Mjane wa aliyekuwa Jaji wa Zanzibar, Marehemu Mkusa Isack Sepetu anatafutwa baada ya kuharibu nyumba ya shirika la nyumba Zanzibar

silent lion

JF-Expert Member
Feb 28, 2012
776
1,000
Wakuu naomba tujadili suala hili kwa kina.

Huyu Mjane alikua anaishi kwenye nyumba ya serekali. Baada ya mumewe kufariki alipewa notisi ya kuhama.

Alifanya jitihada kubwa ya kuiomba Serikali imfikirie na imuachie akae katika nyumba hio ambayo inaonekana walitumia gharama kubwa kuiremba na kuitia mapambo ya kila aina. Hata hivyo ombi lake lilitupiliwa mbali.

Kwa hasira na yeye akang'oa kila kitu kuanzia tiles, gypsum, switch za umeme na hata rangi za ukutani.

Hivyo sasa hivi anatafutwa ili awajibike.

Wito wangu kwa serekali, imuonee huruma mjane huyu na si vizuri kuwanyanyasa wajane na mayatima.

Wito wangu kwa Vijana, tukumbuke kujenga makazi yetu kwani hakuna ajuae kesho itakuwaje.
=============

Kabla mke wa aliyekuwa jaji mkuu wa Zanzibar, marehemu Mkusa Isack Sepetu, Salma Mkusa alitoa malalamiko akidai kwamba shirika la nyumba Zanzibar lilimtaka kuhama na kukabidhi funguo za nyumba waliyokuwa wakiishi na marehemu mume wake maeneo ya michenzani block namba 9.

Aliiomba serikali na shirika la nyumba kutafuta utaratibu sahihi na wa haki juu ya hilo. Alisema hakuwa na deni na mume wake hakua nalo. Anadai majungu mengi yalipikwa kwamba nyumba inatakiwa na serikali na ni mtu mkubwa anahitaji nyumba hiyo. 

Kasie

Platinum Member
Dec 29, 2013
18,347
2,000
Aliyekuwa makamu wa Raisi awamu ya Mkapa (Omar Ali Juma), baada ya kufariki familia yake ilitolewa kwenye nyumba Oysterbay.

Serikali hailei wajane, inawahifadhi watumishi wake tuu. Utumishi ukiisha huduma zinakatwa in exception to President, Jaji mkuu na Spika.

Correct me where erroneously stated.
 

Ulweso

JF-Expert Member
May 24, 2016
17,116
2,000
Aliyekuwa makamu wa Raisi awamu ya Mkapa (Omar Ali Juma), baada ya kufariki familia yake ilitolewa kwenye nyumba Oysterbay.
Serikali hailei wajane, inawahifadhi watumishi wake tuu. Utumishi ukiisha huduma zinakatwa in exception to President, Jaji mkuu na Spika.

Correct me where erroneously stated.
Alitolewa ili akae makamu mpya, katolewa sawa lakini anapelekwa wapi kwa muda huo, masikini mfanyakazi wao akishaondoka mlio nyuma yake mnalia mara 2
 

Countrywide

JF-Expert Member
Mar 2, 2015
7,225
2,000
Huyu mama achukuliwe hatua za kinidhamu. Kuremba nyumba na kuibadilisha ni hiari yako hakuna aliyemlazimisha
 

THOMASS SANKARA

JF-Expert Member
Nov 13, 2014
1,867
2,000
Jaji Mkusa Sepetu(1974-2020) hakuwa Jaji Mkuu wa Zanzibar licha ya kuwa aliwahi mara kadhaa kukaimu nafasi ya Jaji Mkuu.
Hadi mauti yanamkuta mwezi february mwaka huu,Jaji Sepetu alikuwa jaji wa Mahakama kuu ya Zanzibar.

Jaji mkuu wa Zanzibar ni Jaji Othman Makungu.

Je aliyefanya uharibifu huu ni Mke mkubwa ama Mdogo Manake Marehemu Jaji Sepetu aliacha Wajane wawili.
 

mng'ato

JF-Expert Member
Oct 27, 2014
28,581
2,000
Aliyekuwa makamu wa Raisi awamu ya Mkapa (Omar Ali Juma), baada ya kufariki familia yake ilitolewa kwenye nyumba Oysterbay.
Jaji Mkuu Ramadhani aliwahi kukalamika baada ya kustaafu miaka kadhaa iliyofuata ulinzi wa serikali uliondolewa nyumbani kwake mpaka ikabidi yeye mwenyewe kwa pesa zake mfukoni awe anamlipa mlinzi wa Co. Binafsi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom