Mjane ailalamikia CCM kutomlipa kodi ya pango kwa miaka mitano, ofisi yafungwa deni lafikia milioni 3

Waziri2025

Senior Member
Sep 2, 2019
148
379
Mkazi mmoja wa kata ya Osunyai ,katika jiji la Arusha , Gloria Laizer ambaye ni mama mjane, amelazimika kuangua kilio hadharani kumlalamikia mpangaji wake ambaye ni chama Cha Mapinduzi CCM kata hiyo kwa kushindwa kumlipa deni la pango katika ofisi waliopanga katika kipindi Cha miaka mitano linalofikia kiasi Cha zaidi ya shilingi milioni 3.5.

Mjane huyo amesema pamoja na jitihada zote alizozifanya kudai fedha zake ikiwemo kuifunga ofisi hiyo, lakini bado hakuna jitihada zozote za yeye kulipwa fedha zake.

Akiongea kwa uchungu huku akiangua kilio hadharani alisema anachangamoto kubwa ya kusomesha watoto wake kutokana na ukosefu wa fedha na hivyo amemwomba Mwenyekiti wa CCM Taifa ,Rais John Magufuli kumsaidia kuweza kupata madai yake .

Amesema wamefanya vikao mbalimbali na viongozi wa CCM ili kupata mwafaka wa malipo ya Kodi yake lakini amekuwa akiambulia maneno matamu yenye matumaini na mwisho wake kutolipwa kabisa.

"Hivi Mimi nimemkosema Nini mungu nimefanya makosa kupangisha nyumba yangu kwa ccm Mimi ni mjane sina mapato yoyote zaidi ya kuegemea hii Kodi ya nyumba kwani hawa CCM wanisumbue na kutaka kunidhulumu???"alisema Gloria

Aidha alifafanua kwamba waliingia makubaliano na CCM Agosti Mwaka 2015, kwamba ccm italipa kila chumba sh,60,000 Kila mwezi kwa vyumba viwili walivyokodisha .

" lakini chaajabu hadi Sasa hawakuwahi kunilipa chochote na hivyo najikuta nikishindwa kusomesha Hata watoto wangu"alisema

Akizungumzia madai hayo kwa njia ya simu Mwenyekiti wa CCM katika kata ya Osunyai Abdi Madava amekiri kuwepo kwa Deni hilo la muda mrefu , Ila alidai hana habari Kama ofisi zimefungwa kwa sababu hajaingia ofisini kwa muda mrefu.

Naye Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Arusha Joseph Masawe alisema kuwa deni hilo la pango halijalipwa kwa sababu hajaletewa invoice ya madai na hivyo wasingeweza kufanya malipo bila stakabadhi ya madai.

Ends....
 
Huyu mama ana lake jambo!

Kwa nini aliacha deni hilo kupaa hadi kufikia hapo bila kuhoji?

Je kabla hajatafuta msaada toka ngazi ya taifa.

Amejaribu kufika ngazi ya mkoa au ndio hivyo kuanza kutumika ili kuchafua taswira ya chama kitaifa bila kuanzia ngazi za chini kwa ubadhilifu wa watu wachache ngazi ya kata.
 
Lipeni deni!! Hizi dhuluma zitawafikisha wapi? Sasa mnampangia jinsi ya kudai?
 
Mkazi mmoja wa kata ya Osunyai ,katika jiji la Arusha , Gloria Laizer ambaye ni mama mjane, amelazimika kuangua kilio hadharani kumlalamikia mpangaji wake ambaye ni chama Cha Mapinduzi CCM kata hiyo kwa kushindwa kumlipa deni la pango katika ofisi waliopanga katika kipindi Cha miaka mitano linalofikia kiasi Cha zaidi ya shilingi milioni 3.5...
Hhahhaaaaa huyo mama ana lipa kodi ya serikali kutokana na haya mapato ya kodi? Anayo TIN? Kiwanja chenye hiyo nyumba amekilipia kodi? Je property tax amelipa? Na je anayo EFD receipt? Mkataba wake na ccm umesajiliwa kwa mwanasheria wa serikali?

Kama hana hayo yote nampa Pole sana Mama Laizer na ni bora umtafute kaka yako Sinunu uone kama anaweza kukugawia vijisenti kidogo maisha yasonge. Vinginevyo kuendelea kusumbuana na mtu anayesema hujapeka invoice mama unaitafuta jela na TRA waje wauze hicho kijumba chako
 
Huyu mama ni wakala wa mabeberu anatumika kuichafua nchi,kuhusu hela ya kusomesha watoto huo ni uongo sababu elimu sasa hivi ni bure na hata takwimu official za serikali zinaonyesha hakuna mlipuko wa bei za bidhaa zipo stable kabisa na uchumi unakua asilimia 8
 
Lipeni deni!! Hizi dhuluma zitawafikisha wapi? Sasa mnampangia jinsi ya kudai?
Chadema makao makuu mjane wa BOB MAKANI pia anawaza kodi ya pango miaka hamlipi

Hamlipi makao makuu ya Chadema ni nyumba ya mjane ya aliyekuwa mwenyekiti wa Chadema Taifa marehemu Bob Majaji lipeni
 
Mkazi mmoja wa kata ya Osunyai ,katika jiji la Arusha , Gloria Laizer ambaye ni mama mjane, amelazimika kuangua kilio hadharani kumlalamikia mpangaji wake ambaye ni chama Cha Mapinduzi CCM kata hiyo kwa kushindwa kumlipa deni la pango katika ofisi waliopanga katika kipindi Cha miaka mitano linalofikia kiasi Cha zaidi ya shilingi milioni 3.5...
CCM uzeni Viete moja mumlipe Mama Mjane Pamoja na Rib
 
Invoice ya madai, kwani waliambiwa ni nyumba ya kampuni.

Mlipeni mjane mwenzetu.

Huko mombo mbona mnaonesha huruma au mnajifanya ?
 
Huyu mama ana lake jambo!
Kwa nini aliacha deni hilo kupaa hadi kufikia hapo bila kuhoji?

Je kabla hajatafuta msaada toka ngazi ya taifa.
Amejaribu kufika ngazi ya mkoa au ndio hivyo kuanza kutumika ili kuchafua taswira ya chama kitaifa bila kuanzia ngazi za chini kwa ubadhilifu wa watu wachache ngazi ya kata.
Unazan ni kisafi
 
Back
Top Bottom