Mada ya malipo ya mishahara na posho za wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pamoja na watumishi wengine waserikali imekuwa gumzo kubwa katika jamii yetu. Baada Mh. Rais kutaja mshahara wake yupo mbunge ameomba kujua marupu rupu mengine ya Rais, mbali na mshahara wake. Lakini pia, ni kama wiki tu kulikuwa na thread hapa JF ikitukumbusha kuwa kila mbunge wa JMT analipwa Tzs.300,000 kwa siku kama sitting allowance. Kwa maana nyingine, kama mbunge atahudhuria kikao cha bunge kwa mwezi mzima anatakiwa alipwe Tzs.6m/- isiyo katwa kodi, achilia mbali malipo ya posho mbali mbali za kamati maalumu za bunge na msululu lukuki mingine. Hoja kubwa ya wananchi, ambayo hata wabunge wenyewe hawaja twambia sababu za msingi ni kwamba kazi za mbunge zinahusisha kuwakilisha wananchi katika vikao vya bunge vya pamoja. Ina maana kwamba pamoja na ofisi zao za kibunge katika jimbo husika, bado kikao cha pamoja bungeni ni sehemu ya ofisi zao. Meaning, kuhudhuria vikao vya bunge siyo kazi ya ziada kwa mbunge. Kwa nini mbunnge alipwe mshahara (salary) na posho (allowance) kwa kazi hiyo hiyo? Au ni kwa sababu mbunge analazimika kufanya kazi yake nje ya kituo/ofisi (eneo/jimbo) lake la kazi? Kama mtumishi mwingine wa serikali analipwa posho ya safari (per diem) kama atatakiwa kuwa nje ya kituo chake cha kazi, ni nini tofauti ya uhalali wa malipo ya hawa watuimshi wawili? I mean, kuna mtumishi gani mwingine anayelipwa mshahara unaolingana na mshahara wa mbunge halafu akalipwa posho ya safari ya Tzs.300,000+mafuta+...+..... ? Labda niulize tena kwamba nini benchmark, au ni wapi tena duniani nchi husika wanafanya hivi? Nitashukuru kupata mchango wa mbunge yeyote.