Mjane ailalamikia CCM kutomlipa kodi ya pango kwa miaka mitano, ofisi yafungwa deni lafikia milioni 3

Naye Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Arusha Joseph Masawe alisema kuwa deni hilo la pango halijalipwa kwa sababu hajaletewa invoice ya madai na hivyo wasingeweza kufanya malipo bila stakabadhi ya madai.

Invoice gani wanataka, kwani walivyopanga hapo hawakujua kama huyo mama hawezi toa invoice, wamepanga ili wamdhulumu, wajinga kabisa... basi watoke na siyo kukaa bure...

Cc: mahondaw
 
Chadema makao makuu mjane wa BOB MAKANI pia anawaza kodi ya pango miaka hamlipi

Hamlipi makao makuu ya Chadema ni nyumba ya mjane ya aliyekuwa mwenyekiti wa Chadema Taifa marehemu Bob Majaji lipeni
Bob alikuwa Mchagga pia
 
Naye Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Arusha Joseph Masawe alisema kuwa deni hilo la pango halijalipwa kwa sababu hajaletewa invoice ya madai na hivyo wasingeweza kufanya malipo bila stakabadhi ya madai.

Invoice gani wanataka, kwani walivyopanga hapo hawakujua kama huyo mama hawezi toa invoice, wamepanga ili wamdhulumu, wajinga kabisa... basi watoke na siyo kukaa bure...

Cc: mahondaw
Mwenyekiti Massawe na CCM wapi na wapi....kauli yako kama ni kweli inaweza tia chama chetu doa.Nadhani upande ule nwingine ni mzuri kwako
 
Hhahhaaaaa huyo mama ana lipa kodi ya serikali kutokana na haya mapato ya kodi? Anayo TIN? Kiwanja chenye hiyo nyumba amekilipia kodi? Je property tax amelipa? Na je anayo EFD receipt? Mkataba wake na ccm umesajiliwa kwa mwanasheria wa serikali?

Kama hana hayo yote nampa Pole sana Mama Laizer na ni bora umtafute kaka yako Sinunu uone kama anaweza kukugawia vijisenti kidogo maisha yasonge. Vinginevyo kuendelea kusumbuana na mtu anayesema hujapeka invoice mama unaitafuta jela na TRA waje wauze hicho kijumba chako
Wewe mpangaji una lako jambo. Lipa deni.
 
Huyu mama ana lake jambo!

Kwa nini aliacha deni hilo kupaa hadi kufikia hapo bila kuhoji?

Je kabla hajatafuta msaada toka ngazi ya taifa.

Amejaribu kufika ngazi ya mkoa au ndio hivyo kuanza kutumika ili kuchafua taswira ya chama kitaifa bila kuanzia ngazi za chini kwa ubadhilifu wa watu wachache ngazi ya kata.

Dawa ya deni ni kulipa tu.
 
Kama ni mwanachama wa ccm awe mzalendo
Aipotezee tu hiyo kodi

Ova
 
Mkazi mmoja wa kata ya Osunyai ,katika jiji la Arusha , Gloria Laizer ambaye ni mama mjane, amelazimika kuangua kilio hadharani kumlalamikia mpangaji wake ambaye ni chama Cha Mapinduzi CCM kata hiyo kwa kushindwa kumlipa deni la pango katika ofisi waliopanga katika kipindi Cha miaka mitano linalofikia kiasi Cha zaidi ya shilingi milioni 3.5.

Mjane huyo amesema pamoja na jitihada zote alizozifanya kudai fedha zake ikiwemo kuifunga ofisi hiyo, lakini bado hakuna jitihada zozote za yeye kulipwa fedha zake.

Akiongea kwa uchungu huku akiangua kilio hadharani alisema anachangamoto kubwa ya kusomesha watoto wake kutokana na ukosefu wa fedha na hivyo amemwomba Mwenyekiti wa CCM Taifa ,Rais John Magufuli kumsaidia kuweza kupata madai yake .

Amesema wamefanya vikao mbalimbali na viongozi wa CCM ili kupata mwafaka wa malipo ya Kodi yake lakini amekuwa akiambulia maneno matamu yenye matumaini na mwisho wake kutolipwa kabisa.

