Mjadala wa TANESCO kupandisha bei ya umeme kwa asilimia 155 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mjadala wa TANESCO kupandisha bei ya umeme kwa asilimia 155

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by EMT, Dec 1, 2011.

 1. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #1
  Dec 1, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Mnyika: Jitokeze kesho, 2nd Dec, 2011 Ukumbi IFM ktk Mkutano wa wadau ulioitishwa na TANESCO!Kukataa ongezeko la bei ya umeme

  Kesho tarehe 2 Disemba 2011 katika Ukumbi wa Makumbusho Dar es salaam (mkabala na IFM) kuanzia saa 4 asubuhi EWURA imeitisha Mkutano wa Wadau kujadili ombi la TANESCO la kupandisha bei ya umeme kwa wastani wa 155% (zaidi ya mara tatu ya bei ya sasa). Nawaomba wanamtandao wote tuhamasishe umma kwa kutumia TEHAMA (sms, facebook, twitter, email na njia nyingine) ili wananchi waweze kuhudhuria mkutano husika kwa wingi na kutoa maoni.

  Mtakumbuka kwamba tarehe 23 Novemba 2011 nilitoa taarifa kwa umma kwamba Serikali inapaswa kusitisha ombi la dharura la kupandisha bei ya umeme kwa kiwango kikubwa ili kuepusha athari katika usalama na uchumi kutokana na mfumuko wa bei na kupanda kwa gharama za maisha. Aidha, serikali inapaswa kuchukua hatua za haraka kulinusuru Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) dhidi ya mzigo mkubwa wa gharama unaotokana na ufisadi wa muda mrefu katika mikataba ya gesi asilia na gharama za mitambo ya kufua umeme wa dharura badala ya kuweka mkazo katika kuongeza bei ya umeme kwa wananchi wa kawaida.

  Izingatiwe kuwa tarehe 9 Novemba 2011 Mamlamka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) ilipokea ombi la dharura toka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) la kuidhinisha ongezeko la bei za huduma ya umeme kwa wastani wa asilimia 155 ya bei ya sasa (zaidi ya mara tatu).

  Naomba umma wa watanzania uzingatie athari za maombi hayo katika uchumi wa nchi na maisha ya wananchi kwa ujumla hivyo mjadala wa kitaifa unahitajika na natoa mwito kwa wananchi kuweza kutoa maoni yao kuanzia sasa. Aidha ni muhimu kwa wananchi kushiriki kwa wingi katika mkutano wa kukusanya maoni ya wadau ulioitishwa na EWURA tarehe 2 Disemba 2011.

  Umma wa watanzania ufahamu kwamba ongezeko hili sio ombi la TANESCO pekee bali ni agizo kutoka kwa serikali kwa kurejea maelezo ya Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja bungeni katika mkutano wa nne wa bunge na kusisitizwa na kauli ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda mwezi Septemba 2011 akihutubia mkutano wa hadhara mkoani Mara.

  Namshangaa Rais Jakaya Kikwete katika hotuba yake kwa taifa tarehe 18 Novemba 2011 alipozungumzia utekelezaji wa mpango wa dharura wa umeme hakuwaeleza watanzania kwamba uwasilishaji wa ombi hilo ni sehemu ya mpango huo wa dharura ambao utawaongezea wananchi bei ya umeme na gharama na maisha na hivyo kuathiri utekelezaji wa ahadi ya maisha bora kwa kila mtanzania.

  Wananchi wakumbuke kwamba hii ni mara ya pili katika kipindi cha takribani mwaka mmoja kwa TANESCO kupandisha bei ya umeme; mara ya kwanza ikiwa mwezi Januari 2011 ambapo umeme ulipanda kwa asilimia 18.5 na kuchangia katika kupanda kwa gharama za uzalishaji katika nchi na kuongeza ugumu wa maisha kwa wananchi.

