Mjane aliyeangua kilio mbele ya Rais Magufuli adaiwa milioni 400

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,253
DAR ES SALAAM
MJANE aliyelalamika kudhulumiwa mirathi mbele ya Rais John Magufuli, katika sherehe za siku ya Sheria, amefunguliwa kesi na mtoto wa marehemu akidai fidia ya Sh milioni 400 kwa kumtaja kuwa anajihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya.

Kesi hiyo ya madai imefunguliwa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam na mmoja wa watoto wa Marehemu Shosi, Saburia Shosi dhidi ya mjane wa marehemu, Swabaha Shosi.

Katika kesi hiyo namba 38 ya mwaka 2017, Saburia ambaye anawakilishwa na Wakili Abdon Rwegasira, anaiomba mahakama itamke kuwa tuhuma hizo zilizotolewa na mama huyo dhidi yake ni kashfa, pia imwamuru mama huyo amlipe kiasi hicho cha fedha kama fidia ya madhara aliyoyapa kutokana na kwa kashfa hizo, riba pamoja na gharama za kesi.

Kwa mujibu wa hati ya madai ya kesi hiyo, Saburia anadai kuwa yeye ndiye aliyeteuliwa kuwa msimamizi wa mali za marehemu baba yao, Shosi na kwamba mdaiwa alitoa taarifa hizo kwa nia mbaya kwa lengo la kumdhuru kwa kumharibia jina lake, tabia na mahusiano ya kijamii ndani na nje ya nchi pamoja na hali yake kiuchumi.

“Mdaiwa alitoa taarifa hizi kwa hasira na kwa nia mbaya ya kutaka kupata huruma ya rais kwa jambo ambalo liko katika Mahakama za Kisheria na kwamba matokeo ya taarifa hizo zimesababisha watu waniepuke, maumivu makubwa kimwili, kiakili na kisaikolojia na biashara zangu kuvurugika,” inasema hati yake ya madai.

Chanzo: Mtanzania

===========

Mimi hapa naona kama huyu mama ameenda kujipalia mkaa mwenyewe, maana hapo akikutwa na hatia atapataje hiyo pesa? Mambo mengine tuepuke tamaa kwa kisingizio cha simpathy ya jamii.
 
Kama hati (plaint) iko hvo haimanishi mahakama lazma impe hcho kiasi HAPANA yeye kaomba kama madhara ya jumla (general damages) so mahakama inaweza kumpa hata 500,000/= kulingana na madhara aliyoyapata mlalamikaji. Kwa hlo la biashara kuwa ngumu ni madhara yanayodhibitika (specific damages) ambazo atatakiwa kudhibisha kwa nguvu sana (strictly prove thereof) so tuiachie mahakama kuamua.
 
Matatizo ya ulongo na uzushi huishia hapa hapa Dunian na kwa aibu kubwa...vitu kama vile vya uule mama ambae bado mnamuita Mjane sasa sijui mjane wa nani manake hukumu imeshamtoa kwenye Ujane!!! Huisha kwa aibu na fedheha
 
Wamkomeshe kabisa aache kiherehere

Kamchafua huyo bwana na inawezekana hata akisafiri nje anatiliwa shaka,wadau wake wa biashara wanamkwepa na hata msikitini na mtaani haaminiki,angemtandika bilioni mbili kabisa na security for cost kwa kuwa huyo mama ni mkenya anaweza kukimbia
 
Mambo ya madawa haya bhana! Hahaha
Amuu ulize RC kilicho mkuta.

Ila naye alo fungua kesi milion 400 yule sista azitoe wap, awe na common sense bas naye
 
Wamkomeshe kabisa aache kiherehere

Kamchafua huyo bwana na inawezekana hata akisafiri nje anatiliwa shaka,wadau wake wa biashara wanamkwepa na hata msikitini na mtaani haaminiki,angemtandika bilioni mbili kabisa na security for cost kwa kuwa huyo mama ni mkenya anaweza kukimbia
No sio bwana aliemchafua, ni mtoto wa kike huyo saburia sio mwanaume, ni mtoto mkubwa wa huyo Shosi na Ndio msimamizi wa mirathi,
Mama muigizaji yule mpaka alilia machozi ya Steve, huyu angekwenda bongo movie ingemlipa sana
 
DAR ES SALAAM
MJANE aliyelalamika kudhulumiwa mirathi mbele ya Rais John Magufuli, katika sherehe za siku ya Sheria, amefunguliwa kesi na mtoto wa marehemu akidai fidia ya Sh milioni 400 kwa kumtaja kuwa anajihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya.

Kesi hiyo ya madai imefunguliwa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam na mmoja wa watoto wa Marehemu Shosi, Saburia Shosi dhidi ya mjane wa marehemu, Swabaha Shosi.

Katika kesi hiyo namba 38 ya mwaka 2017, Saburia ambaye anawakilishwa na Wakili Abdon Rwegasira, anaiomba mahakama itamke kuwa tuhuma hizo zilizotolewa na mama huyo dhidi yake ni kashfa, pia imwamuru mama huyo amlipe kiasi hicho cha fedha kama fidia ya madhara aliyoyapa kutokana na kwa kashfa hizo, riba pamoja na gharama za kesi.

Kwa mujibu wa hati ya madai ya kesi hiyo, Saburia anadai kuwa yeye ndiye aliyeteuliwa kuwa msimamizi wa mali za marehemu baba yao, Shosi na kwamba mdaiwa alitoa taarifa hizo kwa nia mbaya kwa lengo la kumdhuru kwa kumharibia jina lake, tabia na mahusiano ya kijamii ndani na nje ya nchi pamoja na hali yake kiuchumi.

“Mdaiwa alitoa taarifa hizi kwa hasira na kwa nia mbaya ya kutaka kupata huruma ya rais kwa jambo ambalo liko katika Mahakama za Kisheria na kwamba matokeo ya taarifa hizo zimesababisha watu waniepuke, maumivu makubwa kimwili, kiakili na kisaikolojia na biashara zangu kuvurugika,” inasema hati yake ya madai.

Chanzo: Mtanzania

===========

Mimi hapa naona kama huyu mama ameenda kujipalia mkaa mwenyewe, maana hapo akikutwa na hatia atapataje hiyo pesa? Mambo mengine tuepuke tamaa kwa kisingizio cha simpathy ya jamii.
akikutwa na hatia abanwe kisawasawa ili ajue mahakama sio chuo cha sanaa.Hata kama una haki zako za msingi kumchafua mtu bila ushahidi ni kosa na unaharibu mirija ya kutengeneza pesa ya watu,watu wanachukua muda kujibrand na kuanza kutengeneza pesa sio kwa kujilizaliza tu.ila akithibitisha tuhuma zake kwa shosi,shosi nae abanwe.
 
Back
Top Bottom