silent lion
JF-Expert Member
- Feb 28, 2012
- 1,161
- 1,539
Wakuu naomba tujadili suala hili kwa kina.
Huyu Mjane alikua anaishi kwenye nyumba ya serekali. Baada ya mumewe kufariki alipewa notisi ya kuhama.
Alifanya jitihada kubwa ya kuiomba Serikali imfikirie na imuachie akae katika nyumba hio ambayo inaonekana walitumia gharama kubwa kuiremba na kuitia mapambo ya kila aina. Hata hivyo ombi lake lilitupiliwa mbali.
Kwa hasira na yeye akang'oa kila kitu kuanzia tiles, gypsum, switch za umeme na hata rangi za ukutani.
Hivyo sasa hivi anatafutwa ili awajibike.
Wito wangu kwa serekali, imuonee huruma mjane huyu na si vizuri kuwanyanyasa wajane na mayatima.
Wito wangu kwa Vijana, tukumbuke kujenga makazi yetu kwani hakuna ajuae kesho itakuwaje.
=============
Kabla mke wa aliyekuwa jaji mkuu wa Zanzibar, marehemu Mkusa Isack Sepetu, Salma Mkusa alitoa malalamiko akidai kwamba shirika la nyumba Zanzibar lilimtaka kuhama na kukabidhi funguo za nyumba waliyokuwa wakiishi na marehemu mume wake maeneo ya michenzani block namba 9.
Aliiomba serikali na shirika la nyumba kutafuta utaratibu sahihi na wa haki juu ya hilo. Alisema hakuwa na deni na mume wake hakua nalo. Anadai majungu mengi yalipikwa kwamba nyumba inatakiwa na serikali na ni mtu mkubwa anahitaji nyumba hiyo.