  Ombi la TANESCO la wakati huo la kupandisha umeme lilikuwa ni asilimia 34 likakataliwa na EWURA na kushushwa mpaka asilimia 18.5, sasa Rais Kikwete, Waziri Mkuu Pinda na Waziri Ngeleja wanapaswa kuwaeleza watanzania sababu za kufanya ombi hilo la dharura kuwa la wastani wa asilimia 155 ili wananchi waweze kutoa maoni kwa kuzingatia mzigo ambao umma unataka kubebeshwa.

  Pamoja na matatizo ya kifedha ya TANESCO ambayo serikali inapaswa kuyashughulikia kwa pamoja na mambo mengine kutoa ruzuku katika kipindi hiki cha mpito; gharama kubwa za uzalishaji zinazolikabili shirika zinachangiwa na ufisadi wa muda mrefu katika mikataba ikiwemo ya uzalishaji wa gesi na ukodishaji wa mitambo ya kufua na pia maamuzi ya kukopa kibiashara katika kutekeleza mpango wa dharura wa umeme.

  Kabla ya kuongeza bei ya umeme kwa watanzania wa kawaida, Serikali iwaeleze wananchi imewapunguzia mzigo kiasi gani kwa kupitia upya mikataba ya kifisadi inayolinyonya Shirika la Umeme Tanzania kama ilivyopendekezwa kwenye ripoti mbalimbali ikiwemo katika maazimio ya Bunge ya mwaka 2008 juu ya mkataba wa ukodishaji wa mitambo ya kufua umeme ya Kampuni ya Richmond Develepment Company LLC ambapo orodha ya mikataba na makampuni mengine ilitajwa.

  Aidha, umma uelezwe pia ukweli iwapo uamuzi wa kuchukua mikopo ya kibiashara yenye riba kubwa umeongeza zaidi gharama za uzalishaji wa umeme na hivyo kuifanya TANESCO iongeze zaidi bei ya umeme kwa wateja ikizingatiwa kuwa tarehe 15 Julai 2011 na 13 Agosti 2011, nilisisitiza bungeni serikali ipunguze bajeti katika maeneo mengine yasiyokuwa ya lazima na kuelekeza rasilimali nyingi zaidi kwenye umeme bila kuongeza mzigo mkubwa wa riba utakaolipwa na wananchi kupitia ongezeko la bei.

  Uamuzi huu wa kupandisha kwa kiwango kikubwa bei ya umeme utasababisha ongezeko la ziada la mfumuko wa bei hali ambayo ni tishio wa usalama na uchumi wa nchi na maisha ya wananchi kwa ujumla.

  Serikali izingatie kwamba mfumuko wa bei nchini hivi sasa umefikia asilimia 17.9 na bidhaa zinazochangia mfumuko huo kwa kiwango kikubwa ni vyakula, mafuta na umeme. Kupanda kwa bei kwenye sekta ya nishati pekee kumekuwa kwa asilimia 37.4 na kusababisha kupanda kwa gharama za maisha, sasa viongozi wajiulize itakuwaje umeme ukapopanda kwa wastani wa asilimia 155.

  Wananchi wakumbuke kwamba katika hotuba yake kwa taifa tarehe 18 Novemba 2011 Rais Kikwete ameelezea kwamba mfumuko wa bei na kuporomoka kwa thamani ya shilingi ya Tanzania dhidi ya dola kwa ujumla kumetokana na uchumi wa nchi mbalimbali duniani hususani za Ukanda wa Sarafu ya Ulaya (Eurozone) kuwa katika kipindi kigumu na cha mashaka na kueleza kwamba suluhisho la matatizo la uchumi wetu litategemea uchumi wao.

  Kauli hii imedhihirisha kwamba Serikali haina mpango wa haraka wa kukabiliana na mfumuko wa bei, kuporomoka kwa shilingi na kupanda kwa gharama za maisha. Hali itakuwa mbaya zaidi iwapo tutaruhusu pamoja na sababu za nje ya nchi yetu tukaongeza vyanzo vya ndani vya kuongezeka kwa gharama za uzalishaji na bei za bidhaa kwa kupandisha bei ya nishati ya umeme ambayo chanzo chake ni hapa hapa nchini. Hivyo, mpango huu wa kupandisha bei ya umeme kwa wastani wa asilimia 155 unapaswa kusitishwa ama kubadilishwa kwa kulinda maslahi ya makundi mbalimbali kwa kuzingatia aina za matumizi.

