MJADALA WA WIKIENDI: Kufurika katikati ya Jiji la Dar ushahidi wa kikomo cha uwezo wetu kufikiri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

MJADALA WA WIKIENDI: Kufurika katikati ya Jiji la Dar ushahidi wa kikomo cha uwezo wetu kufikiri

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Apr 13, 2012.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Apr 13, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,395
  Trophy Points: 280
  Miaka nenda rudi tumesikia "mafuriko" na kila mafuriko yanapotekea utasikia "mabondeni". Kila mafuriko yanapotokea zinapigwa picha ya jinsi watu wanavyoweza kusurvive mafuriko hayo. Tumeandika hapa mara nyingi na picha nyingi za mafuriko katika Jiji la

  Dar zimewekwa. Tumeona watu wakiendesha magari na pikipiki kwenye mitaa iliyojaa maji na pia tumeona watu wengine wakibebwa mgongoni (kwa ada fulani) kuhamishwa toka upande mmoja kwenda mwingine.

  Kwenye baadhi ya maofisi kuna matairi yamepangwa au matofali ambayo yamekaa hapo kwa ajili ya wakati wa mafuriko ambapo watu huwezi kutumia na sehemu nyingine kuna watu huweka matairi au matofali na kuwatoza watu fedha kwa kupita wakati wa mafuriko na kweli kabisa wapo watu wanapita na kulipa bila kufikiria.

  Jiji la Dar ni miongoni mwa miji midogo kabisa kijiografia labda kuliko mji mwingine wowote Tanzania. Lakini tunaweza kusema pasipo shaka kuwa kushindikana kwa kutengenezwa kwa mfumo mzuri wa maji ya mafuriko (storm water) na maji machafu (sewage system) ni dalili tu kuwa tuna wasomi wengi na wanasiasa wengi ambao wanaishi Dar lakini wote hawa wameshindwa kabisa kutafuta suluhisho la tatizo la mafuriko.

  Sasa hivi magenius wetu wameamua kuja na mradi mkubwa wa mabasi yaendayo kasi ambayo nayo kwa hakika yatapita kwenye njia hizi za mafuriko. Licha ya mradi huo mradi mwingine wa mabilioni umebuniwa wa kujenga mabarabara ya juu kwa juu ili na sisi tuweze kupiga picha nyingi na kuonesha kuwa na sisi "tunazo". Ukijumlisha na mradi wa daraja kubwa la Kigamboni ni wazi kabisa kuwa Watanzania wanaonekana wanaweza! Lakini unajiuliza kwanini wameshindwa hili la kuhakikisha jiji halifuriki kila mvua ikinyesha?
   
 2. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #2
  Apr 13, 2012
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Mkuu Mwanakijiji

  CCM inakufa, Serikali iko busy na kuokoa chama kinachoelekea kaburini, ndo mana ikitokea misiba kongamano etc ccm inajitahidi kujichomoka ili watu waone bado chama kinaishi haya mambo ya kutoa huduma kwa wananchi husitegemee mpaka nchi itakapozaliwa upya


  Vijana wote pamoja na wazee wanakichukia chama cha mapinduzi
  Narudia kusema huduma nyingi za jamii zinazomgusa mwananchi moja kwa moja zitazolota mpaka
  nchi itakapozaliwa upya
   
 3. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #3
  Apr 13, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  Hii ni nchi ya "MIRADI" hatupigi hesabu ya faida uigawe kwa muda itakaodumu, unabuniwa mradi, inatengenezewa budget, hakuna anayeichallage hiyo budget, mkija shtuka wameshautumia huo mradi kama container kupitishia mafungu yao ya kuwagharimia kina lulu.
   
