Mjamzito aanza kujifungua ndani ya tax | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mjamzito aanza kujifungua ndani ya tax

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Apr 20, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Apr 20, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  KATIKA hali ya majibizano kati ya ndugu wa mume na mke ni hospitali gani apelekwe mwanamke aliyekuwa mjamzito na jibu kutopatikana mapema ilifanya mwanamke huyo aanze hatua za awali za kujifungua ndani ya tax wakati anakimbizwa hospitalini Mwanamke huyo [31][jina kapuni] mkazi wa Kinondoni Mkwajuni, alishikwa na dhahama hiyo jana, majira ya saa 6, baada ya ndugu zake na ndugu za mume wake kutoelewana ni hospitali ipi apelekwe aende akajifungulie.

  Ilidaiwa na shuhuda wetu kuwa, mwanamke huyo alianzwa na uchungu mwepesi majira ya usiku wa saa kumi na kumtaarifu dada yake mkubwa aishie Mbagala aje ili aje amsindikize hospitali aende kujifungua.

  Taarifa hiyo ilipomfikia dada yake huyo alifika nyumbani kwa mdogo wake huyo asubihi ya saa kumi na mbili na nusu akiwa na mdogo wao wa kike.

  Wakati huohuo mume wa mke aliyetambulika kwa jina mja la Othumani alimtaarifu dada yake kuwa afike nyumbani kwake ili amsaidie wifi yake kumpeleka hospitali.

  Ilidaiwa utata ulianza baada ya dada wa mwanamke mjamzito kutaka mdogo wake apelekwe akajifungulie hospitali binafsi, wakati dada wa mume kupinga na kutaka wifi yake mpendwa apelekwe hospitali ya serikali yaani Mwananyamala kwa kuwa ilikuwa karibu na hapo kwa kudai hospitali binafsi hawana taaluma nzuri kwenye masuala ya uzazi na kudai anaweza akafanyiwa operesheni pasipo na sababu za msingi.

  Dada wa mgonjwa aliposikia imetajwa hospitali ya Mwananyama alianza kupandwa na mori na kuanza kujibizana na dada wa mume na kuongea kwa lugha ya ugomvi na kudai mdogo wake hapelekwi kujifungulia Mwananyama na kama atapelekwa hatahusika na atataizo lolote na mgonjwa huyo na atamuachia wifi yake huyo.

  Wakati hapo masaa yanaenda na hali ya kutoelewana inazidi kuendelea. Dada wa mume aliposikia dada yake amegoma asipelekwe Mwananyamala aliamua basi wifi yake apelekwe Amana ili akajifungulie huko ili hali asipelekwe binafsi.

  Kwa wakati huo mume wa mgonjwa alikuwa hajui aelekea upande upi wa maamuzi na kubaki na utata na kutotambua atoe maamuzi yepi.

  Wakati muafaka bado haujapatikana mwanamke huyo uchungu ulimzidia katika majira ya saa sita mchana na kuamuru apelekwe popote ili hali asilimishe kiumbe na kumtaka dada yake aachie upande wa mume wea maamuzi.

  “ Kauli hiyo ya mdogo wake hakupendezewa nayo na kumwambia wewe huwezi kwenda Mwananyamala ili hali kila siku kuna matatizo yanajitokeza huko huyasikii mdogo wangu mimi sikubali” huku dada huyo akilia

  Mume wa dada huyo alipoona hakuna maelewano katika hilo na kuona mke wake anazidi kujikanyaga kwa uchungu ndani alichukua umanuzi wa kwenda kuchukua tax na kurudi hapo ili ampakize mke wake ampeleke popote ili akajifungue.

  Wakati mama huyo anapakizwa ndani ya gari hiyo bila kuamini macho yao mama huyo alionekana kuanza hatua za awali za kujifungua na kupiga makelele huku na huko na mume kumuamuru dereva akimbize gari MWnanyamala na kuwaacha dada yake na shemeji yake hapohapo.

  Ilidaiwa kuwa mwanamke huyo alikuwa na matatizo ya kushika ujauzito na hakuwahi kubahatika kupata mtoto katika ndoa yake iliyodumu kwa muda wa miaka mitano ndio mana mzozo huo ulizuka kwa kuwa kila mtu alikuwa ana upendo wa kutosha na mtoto atakayezaliwa.

  Ilidaiwa kuwa mwanamke huyo aliweza kumalizia kujifungua na kupata mtoto wa kiume sekunde kadhaa mara tu alipofikishwa wodini katika hospitali ya Mwananyamala.
  http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsId=4373670&&Cat=1
   
Loading...