwa ambaye ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CDM na kwa hapa Iringa yeye na Msigwa ni majirani.

  Mjane huyo ameendelea kusema kitendo hicho kilichofanywa na gazeti hilo kimeamsha Msiba upya kwake kwani kina lengo la kutaka Jamii imdharau.

  Anaomba watanzania kuupuza habari hizo na ameshanga ni maadili gani haya ya uandishi na hajui kwa hali hii Taifa linakwenda wapi.


  [​IMG]
   
 12. sop sop

  sop sop JF-Expert Member

  #12
  Oct 5, 2012
  Joined: May 2, 2012
  Messages: 650
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Mjane wa Mwangosi alilia rambirambi za Slaa

  UTAMADUNI mpya wa siasa za misibani, unaoendana na mauaji yaliyotokana na ukaidi wa wanasiasa kwa Jeshi la Polisi, umeanza kuiumbua Chadema ambayo imejikuta ikishindwa kutimiza ahadi ndogo ndogo za kutoa rambirambi inazoahidi kwa wafiwa.

  Juzi, mjane wa mwandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha Channel Ten, Daudi Mwangosi, Aneti, alijikuta akiomba wanahabari wasaidie kufuatilia rambirambi iliyoahidiwa na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa kutokana na kiongozi huyo, kukata mawasiliano baada ya msiba.

  “Nina mawasiliano na Profesa Mark Mwandosya ambaye pia aliahidi kumsomesha mtoto mmoja, yeye aliniambia nitakapokuwa tayari nimjulishe ili atume fedha kwenye akaunti ya shule, lakini sina mawasiliano na Dk Slaa,” alisema Aneti.

  Mwangosi aliuawa Septemba 2 mwaka huu, kwa k

  upigwa na kitu kinachodaiwa kuwa ni bomu katika Kijiji cha Nyololo, wilayani Mufindi mkoani Iringa.

  Aliuawa wakati Polisi ikizuia wafuasi na viongozi wa Chadema kufanya mikutano ya hadhara ambayo ilipigwa marufuku ili kuruhusu shughuli ya Sensa ya Watu na Makazi, kufanyika bila kuingiliwa.

  Baada ya mauaji hayo, wakati wa maziko ya mwandishi huyo, Dk Slaa aliahidi kubeba jukumu la kusomesha mtoto wa kwanza wa Mwangosi aitwaye Nehemiah, ambaye yuko kidato cha nne katika Sekondari ya Malangali, Mufindi, Iringa.

  “Mtoto huyu alifika na kutaka kujua sababu za kifo cha baba yake, kwa uchungu huku machozi yakimtoka, nimewasiliana na mdau wangu na kuahidi kubeba jukumu la kumsomesha na pia naahidi kufuatilia ahadi hiyo kwa kipindi chote cha masomo yake,” alinukuliwa Dk Slaa akiahidi.

  Hata hivyo ahadi hiyo, mbali na ukweli kuwa haijatekelezwa, lakini pia hata mawasiliano kati yake na mjane wa Mwangosi hayapo mpaka mjane huyo kuamua kuomba waandishi wamfuatilie.

  Mwingine aliyeahidi kusaidia familia hiyo ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais asiye na Wizara Maalumu, Profesa Mwandosya, ambaye aliiwakilisha Serikali na katika salamu zake za rambimbambi msibani, alisema atabeba jukumu la kusomesha watoto wengine wa

  marehemu huyo.

  Aliahidi pia kufuatilia ahadi za watu wengine katika kuisaidia familia ya Mwangosi kwa kuwa ni ndugu yake na jirani. “Nitahakikisha familia hii inaishi maisha kama ambavyo angelikuwapo baba yao kwa kuhakikisha kila mtoto wa familia hiyo anasoma kwa kila hatua kwa kuzingatia kuwa hao ni sehemu ya familia yangu,” alisema Mwandosya, ambaye pia ni Mbunge wa Rungwe Mashariki (CCM).

  Gazeti hili lilipompigia Dk Slaa simu kujua mipango yake ya kutekeleza ahadi hiyo, simu yake ilikuwa inaita mara zote bila kupokewa.