 4. Negotiator

  Negotiator JF-Expert Member

  #4
  Apr 13, 2012
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 303
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hapana sisi(watanzania) hatujafikia ukomo wa kufikiri, ni hao tuliowapa mamlaka na madaraka ya kufikiri kupanga na kuamua kwa niaba yetu. kwa kua wamethibitisha hilo kwa hali ya mambo ilivyo, hima sasa na tutwae madaraka na mamlaka tuliyowapa na kuwapatia tunaoamini wanaweza kurekebisha mambo. Tunahitaji uongozi wenye muono wa mbeleni na wenye kujua kupanga vipaumbele. huu wa sasa ni utawala unaoendeshwa kwa matukio. HAUFAI TENA KUTUONGOZA
   
 5. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #5
  Apr 13, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,481
  Likes Received: 5,862
  Trophy Points: 280
  Nadhani watawala wetu wana vipaji vikubwa sana vya usahaulifu. Mafuriko mabaya yalitokea Desemba na leo hii Aprili washasahau. Hakuna hatua zozote zinazochukuliwa kuzuia balaa lisitokee tena. Yaleyale ya TUMWACHIE MUNGU!!!

  Kingine ni mazoea ya kuishi na kufanya kila kitu katika mazingira ya dharura badala ya kupanga na kuamua.
   
 6. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #6
  Apr 13, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mimi hata sielewi hawa watu wa mipango miji wapo kwa ajili gani! Wanalipwa mishahara minono lakini tija yao haionekani kabisa. Building permit zinatolewa hovvyo hovyo bila hata kufika site! Business License zinatolewa, na wao wanaidhinisha bila hata kufika eneo la biashara (tena sasa hivi hata hawaidhinishi tena na bado leseni zinatolewa) na mbaya zaidi wameshindwa hata kushirikiana na Mamlaka ya Maji ili kutengezena mifumo mfumo mzuri wa maji taka na maji safi.

  MM uliposema "...ni kikomo cha uwezo wetu wa kufikiri..." nilitaka nisikubaliane na wewe kwani zigo hili wanastahili kubeba walio frontline, but nilipojiuliza hao waliopo frontline wamefikaje huko, nikabaki ninacheka! Cha kushangaza sasa, ni kwamba jiji hili ndilo linaongoza kwa kukumbatia watu wale wale walioshindwa kwa miaka hamsini?????

  Kweli kufurika katikati ya Jiji la Dar ni ushahidi wa kikomo cha uwezo wetu kufikiri
   
 7. Chimama

  Chimama Member

  #7
  Apr 13, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  MMM...Post yako inanifanya nikumbuke msemo mmoja usemao FAMILIARITY BREEDS CONTENT. Unaona tatizo ambalo linawezekana kabisa kutatuliwa lakini kwa vile sio la kila siku basi unaignore na kujifunza kuishi nalo. Huwa ninakerwa sana nikiona jinsi jiji hasa posta palivyo karibu na bahari halafu eti maji yanafurika..ridiculous. Naamini tuna wahandisi wenye uwezo wa kuchora njia maji taka na mafuriko hadi baharini kama hatuwezi ku-recycle au kuvuna maji. Mvua ya Jumanne, watu wazima tumezamisha viatu kwenye maji halafu husikii likizingumziwa kabisa...Pale ferry pembeni ya stand ya DRT(Dar Rapid Transport) maji huwa yanafurika usipime..sasa sijui hata hilo halionekani hali bahari is less that 100metres kutoka hapo..sielewi.
  Priorities mixed up!!!!
   
 8. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #8
  Apr 13, 2012
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,004
  Likes Received: 590
  Trophy Points: 280
  mradi wa mabasi yaendayo kasi, yangu mie macho tu.
   
 9. Noti mpya tz

  Noti mpya tz JF-Expert Member

  #9
  Apr 13, 2012
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 936
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hatuna vipa umbele na tuna upungufu mkubwa wa fikra za kimaendeleo badala ake tumejaa sifa kuwa nasi tuna akili.
   
