Trainee
JF-Expert Member
- Sep 22, 2018
- 2,208
- 2,808
Habari ndugu zangu...
Soma hii stori ya kumhusu mke wangu halafu naomba ushauri.
Tarehe 28 April 2020 nilimuoa (tukaingia kwenye fungate). Tarehe 4-5 May akasema tumbo linauma nikamnunulia dawa inaitwa amoxicillin (nilishauriwa kutokana na maelezo ya jumla aliyotoa)
Katikati ya May ikazuka hali mpya sasa ya kuhisi anataka kukojoa akienda mkojo hakuna au unatoka kidogo tu na anashinwa kuondoka chooni kwakuwa anakuwa bado anahisi anataka kukojoa; hali hii inamtokea pengine siku nzima akienda chooni anakaa karibu dakika 30 na akitoka hachukui dakika 15 amerudi tena chooni.
Akawa anapata nafuu (anapona) mara vinatimka tena na kichwa basi ikawa ni mwendo wa paracetamol na amoxicillin (hakupimwa). Hali ikawa ndo hiyo lakini kilichonipa wazimu ni hii ya mkojo kwani alisema anahisi kama anatekenywa kuna vitu vitu vinatembea kwenye njia ya mkojo
Tarehe ishirini na kitu May tukapewa ciprofloxacin (bila kupimwa) wakisema itakuwa ni UTI dozi ikaisha siku saba bila yeye kuonesha dalili ya kupona . Mwezi June mwanzoni ndo akapimwa akaonekana ni mjamzito ila ana Malaria basi akapewa quinine vidonge na kuanza clinic mojakwamoja. Akamaliza dozi hali bado kurudi zahanati wakasema atumie tu amoxicillin itatulia nikanunua dawa lakini sikumpa anywe kesho asubuhi nikafunga safari mpaka hospitali.
Ilikuwa tar24 June Kufika kule akamulikwa x-ray na kupimwa tena wakasema ni malaria ila mimba haina shida ina wiki 7 na siku 1. Basi wakaandika amoxillin na quinine ila safari hii sindano sasa siyo vidonge tena. Basi kitu nilichoshukuru ni kwamba walimzungusha zungusha pale nenda huku rudi kule hakuchomwa basi mke wangu akanipigia niende pale nikamsaidie achomwe sindano (maana nilitoka kidogo pale hospitali- utajua mbeleni kwanini nilishukuru walivyomzungusha)
Basi me nilipofika pale sikuwakuta wahusika wote naambiwa wametoka kidogo eti kwa hasira nikamwambia mke twende utendachomewa kule zahanati kijijini kwetu... kufika nikamwambia anywe zilezile aliandikiwa zahanati halafu sindano twende akachomwe na nesi pale pale
Bwana wewe kufika nesi anaangalia chupa zile zime expire siku nyingi tukazitupa anaendelea na amoxicillin lakini hatahivyo tatizo lipo palepale na juzi amejisaidia minyoo miwili mirefu kwenda zahanati wakasema mpaka afike miezi mitatu mimba ndo atakula dawa za minyoo
Msaada tafadhali!
Tanbihi;
Sijabobea kwenye uandishi kwahiyo inawezekana sehemu nyiingine ikawa nimechanganya madesa!... kikubwa tuvumiliane
Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app