  John Mnyika (Mb)
  Waziri Kivuli wa Nishati na Madini
  1/12/2011
   
 2. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #2
  Dec 1, 2011
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,934
  Likes Received: 2,085
  Trophy Points: 280
  Asilimia 155! Hivi hawa Tanesco/serikali inawaonaje/inawachukuliaje watanzania?
   
 3. Mchaga 25

  Mchaga 25 JF-Expert Member

  #3
  Dec 1, 2011
  Joined: Oct 29, 2011
  Messages: 463
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kutokana na wito wa kuhudhuria mkutano wa EWURA TAREHE 2 DECEMBER kujadili ongezeko la umeme wananchi wameamua kutumia fursa hiyo kutimiza kiu yao ya kupinga wizi na uonezi wa serikali, kwa malipo hewa ya DOWANS na ongezeko la umeme kwa asilimia 155% ambalo tanesco wameomba lipitishwee.
  MY TAKE


  Maumivu ya kichwa huanza polepole.
   
 4. J Mbungi

  J Mbungi Senior Member

  #4
  Dec 1, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  BY: John Mnyika
  Kesho tarehe 2 Disemba 2011 katika Ukumbi wa Makumbusho Dar es salaam (mkabala na IFM) kuanzia saa 4 asubuhi EWURA imeitisha Mkutano wa Wadau kujadili ombi la TANESCO la kupandisha bei ya umeme kwa wastani wa 155% (zaidi ya mara tatu ya bei ya sasa).

  Nawaomba wanamtandao wote tuhamasishe umma kwa kutumia TEHAMA (SMS, Facebook, Twitter, email na njia nyingine) ili wananchi waweze kuhudhuria mkutano husika kwa wingi na kutoa maoni.

  Soma zaidi:
  http://mnyika.blogspot.com/2011/12/jitokeze-kesho-2nd-dec-2011-ukumbi-ifm.html

   
 5. V

  Vonix JF-Expert Member

  #5
  Dec 1, 2011
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 1,994
  Likes Received: 508
  Trophy Points: 280
  Biashara matangazo.
   
 6. BBJ

  BBJ JF-Expert Member

  #6
  Dec 1, 2011
  Joined: Sep 2, 2011
  Messages: 1,183
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Dah!Ma viongozi haya yaliyopo madarakani dawa yao ni kitanzi tu.Hayawezi kutuumiza hivi WA-TANZANIA.
   
 7. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #7
  Dec 1, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,657
  Likes Received: 35,418
  Trophy Points: 280
  Utapandishaje bei ya huduma ambayo si ya uhakika? Mijitu mingine bana
   
 8. Mchaga 25

  Mchaga 25 JF-Expert Member

  #8
  Dec 1, 2011
  Joined: Oct 29, 2011
  Messages: 463
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  kesho mpaka kieleweke unless otherwise
   
 9. jino kwa jino

  jino kwa jino JF-Expert Member

  #9
  Dec 1, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 769
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Wamepandisha bei ya sukari tumevumilia ila hapa knye umeme patachimbika, sukari naweza nisinywe chai ila umeme anapokea mwenye nyumba nisipolipa atanifukuza ............oooooooooh my god sijui nitembee na panga au kisu au sime!!

  Jamani hivi ni wapi wanakodisha bastola na risasi zake
   
 10. M

  Mzalendoo Member

  #10
  Dec 1, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 98
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Haya mambo wameshafanya maamuz serikaln kitambo kuwa umeme lazma upande hvyo hyo kesho hata tuchangie tukiwa uchi wa mnyama watapandisha tu,hil ni sikio la kufa ,tunalalamka posho bungen lakn wap,twalalamika sheria ya mswaada wa katiba lakn wap,hii serikal imechooka.
   
