SoC02 Mjadala wa wachezaji 12 wa kigeni kwenye ligi kuu Tanzania bara; bado hatui tulipojikwaa?

Stories of Change - 2022 Competition

chai ya moto

Member
Jul 27, 2021
25
72
Kama kuna biashara inayolipa sasa hivi ni biashara ya mpira wa miguu na vyote vinavyohusiana navyo,hapa nazungumzia biashara kama kuuza na kununua wachezaji,kuuza jezi na vifaa vya klabu,kuonyesha mpira,vituo vya runinga vinalipa fedha ili kupata haki za kurusha matangazo,udhamini mbalimbali, mashabiki kulipa viingilio vya kuingia uwanjani na mpira wa miguu ndiyo mchezo unaoongoza kwa watu kuuchezea kamari/kubashiri.

Pia mpira wa miguu umeleta ajira kwa vijana kwa kuucheza,kufundisha,kuamua(waamuzi) na wataalam mbalimbali wa mpira wa miguu wameajiriwa kwenye mpira wa miguu.Pia kuna wahasibu,madaktari,wapishi,maderava,wapiga picha,maafisa habari na watendaji wengine wote hao wanaendesha maisha yao kupitia mpira wa miguu.

Mpira wa miguu umewapa utajiri wachezaji waliocheza na wanaocheza ligi za Ulaya mfano mzuri kwa hapa Afrika ni Samuel Eto'o mchezaji wa zamani wa Cameroon na vilabu vya Barcelona,Inter Milan
na Chelsea ana utajiri wa dola za Marekani milioni 95,anamiliki biashara mbalimbali kama kampuni ya mawasiliano ya simu ya 9 Telecom na kampuni ya michezo ya kubashiri ya BETOO biashara hizi na utajiri wa Eto'o zimetokana na fedha alizokuwa analipwa wakati akicheza mpira.Biashara hizi za Eto'o zinalipa kodi na zimeajiri watu wa Cameroon.

Screenshot_20220911-174452_1.jpg

Picha kwa hisani ya mtandao wa Google ikimuonesha Samuel Eto'o siku alipokuwa anazindua kampuni yake ya michezo ya kubashiri ya BETOO.

Pia serikali zinafaidika kutokana na Mpira wa miguu, taarifa ya mtandao wa qz.com inasema msimu wa 2019/20 ligi kuu ya Uingereza ilichangia pauni bilioni 3.6 kwenye mfuko mkuu wa serikali ya Uingereza.Hizo ni fedha zilizotokana na kodi za kawaida, kodi za mishahara ya wachezaji na wafanyakazi,bima na vibali vya kufanyia kazi.

Taarifa hiyo pia inasema kuna wachezaji zaidi ya 500 wa Kiafrika wanaocheza soka Ulaya katika ligi mbalimbali lakini wengi wao wanatoka nchi za Afrika magharibi nchi kama Senegal ina wachezaji 62 wanaocheza soka Ulaya, Moroco wana 55, Nigeria wana 54, Ivory Coast wana 50,Ghana wana 46, Algeria wana 32,DRC wana 23 na Guinea wana 13.Wachezaji hawa wanapeleka fedha walizochuma Ulaya kwenye nchi zao ambazo zinaenda kujenga majumba ya kifahari,zinaenda kwenye uwekezaji na hivyo kulipa kodi kwa maendeleo ya nchi zao pamoja na kuzalisha ajira.

Kwa Tanzania idadi kamili haijulikani kwa sababu hatuwafuatilii ingawa kuna wachezaji watatu wanaofahamika kuwa wanacheza ligi kuu ya Ubeligji ambao ni Mbwana Samata, Kelvin John na Novatus Dismas, wengine wanaofahamika kama Haji Mnoga anachezea Portsmouth ya Uingereza ambayo ipo ligi ya madara ya chini.

Wakati kwa wenzetu soka inawapa utajiri sisi hatuna habari,tumekuwa tunajadili mambo madogo madogo ambayo hayana umuhimu,kwa kifupi hakuna nia ya dhati ya kukuza soka.

Timu yetu ya taifa imekuwa kichwa cha mwendawazimu, ambacho kila mtu anajifunzia kunyoa hakuna mafanikio kwenye timu ya Taifa Novemba 11,2021 timu yetu ya taifa ilifungwa 0-3 na timu ya taifa ya DRC mchezo huo ulichezwa kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam, matokeo ya mchezo huo yalisababisha kufa kwa matumaini ya Taifa Stars kucheza fainali za kombe la Dunia zinazotarajiwa kufanyika Qatar mwishoni mwa mwaka 2022,baada ya kutolewa hakuna mjadala wowote wa maana uliofanyika kujadili kwanini tumeshindwa kwenda Qatar.Pia hivi karibuni timu hiyo imeshindwa kufuzu kushiriki kombe la CHAN,ambalo ni maalum kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani.Mchezo wa kwanza ulichezwa August 28,2022 tulifungwa na timu ya taifa ya Uganda nyumbani 0-1,na pia walitufunga kwao 3-0.

Kama kawaida yetu hatuna mijadala ya maendeleo ,baada ya kushindwa kufuzu CHAN tumetoa lawama kwa baadhi ya wachezaji na wengine wanalaumu viongozi wa shirikisho la soka Tanzania (TFF),TFF nao wakamtwisha mzigo wa lawama kocha wa timu ya taifa Kim Poulsen na haikuwa ajabu kumfukuza.Kim alianza kufundisha Taifa stars Februari 15,2021 na akafukuzwa Agosti 29,2022.Taifa Stars kuanzia mwaka 2015 imefundishwa na makocha sita,ambao ni Mart Nooji, Boniface Mkwasa,Salum Mayanga, Etienne Ndayirajige, Emanuel Amunike na mwishowe Kim Poulsen.