 10. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #10
  Apr 13, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 159
  Trophy Points: 160
  Pale Tegeta maji hutuama juu ya daraja na chini kuna mto.....badala ya kuchukia nabaki kucheka
   
 11. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #11
  Apr 13, 2012
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Si kwamba uwezo wetu wa kufikiri umeishia hapo, nadhani wale walio katika nafasi ya kutatua matatizo ndio hawana fikra mpya za namna ya kupambana na matatizo. Ni wakati muafaka wa kubadili mfumo wetu wa uongozi ili kuleta fikra mpya.
   
 12. B

  BobMic Member

  #12
  Apr 13, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Manispaa hizi 3,kinondoni,ilala na temmeke wanakusanya mapato mengi sana,lakini ufisadi ndo unakwamisha mambo,mbona kuna vichwa kibao vinaweza design system nzuri ya maji safi na maji taka???? mimi sitaki kulaumu lakini wabadilike ni muda sasa wa kutumia wataalam wetu waliopo,...maana system iliyopo ni ya kipindi cha mkoloni haiendani na ukuaji wa watu na jiji kwa ujumla..... vijana wenye ujuzi na hzo mambo mpoo///
   
 13. taffu69

  taffu69 JF-Expert Member

  #13
  Apr 13, 2012
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Miradi mingi kwa Tanzania inaonekana mizuri kwenye makaratasi lakini linapokuja suala la utekelezaji huwa ni michache sana inatekelezwa kama ilivyopangwa. Binafsi naona kuwa miradi mingi inaandaliwa kwa lengo la aidha kuombea fedha kutoka kwa wafadhili au kama nyenzo ya kuchota fedha kutoka Serikalini kwa manufaa ya wabinafsi wachache ama mafisadi wachache.

  Hili la Dar Es Salaam na mafuriko nalo linanitatiza sana kwani mara nyingi huwa najiuliza kama ujenzi holela ni kwa wale wanaojenga mabondeni na kwenye maeneo yasiyopimwa pekee ama ni pamoja na wale wanaojenga maeneo yaliyopimwa bila kuangalia uwepo wa miundo mbinu muhimu kama sewage systems pamoja na namna ya kukabiliana na majanga kama moto n.k pale yanapotokea. Dar Es Salaam inasifika kwa sasa kwa msururu wa maghorofa yanayoota kila siku kama uyoga lakini hakuna jitihada zozote za kuboresha miundombinu kama ya maji, vikosi vya kukabiliana na maafa kama moto, mafuriko na mengineyo.

  Kwa Dar Es Salaam pale itakapotokea (naomba Mungu aepushie mbali) jengo kama Benjamini Mkapa Tower likashika moto kwenye ghorofa kama ya 15 hivi naamini maafa yakayotokea ni zaidi ya yale ya M.V Bukoba ama Spice Islander lakini viongozi wetu hawalioni hilo na sidhani kama liko akilini mwao
   
 14. Viper

  Viper JF-Expert Member

  #14
  Apr 13, 2012
  Joined: Dec 21, 2007
  Messages: 3,665
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  January Makamba alipokuwa katika kipindi cha mkasi aliulizwa na salama jabir .. kwanini anaishi dar ..! na yeye ni mbunge wa bumbuli ..! simply alidai DAR ndio kuna kila kitu....
   
 15. O-man

  O-man JF-Expert Member

  #15
  Apr 13, 2012
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 318
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Mwanakijiji nimekukubali. Hilo moja. Wahenga walinena . . . "aliyeshiba hamjui mwenye njaa". Usemi huu na viongozi walio na madaraka na uwezo wa kuondoa kero hii hawajawahi kukosa mishahara, wamefanya kazi au la! Mimi naamini upo mfumo wa uwajibikaji. Tu-explore huo mfumo na wahusika wawajibike. 2015 ni mbali sana. Mwanakijiji kaliona na nina imani wengi wameliona lakini lilibakia vijiweni. Nawasilisha.
   
 16. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #16
  Apr 13, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  ni 'CONTEMPT' siyo 'CONTENT'
   
Loading...