  Rambirambi zingine Wakati huo huo, wafanyakazi wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) mkoani Iringa, wametoa rambirambi zao kwa mjane huyo. Mhasibu Mkuu wa Tanroads Iringa, Alex Mgeta alikabidhi Sh 265,000 juzi katika nyumba yao iliyopo Kihesa Bwawani mjini hapa.

  “Nashukuru sana lakini pia nawaomba kwa kupitia michango ambayo nimeambiwa inaendelea kukusanywa mnisaidie nimalizie nyumba hii,” alisema Aneti.

  Aneti alisema nyumba hiyo yenye vyumba vinne vya kulala haijakamilika na ikikamilika, atapangisha baadhi ili kiasi cha fedha atakachopata kitumike kuendesha familia yake.

  Septemba 30 katika harambee iliyofanyika Iringa kwa mujibu wa blogu ya Mjengwa, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Kabwe Zitto alijitolea kumchangia mjane huyo kwa kumlipia ada ya uanachama wa Bima ya Afya kila mwezi kwa miaka mitatu mfululizo.

  Alikaririwa akisema: "Nimeona nami niunge mkono harambee hii. Pamoja na michango ya fedha iliyotolewa kumsaidia mjane kuanzisha mradi wa kujikimu, naona ni muhimu akawa na uhakika wa huduma ya afya yake na watoto wake wanne.

  Hivyo, mchango wangu utakuwa ni kwenye eneo hilo la Bima ya Afya kwa miaka mitatu.
  "Baadhi ya watu wengine maarufu waliojitokeza kumchangia mjane kupitia mtandao wa kijamii wa Mjengwablog.com ni pamoja na Shy-Rose Bhanji, Ananilea Nkya, John Bukuku na Mobhare Matinyi aliyepata kuwa Mhariri wa Majira.
   
 13. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #13
  Oct 5, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,134
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Katika yale magazeti yaliyoitwa Vigazeti Uchwara na waandishi Uchwara na aliyekua Raisi wa awamu ya tatu Muheshimiwa Benjamini Mkapa basi moja ya magazeti hayo ni hili gazeti la Habari Leo!
   
 14. KIJOME

  KIJOME JF-Expert Member

  #14
  Oct 5, 2012
  Joined: Jun 7, 2012
  Messages: 3,079
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  nasikitika sana kwa haya mambo ya kipuuzi,ila ipo siku kodi zetu zitaheshimiwa....kwa habari hii ya udaku waandishi wote wa habari leo na vibaraka wengine ni makanjanja,shen..zi taipu.
   
 15. sop sop

  sop sop JF-Expert Member

  #15
  Oct 5, 2012
  Joined: May 2, 2012
  Messages: 650
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Kumbe na dr slaa ni tapeli,hahahahahahahahaah,nilikuwa sijui kama kuna mapadre matapeli
   
 16. Mkirua

  Mkirua JF-Expert Member

  #16
  Oct 5, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 5,667
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Nilisema ile habari ni ya kipashkuna hata ukiisoma utagundua imepikwa na mwanafunzi wa kova asiyejua hata kudanganya wenye akili.
   
 17. ntogwisangu

  ntogwisangu JF-Expert Member

  #17
  Oct 5, 2012
  Joined: Nov 25, 2011
  Messages: 516
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  Aweda in action!!!we acha kujipendekeza!!!!
   
 18. U

  Uswe JF-Expert Member

  #18
  Oct 5, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,201
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135

  Tunahitaji kufanya kitu, tunahitaji kujua Ukweli na kulifikisha mahakani hili gazeti kwa kuandika uongo, bila hivi hawatajifunza kamwe!
   
 19. piper

  piper JF-Expert Member

  #19
  Oct 5, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 3,260
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Makajanja wanaharibu taaluma ya habari, udaku unatakiwa kwenda kwenye magazeti ya udaku
   
 20. +255

  +255 JF-Expert Member

  #20
  Oct 5, 2012
  Joined: Jan 1, 2012
  Messages: 1,909
  Likes Received: 285
  Trophy Points: 180
  Hivi P. Msigwa = W. Slaa?
  Mbona anajipendekeza kukanusha issue isiyomuhusu au yeye Msigwa ndo aliyetoa ahadi?
   
Loading...