Tatizo kubwa la mpira wetu wa miguu ni kuwa hatuandai wachezaji na ndiyo maana hivi karibuni kulizuka mjadala baada ya TFF kuongeza idadi ya wachezaji wa kigeni kufikia 12 wanaoruhusiwa kucheza kwenye mechi moja ya vilabu vyetu vinavyoshiriki ligi kuu ya NBC, wengine walidai ongezeko hilo litasababisha timu ya Taifa kukosa wachezaji mahiri kwa sababu ligi itatawaliwa na wachezaji wa kigeni na baadhi ya watu waliunga mkono ongezeko hilo.

Lakini kabla ya mjadala huo ilitakiwa tujiulize tumefikaje hapo? Kwanini timu zetu za ligi kuu hasa Azam,Simba,Yanga na Singida big stars zinakimbilia wachezaji wa kigeni? jibu ni moja tu kuwa hatuandai wachezaji wetu, wachezaji wa Tanzania wana vipaji vikubwa lakini wanakosa mafunzo ya soka tangu wakiwa watoto wanaibuka wakiwa wakubwa na wakiibuka wanakutana na wenzao walioandaliwa tangu wakiwa watoto,ambao wana vipaji na ujuzi lakini wetu wana vipaji tu hawana ujuzi na tukumbuke samaki mkunje angali mbichi .Huyu kijana wa Kitanzania anayekutana na wataalam akiwa na miaka zaidi ya 20 atakuwa tofauti sana na mchezaji wa kigeni anayekutana na wataalam tangu akiwa na miaka 6 au 7.

Screenshot_20220910-150119_1.jpg

Picha kwa hisani ya mtandao wa Google ikimuonesha mchezaji kinda Kelvin John anayechezea klabu ya ligi kuu ya Ubeligji,Kelvin Ni mfano mzuri wa kuandaa wachezaji wa mpira wa miguu tangu wakiwa watoto.

Wachezaji wa mpira wa miguu wanaandaliwa kwenye vituo maalum au shule za soka,mfano wa kituo kilichofanikiwa hapa Afrika ni kituo cha klabu ya Asec Mimosas kilichopo Abdjan, Ivory Coast kituo hiki kilichoanzishwa mwaka 1993 na Jean-Marc Guillon akiwa na lengo la kutengeneza wachezaji wa baadaye wa Asec na pia kuwapa elimu yaani elimu ya kawaida na elimu ya soka kwa ajili ya kuwauza Ulaya.Kituo hicho kimekuwa msaada mkubwa kwa vijana wa Ivory kwani wengi wao wamefanikiwa kwenda Ulaya kupitia kituo hicho.Wenyewe wanasema mchezaji akiwa na miaka 17-18 anaweza kucheza ligi ya mabingwa Afrika ambayo ni michuano mikubwa zaidi kwa ngazi ya vilabu Afrika na inayofuatiliwa na vilabu vingi vya Ulaya,wanaona michuano hiyo kama soko la kuuza wachezaji wao.

Baadhi ya wachezaji maarufu waliopita kwenye kituo hicho ni Yaya Toure mchezaji wa zamani wa Barcelona na Manchester city na timu ya Taifa ya Ivory Coast, Solomon Kalou mchezaji wa zamani wa Chelsea na timu ya taifa ya Ivory Coast na wengine wengi.Mchezaji wa karibuni kuuzwa Ulaya aliyeanzia kucheza mpira kwenye kituo hicho ni Karim Konate, Konate mweye umri wa miaka 18 aliuzwa kwenye klabu ya FC Salzburg.

Konate pia alianza kuchezea timu ya taifa ya Ivory Coast mwaka 2021 akiwa na umri wa miaka 17 na alianza kuchezea timu ya wakubwa ya Asec Mimosas tangu mwaka 2020 akiwa na miaka 16,je umri wa aina hii wachezaji wetu wanakuwa ngazi gani ya kucheza mpira?jibu ni rahisi wengi wanakuwa mitaani.

Screenshot_20220911-174158_1.jpg

Picha kwa hisani ya mtandao wa Google ikimuonesha mchezaji mahiri kinda wa Ivory Coast Karim Konate.

Kama kweli tunataka mafanikio kwenye mpira wa miguu ni lazima tuwekeze kwa kuanzisha vituo vya kuwaandaa wachezaji tangu wakiwa watoto,vituo hivi ni muhimu kwa sababu watoto wanafundishwa elimu ya kawaida,elimu ya soka ambayo inawapa ujuzi wa kusakata kandanda na ambayo pia inawafanya wawe wachezaji mahiri.

Kwenye vituo pia wachezaji wanafundishwa tabia njema,jinsi mchezaji wa kulipwa anatakiwa awe,jinsi ya kuwasiliana na watu ikiwemo kujifunza lugha za kimataifa.Mafunzo hayo yote yanalenga kumuandaa mchezaji kuwa wa kulipwa na ndiyo maana tunamuona Konate akiwa na miaka 17 anacheza timu ya taifa ya wakubwa ya Ivory Coast.

Karibuni kwa mjadala na naomba kura zenu.
 
View attachment 2353699

View attachment 2353707

View attachment 2353703

Mimi naitwa Lumola Nimekupigia Kura Naomba na Mimi unipigie Kura kupitia SoC 2022 - Tufuge nyuki kwa maendeleo endelevu na tuwalinde kwa wivu mkubwa
 
Mods naomba mnirekebishie kichwa cha habari neno hatui liwe hatujui.

Kwahiyo naomba kichwa cha habari kisomeke ; Mjadala wa wachezaji wa 12 wa kigeni kwenye ligi kuu Tanzania bara;bado hatujui tulipojikwaa?

Shukrani.
 
Back
Top Bottom