 11. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #11
  Dec 1, 2011
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  Ndg yangu J. Mnyika, naamini unalipenda taifa lako, sina shaka kabisa. kama kuna kitu chadema mnakosea ni kuwasaidia ccm kimipango. hebu waacheni wapandishe hizo bei za umeme, watakuwa wamejipotea uungwaji mkono jambo litakalorahisisha mapinduzi ya kifikra miongoni mwa watz. mkiwashtua wakaghairi ni watanzania wachache sana watakaotambua mchango wa chadema katika hili, sanasana mtawapa nafasi ccm na serikali yake kujinadi ni sikivuuu, inawajali watu wakeee! waacheni wakosee warahisishe kazi ya ukombozi.
   
 12. f

  firehim Member

  #12
  Dec 2, 2011
  Joined: Oct 10, 2011
  Messages: 94
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Leo Ewura imeitisha mkutano wa wadau kujadili ombi la Tanesco la kupandisha bei ya umeme kwa asilimia 155 ambao utafanyika katika jumba la Makumbusho ya Taifa kuanzia saa 4:00 asubuhi. Nawaomba wadau tujitokeze kwa wingi kupinga ongezeko hilo kwani litatuumiza sana sisi wanacnhi wa kawaida. Hii bei tuliyonayo tu inatuumiza halafu tupandishiwe tena si ndo balaa.

  Nawasilisha.
   
 13. F

  FUSO JF-Expert Member

  #13
  Dec 2, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,889
  Likes Received: 2,346
  Trophy Points: 280
  usitudanganye, hatuwezi kupinga sera za chama chetu mzee, msilete uvunjifu wa amani hasa mkizingatia tuna sherehe za miaka 50 ya uhuru wetu.
   
 14. Sordo

  Sordo JF-Expert Member

  #14
  Dec 2, 2011
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 397
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Huko hakuna Alshabab?
   
 15. f

  firehim Member

  #15
  Dec 2, 2011
  Joined: Oct 10, 2011
  Messages: 94
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ahaa fuso haya sio maandamano ni kongamano juu ya upandishwaji wa bei . Inamaana ww unasupport bei iongezeke tena ili dowans ilipwe?
   
 16. kikahe

  kikahe JF-Expert Member

  #16
  Dec 2, 2011
  Joined: May 23, 2009
  Messages: 1,273
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Huu ni unyonyaji wa watanzania. Mshahara hawataki kupandisha, iweje sasa mnapandisha bei ya umeme? Wale wazee walikutana na JEIKEI wakashangilia kutokupandishwa mshahara sasa sijui wataseme nini kuhusu hili
   
 17. s

  semako Senior Member

  #17
  Dec 2, 2011
  Joined: Nov 10, 2011
  Messages: 102
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  TANESCO hawana budi kufanya hivyo,kumbuka tumejikwaa Richmondi na haya ndio matokeo;Taasisi za serikali hazililpi bili,wenzetu Zanzibar ndo hawalipi kabisaaa ukisema walipe utasikia tunavunja muungano sasa TANESCO watajiendesha vipi?
   
 18. Goldman

  Goldman JF-Expert Member

  #18
  Dec 2, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 1,262
  Likes Received: 853
  Trophy Points: 280
  it can only happen in tz!
   
 19. kikahe

  kikahe JF-Expert Member

  #19
  Dec 2, 2011
  Joined: May 23, 2009
  Messages: 1,273
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Huu ni unyonyaji wa watanzania. Mshahara hawataki kupandisha, iweje sasa mnapandisha bei ya umeme? Wale wazee walikutana na JEIKEI wakashangilia kutokupandishwa mshahara sasa sijui wataseme nini kuhusu hili
   
 20. S

  Samkyjr JF-Expert Member

  #20
  Dec 2, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 364
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Du hii bei ya sasa watu tumeacha kabisa kutumia majiko ya umeme wamebaki jwtz na polisi kwenye kota zao sasa kama mapendekezo yoa yatapita sijui hali itakuwaje.
   
Loading...