"Hivi Mimi nimemkosema Nini mungu nimefanya makosa kupangisha nyumba yangu kwa ccm Mimi ni mjane sina mapato yoyote zaidi ya kuegemea hii Kodi ya nyumba kwani hawa CCM wanisumbue na kutaka kunidhulumu???"alisema Gloria

Aidha alifafanua kwamba waliingia makubaliano na CCM Agosti Mwaka 2015, kwamba ccm italipa kila chumba sh,60,000 Kila mwezi kwa vyumba viwili walivyokodisha .

" lakini chaajabu hadi Sasa hawakuwahi kunilipa chochote na hivyo najikuta nikishindwa kusomesha Hata watoto wangu"alisema

Akizungumzia madai hayo kwa njia ya simu Mwenyekiti wa CCM katika kata ya Osunyai Abdi Madava amekiri kuwepo kwa Deni hilo la muda mrefu , Ila alidai hana habari Kama ofisi zimefungwa kwa sababu hajaingia ofisini kwa muda mrefu.

Naye Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Arusha Joseph Masawe alisema kuwa deni hilo la pango halijalipwa kwa sababu hajaletewa invoice ya madai na hivyo wasingeweza kufanya malipo bila stakabadhi ya madai.

Ends....
Hawa nzi wa kijani kodi huwa hawalipi mana wamezoea dhuluma....majengo yao wameiba ya serikali na kujimilikisha
 
Lipeni deni!! Hizi dhuluma zitawafikisha wapi? Sasa mnampangia jinsi ya kudai?
Hahaaaa!!kumbe pole pole anakomalia ya wengine kwwnye kile kipindi chake chaneli ten(papo kwa hapo), tena anakuwa mkali kweli eti awamu ya tano haitakunali kuona mnyonge anadhurumika kumbe na wao ni wale wale!!
 
...
Naye Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Arusha Joseph Masawe alisema kuwa deni hilo la pango halijalipwa kwa sababu hajaletewa invoice ya madai na hivyo wasingeweza kufanya malipo bila stakabadhi ya madai.

Ends....
... naona mashetani wa kijani wameamua kumtega huyo mama mjane; hiyo statement ina maana kubwa sana na uelekeo ni kumdhulumu. Hivi kweli nyumba zetu za uswahilini zinatoa "invoice"? Hawa majama wana dhambi sana. Naye huyo mama akome, unawezaje kuwapangisha hawa jamaa? Kama ni mwenzao apotezee tu aache kulalamika.
 
Huyu mama ni wakala wa mabeberu anatumika kuichafua nchi,kuhusu hela ya kusomesha watoto huo ni uongo sababu elimu sasa hivi ni bure na hata takwimu official za serikali zinaonyesha hakuna mlipuko wa bei za bidhaa zipo stable kabisa na uchumi unakua asilimia 8
Upo SAHIHI kabisa tena mia kwa mia na nimekuelewa.
Endelea kuandika DHULMA HAIDUMU NA IKIDUMU HUANGAMIZA.
Pia tuandikie kwamba Kila nafsi itaonja UMAUTI na tutahukumiwa kwa matendo yetu.
Mwisho tukumbushe Uchaguzi umekwisha sasa tuchape kazi.
 
... naona mashetani wa kijani wameamua kumtega huyo mama mjane; hiyo statement ina maana kubwa sana na uelekeo ni kumdhulumu. Hivi kweli nyumba zetu za uswahilini zinatoa "invoice"? Hawa majama wana dhambi sana. Naye huyo mama akome, unawezaje kuwapangisha hawa jamaa? Kama ni mwenzao apotezee tu aache kulalamika.
Kwa mfano ikatokea CHADEMA ikamlipa huyo Mama kwa kuisaidia CCM itakuwa ni kitu mbaya..??
Watu waongo..eti CCM inanunuwa wabunge kwa ma millioni lakini inashindwa kumlipa mjane M3 tuuu.
Wanasema CCM ina ma V 8 haishindwi kulipa hiyo m 3.
Tumuombe Mwenyezimungu atubainishie HAKI ili tuweze kuifuata na atubainishie BATWIL ili tuweze kuiacha.
 
Back
Top Bottom