Mjadala wa ufisadi wa Tanesco sasa kupelekwa bungeni

Josh Michael

JF-Expert Member
Jun 12, 2009
2,523
77
KATIKA hali inayoashiria kwamba ni kuepuka mijadala ambayo inaweza kuwaweka pabaya, serikali imeamua kuwa itatoa taarifa ya uchunguzi wa tuhuma za ufisadi wa Sh1.4 bilioni ndani ya Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kwenye mkutano ujao wa Bunge utakaoanza Oktoba 25, mwaka huu, mjini Dodoma, Mwananchi limebaini.

Tuhuma hizo, zilikuwa zimetolewa katika mkutano uliopita wa Bunge na Mbunge wa Sumve, Richard Ndassa (CCM), akielezea kuwa fedha hizo zilitumika kifisadi, kukarabati nyumba saba.

Ndasa alisema nyumba moja ilikarabatiwa kwa Sh600 milioni ili baadae kigogo mmoja wa Tanesco ajiuzie kwa Sh60 milioni.

Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja alikuwa ameahidi wizara yake itazichunguza tuhuma hizo, na kuziweka bayana matokeo ya uchunguzi wiki hii.

Taarifa zilizolifikia gazeti hili jana zilieleza kwamba Ngeleja sasa ameamua matokeo ya uchunguzi, atayaweka hadharani bungeni.


Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Adam Malima alisema kwamba waziri Ngeleja anafahamu kwamba suala hilo, lazima alitolee taarifa kwa kuwa asipofanya hivyo, anaweza kujikuta anawekwa kitimoto na wabunge.


"Mimi ningekuwa mwandishi wala nisingejisumbua kwa hili kwa sababu hata kama Waziri (Ngeleja) hatalielezea bungeni, hili liko wazi wabunge watambana," alisema Malima.

Alipotakiwa kuelezea juu ya namna uchunguzi huo ulivyofanyika, Malima alisema kwamba wizara iliiamuru bodi ya wakurugenzi ya Tanesco kuchunguza suala hilo na kumpatia waziri taarifa itakayoweka bayana suala hilo.

Hata hivyo, Malima alikataa kuweka wazi endapo tayari waziri amekabidhiwa ripoti hiyo au la, lakini vyanzo vyetu ndani ya wizara hiyo, vilieleza kwamba tayari imewasilishwa ofisini kwake.

Vyanzo hivyo pia vilieleza kwamba Ngeleja akiitoa ripoti hiyo nje ya bunge, inaweza kuzua mjadala ambao inaweza ukaichanganya jamii.

Wakati akilipua tuhuma hizo katika mkutano wa Bunge uliopita, Ndasa alisema matumizi mabaya fedha yamekuwa yakikwamisha maendeleo mbalimbali nchi.


Ndasa ambaye alikuwa akichangia kwenye mjadala wa makadirio na matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini, alisema tathmini yake inaonyesha kwamba fedha zilizotumika kukarabati nyumba hizo saba, zingeweza kujenga nyumba mpya 20.

Tuhuma hizo, zilielekea kumshangaza Ngeleja wakati huo wakati bajeti ya wizara yake, ilikuwa ikijadiliwa na hakusita kudai kwamba zilikuwa ni habari mpya kwake.


Ngeleja alisema kuwa tuhumza hizo, ni changamoto kubwa kwake ambayo inambidi ajipange ili kuikabili na kuweka wazi suala hilo kwa jamii.

Wakati akilipua tuhuma hizo bungeni, Ndasa aliitaja nyumba ambayo ilikuwa ikarabatiwe kwa Sh600 milioni ili baadae kigogo wa Tanesco ajiuzie kwa bei chee ya Sh60 milioni ni namba 13 iliyopo Mtaa wa Toure/Chaza, Oysterbay.

Alisema nyumba nyingine, ni namba 89 iliyopo mtaa wa Gine ambayo ukarabati wake uligharimu Sh 250 milioni nyingine ni namba 65, iliyopo Mtaa wa Laibon ambayo iligharimu Sh 190 milioni na namba 459, Mtaa wa Mawenzi iliyogharimu Sh130 milioni.
Katika orodha hiyo, Ndasa alisema nyumba namba 93, iliyopo Mtaa wa Gine imegharimu Sh 88.5 milioni nyingine namba 315 mtaa wa Toure Drive iligharimu Sh79 milioni na namba 98 mtaa wa Uganda Line, imekarabatiwa kwa
 
Ziko wapi enzi hizo ambapo tuhuma tu zilitosha kumpeleka mtu ndani na kumpa mboko 24?Mbona kwa utaratibu wa sasa hivi inaelekea hakuna fisadi atakayefungwa?
 
Back
Top Bottom