Mjadala wazuka kuhusu afya ya akili ya Rais Donald Trump

Wabongo wengi wanamshabikia Trump ati kwa sababu anapinga ushoga. Kama ndivyo basi, someni habari hii hapa:
https://www.nytimes.com/2017/01/30/us/politics/obama-trump-protections-lgbt-workers.html?_r=0

Msifanye ushabiki bila ya kujihabarisha kiasi cha kutosha na kuwa na critical thinking.
Hizo fake news channels na magazine huwa sifungui kusoma wala kuangalia! Mi kila siku ya napata info from trump himself anachofanya and everything he talking so hayo ya kusoma kasome wewe uendelee kuwa brainwashed
 
Wakimaliza kumpima afya ya akili ya Trump ningeshukuru kama wangekuja East Africa nina wasiwasi wenye asilimia kubwa kuna Rais mmoja kwenye hizi nchi afya ya akili yake inatia mashaka

Ushauri tuwapime afya ya akili wagombea wa uraisi before
Hahahahaa aiseee
 
_94673452_32aae7f5-e971-4ddb-b806-99d05d5cc3c2.jpg

Wataalamu wa afya ya kiakili wameandika barua wakisema Trump hafai kuwa rais.

Ni suala ambalo hungetarajia watu walizungumzie hasa kuhusu mtu ambaye amekuwa akisimamia biashara ya thamani ya mabilioni ya dola na alishinda mpinzani wake Hillary Clinton katika uchaguzi mkuu uliokuwa na ushindani mkubwa mwaka jana.

Lakini sasa wataalamu wa afya ya kiakili wanajadili hali ya rais wa Marekani Donald Trump.

Mjadala huo umekuwa wazi sasa baada ya wataalamu kadha kuandika barua ya wazi wakisema Trump ana matatizo makubwa ya kiakili na hafai kuwa rais.

Wito huo unaonekana kwenda kinyume na msimamo wa muda mrefu wa wataalamu wa kutojadili matokeo ya uchunguzi kuhusu afya hadharani.

Barua hiyo imeshutumiwa na baadhi ya wataalamu.
Mmoja amesema ni ya aibu na sawa na matusi kwa wagonjwa wa matatizo ya kiakili.
Ingekuwa Africa kuna uhuru kama huko hata huku tunao tatizo woga
 
Vilema hatuchekani. Huku kwangu TZ nako majanga tena afadhali ya USA kidogo kuna vyombo huru vinavyoweza kurekebisha mambo. Hapa TZ yule mkubwa sana akishasema ndo imetoka hivyo!
 
Inawezaje kuingia akialini! Mgonjwa wa akili apambane na wenye afya ya akili wengi ndani ya republican na awashinde wote! Halafu huyu mgonjwa wa akili aliyewashinda wapinzani wake huko republican anapambana na mgombea wa Democratic mwenye afya ya akili akisaidiwa na marais wastaafu wanne (Obama, Clinton, na bush Mdogo na bush mkubwa) lakini hawa pia wakashindwa na mgonjwa wa akili! Wapiga kura wote wana akili timamu lakini kwa utaratibu wa marekani wakampa kura za kutosha mgo njwa wa akili awe rais! Pamoja na kulundikiwa kashfa bado wapiga kura walimwamini mgonjwa wa akili kuliko walio wazima!
Ikitokea kuwa ni kweli Trump ni mgonjwa wa akili, basi wapinzani wake wote ni wagonjwa wa akili zaidi kuliko Trump na wapiga kura wakaona wamchague ambaye ugonjwa wake wa akili una nafuu zaidi! Kwa sababu huwezi ukadai wewe ni mzima kama watu wazima wakamwamini chizi awaongoze kuliko wewe!
Kuonyesha kuwa Trump yuko vizuru anakumbuka vizuri ahadi alizoahidi kwenye kampeni na akaanza kuzitekeleza kuanzia siku ya kwanza! Hii ni rekodi ya dunia! Yale maamuzi na maagizo anayotoa yanayowafanya wengine wamwone chizi ndiyo aliyokuwa ameyaahidi kwenye kampeni na ndiyo yaliyovutia watu wampe kura!
very true
 
_94673452_32aae7f5-e971-4ddb-b806-99d05d5cc3c2.jpg

Wataalamu wa afya ya kiakili wameandika barua wakisema Trump hafai kuwa rais.

Ni suala ambalo hungetarajia watu walizungumzie hasa kuhusu mtu ambaye amekuwa akisimamia biashara ya thamani ya mabilioni ya dola na alishinda mpinzani wake Hillary Clinton katika uchaguzi mkuu uliokuwa na ushindani mkubwa mwaka jana.

Lakini sasa wataalamu wa afya ya kiakili wanajadili hali ya rais wa Marekani Donald Trump.

Mjadala huo umekuwa wazi sasa baada ya wataalamu kadha kuandika barua ya wazi wakisema Trump ana matatizo makubwa ya kiakili na hafai kuwa rais.

Wito huo unaonekana kwenda kinyume na msimamo wa muda mrefu wa wataalamu wa kutojadili matokeo ya uchunguzi kuhusu afya hadharani.

Barua hiyo imeshutumiwa na baadhi ya wataalamu.
Mmoja amesema ni ya aibu na sawa na matusi kwa wagonjwa wa matatizo ya kiakili.
Ningefurahi sana hii ingekuja na hapa tanzania
 
Back
Top Bottom