Mjamzito auawa na mume wake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mjamzito auawa na mume wake

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by MziziMkavu, Oct 22, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Oct 22, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  22nd October 2009  Mama mmoja mjamzito aliyetambuka kwa jina la Shida Madoki ameuawa na mumewe Gamaliel Mtonyele, 27 kutokana na kile kilichobainika mahakamani kuwa ni wivu wa kimapenzi.
  Tukio hilo ambalo mahakama imebaini kuwa ni la mauaji ya kutokusudia, limetokea katika Kijiji cha Kalangali, Wilaya ya Manyoni mkoani Singida.
  Imeelezwa juzi katika Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma kabla ya hukumu ya tukio hilo ambalo limetupa jela miaka sita muuaji Mtonyele kuwa, lenyewe lilitokea Aprili 17, mwaka 2006.
  Ikaelezwa zaidi kuwa siku hiyo, Mtonyele alimuua mkewe wakati wakisaka wote kuni katika pori moja liitwalo Masimba, hukohuko katika Kijiji chao cha Kalangali, wilaya ya Manyoni.
  Ikaelezwa kuwa wakiwa huko, ndipo mshtakiwa alipomuua mkewe kutokana wivu, hasa pale alipouliza juu ya mtu aliyempa mimba mkewe huyo (marehemu Shida).
  Imeelezwa na Wakili wa Serikali Magambo Mayeye, mbele ya Jaji wa Mahakama Kuu, Mwanaisha Kwariko kuwa katika mauaji hayo, mshtakiwa alimkata kisogoni mkewe kwa kutumia kitu chenye ncha kali na hivyo kumsababishia umauti wa papohapo.
  Mahakama ikaelezwa kuwa siku ya tukio , mshtakiwa na marehemu walienda porini kwa ajili ya kukata kuni, lakini walipofika huko alimuuliza mkewe kuhusu mtu aliyempa ujauzito alionao na mkewe kumjibu akisema, 'usinifuatefuate', jambo lililomtia ghadhabu mshtakiwa na kumfanya atende kosa hilo.
  Mshtakiwa alikiri kosa hilo la kuua bila kukusudia na ndipo mahakama ikamuhukumu kifungo hicho cha miaka sita.
  Katika shauri jingine, mahakama hiyo imemuhukumu mkazi wa Kijiji cha Nkalakala wilayani Iramba Alexander Godfrey ,21, kifungo cha miaka mitatu jela, baada ya kukiri kosa la kumuua Petro John bila ya kukusudia wakati wakigombea sehemu ya kulala.
  Mbele ya mahakama hiyo, ilielezwa na Wakili wa Serikali Magambo Mayeye kuwa mauaji hayo yalifanyika Septemba 20 mwaka 2006, saa 2:00 usiku, huko katika Kijiji cha Nkalakala, tarafa ya Nduguti wilayani Iramba.  CHANZO: ALASIRI
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Oct 22, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Wanasheria nisaidieni, hizi hukumu zinakuwakuwaje, mmoja kaua mkewe, miaka sita jela, mwingine kamuua Petro, akafungwa miaka 3 jela...imekaaje hii?
  SI WOTE WAMEUA....Ebo?
   
Loading...