Mjane aliyemlilia Rais Magufuli, akamatwa akiaandaa banda la chakula

Mtarban

JF-Expert Member
Jan 14, 2015
3,818
5,007
  • Mwanasheria wa mwanamke huyo aliyejitambulisha kwa jina la Shukuru Khalifa alisema mteja wake alikamatwa mchana alipokuwa akiandaa banda hilo.


Mwanamke aliyeangua kilio mbele ya Rais John Magufuli wakati wa maadhimisho ya siku ya sheria jijini Dar es Salam, Februari 2, mwaka huu, Swabaha Shosi amekamatwa na polisi mjini hapa akiwa katika Uwanja wa Chongoleani. Swabaha ambaye baada ya tukio hilo alijizolea umaarufu na kupachikwa jina la ‘mjane wa Magufuli’ alikamatwa jana wakati akiandaa banda la kuuzia chakula kwa ajili ya kuwauzia watu watakaohudhuria sherehe za uzinduzi wa mradi wa bomba la mafuta kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga.

Mwanasheria wa mwanamke huyo aliyejitambulisha kwa jina la Shukuru Khalifa alisema mteja wake alikamatwa mchana alipokuwa akiandaa banda hilo.

“Anasema akiwa Chongoleani wakati akiendelea na maandalizi, alipigiwa simu na mkuu wa polisi wa Wilaya ya Tanga akiulizwa yuko wapi, alipojibu alipo baada ya muda mfupi alifuatwa na askari akapelekwa kituo cha Chumbageni” alisema Shukuru. Mwanasheria huyo alisema alipokwenda katika kituo hicho kwa ajili ya kumdhamini alizuiwa kwa madai kwamba mwanamke huyo anadaiwa kufanya biashara eneo ambalo haliruhusiwi.

Shukuru alisema anadhani mteja wake alikamatwa baada ya vyombo vya dola kujenga hisia kwamba anaweza kuandaa bango ili kulionyesha kwa Rais Magufuli kama alivyofanya jijini Dar es salaam.

“Ukweli ni kwamba Swabaha hakuwa na nia ya kumwendea Rais, alikwenda kuweka banda ili afanye biashara kama ilivyo kwa wengine na alifuata taratibu zote akaruhusiwa,” alisema Shukuru.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Benedict Wakulyamba alipotafutwa kuelezea tukio hilo simu yake iliita bila kupokewa.


Chanzo: Mwananchi
 
Bora wamemuwahi maana kesho tusingeskia habar za Ruge na bashite ni yeye ndo angesikika magazetini.

Hachelewi kuharibu hali ya hewa yule
 
Bibie Amejawa na Usanii na huwa haeleweki kabisa, Achunguzwe zaidi
 
Back
Top Bottom