Mjadala wa Sheria Mpya ya Madini: Sintofahamu yaendelea Dodoma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mjadala wa Sheria Mpya ya Madini: Sintofahamu yaendelea Dodoma

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pascal Mayalla, Apr 21, 2010.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Apr 21, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,552
  Likes Received: 18,233
  Trophy Points: 280
  Hali ya sintofahamu kuhusiana na hatima ya mjadala wa sheria mpya ya madini, ambapo Spika Sitta jana alitangaza kwa mbwembwe kuwa mjadala huo ni leo, ametangaza kabisa ili wachangiaji wajiandae.

  Sintofahamu hiyo imeibuka asubuhi hii hapa Dodoma, baada ya kukutikana habari kuwa mjadala huo haupo tena na badala yake, waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, atatoa taarifa ya serikali kuhusu hilo siku ya Ijumaa, ambyo ndio siku ya mwisho ya kikao hiki cha 19.

  Update 8:00 am 22/04/10

  Sintofahamu hii, itamalizika rasmi Saa 5:00 asubuhi hii (Aprili 22, 2010), baada ya kipindi cha maswali na majibu, Muswada huu utawasilishwa rasmi na Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Wiliam Ngeleja.
   
 2. Technician

  Technician JF-Expert Member

  #2
  Apr 21, 2010
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 843
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  "The fault is not in the stars, but in ourselves." We created our circumstances by our past choices. We have both the ability and the responsibility to make better choices beginning today."
   
 3. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #3
  Apr 21, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Hivi jameni kuna mdau mwenye rasimu ya hiyo sheria mpya ya madini? tutoe maoni yetu
   
 4. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #4
  Apr 21, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,552
  Likes Received: 18,233
  Trophy Points: 280
  Jana nilikaa na Mhe. Zitto mahali, akanijulisha wameshaukamilisha mswada huo, waliusasambua wote na kuuunda upya, hivyo uamuzi wa serikali kuuondoa hatua za mwisha, ni uthibitisho kuwa mambo bado, hivyo hakuna mali popote itakapopatikana rasimu hiyo.
   
 5. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #5
  Apr 21, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,552
  Likes Received: 18,233
  Trophy Points: 280
  Hii sintofahamu kuhusiana na muswada huu, ni kuvuja kwa pakacha, au blessing in disguise kwa sababu serikali imefanya kiherehere cha kuukimbiza bungeni hima hima under the cerficate of urgency kana kwamba ni jambo la dharura sana kumbe lengo ni kutekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM, jamaa aliahidi, na sasa wamekumbuka shuka alfajiri. Hii sintofahamu, itatoa fursa kwa wanaharakati kuujadili kwa kina.

  Kitachofanyika, ni Ngeleja kuomba radhi kuwa wanaurudisha serikalini, utawasilishwa wiki ya mwisho ya bunge la bajeti, wakati huo wabunge wameshajichokea, utasomwa kwa mara ya kwanza na kujadiliwa kwa nusu siku, utasomwa kwa mara ya pili na mara ya tatu papo kwa papo halafu huo... utapita!.
   
 6. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #6
  Apr 21, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,552
  Likes Received: 18,233
  Trophy Points: 280
  Kikao cha Bunge kimeanza kwa hati mbalimbali kuwasilishwa mezani. Nilidhani spika angezumzia majaaliwa ya mswada wa madini, bado hajazungumza, nadhani atazungumza saa 4:30 baada ya kipindi cha maswali na majibu.
   
 7. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #7
  Apr 21, 2010
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Apart from kutimiza ahadi, wale jamaa wa Uranium wanataka kuanza kujenga na hakuna legal framework. Nasikia hata uranium regs zimekuwa tayari. Hilo vipi Mkuu Pasco katika pita zako huko? Did the government get loan/grant to revise this Act?
   
 8. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #8
  Apr 21, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,552
  Likes Received: 18,233
  Trophy Points: 280
  Jana naibu waziri wa madini, Malima, alizungumzia kidogo issue ya Uranium. Serikali haihitaji loan/grant kurevise sheria zozote, ila nijuavyo mimi kuna sheria zinakuwa revised under foreign pressure, kama hili la sheria kuwahukumu maharamia sio letu, hata sheria ya anti terrorism sio yetu.

  Mataifa yenye nguvu, huwachukua waserikali wanene, kuwapiga trip nene ya nguvu huko majuu na fungu nene la shopping, wakirudi tuu, sheria inatinga bungeni.

  Hii ya madini, nadhani kina Zitto wameitight sana kwa kuwabana wawekezaji, wenyewe wakaipata, wakaikatishia denge kwa JK kuwa ikipita tuu, sisi tunafungasha!. JK atakuwa kampigia Ngeleja asitopishe kabla.
   
 9. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #9
  Apr 21, 2010
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  Mswaada huo ni kitanzi cha CCM, tusubiri tuone naye JS atasema nini kwani ndiye anayetutayarishia miswaada yote ya madini TZ na nafikiri huu umeandaliwa kwa haraka ya wawekezaji na ili ccm wapate senti za uchaguzi toka kwa akina JS na watu wake
   
 10. Kisoda2

  Kisoda2 JF-Expert Member

  #10
  Apr 21, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 1,240
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Mkuu ni hatari,hapo kwenye nyakundu weka wazi kabisaa,ikibidi nitafute ppt za watoto na kutafuta chimbo la karibu.
   
 11. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #11
  Apr 21, 2010
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Unajua wakati wa Ben ishu kama hii angekuwa Dom na angefanya maandalizi yake mapemaaaa. But duh, tuendako ni kiza kitupu.
   
 12. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #12
  Apr 21, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Kuna kitu fish nini kinaendelea.Hizi kalenda isije kuwa kama Richmomd kalenda mpaka hamu zikaisha..Haya na tusubiri tuone.
   
 13. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #13
  Apr 21, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,552
  Likes Received: 18,233
  Trophy Points: 280
  Spika katangaza wajumbe wa kamati ya nishati na madini wakutane saa 5 hii. Waunge wote wamegaiwa nakala za sera ya madini na kutangaziwa ili wajiandae kuchangia vizuri.
  Fungu la CDCF zimetoka, waraka wa mgao umetoka.
  Spika hajazungumzia chochote kuhusu muswada wa sheria mpya ya madini. Something is fishy.
   
 14. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #14
  Apr 21, 2010
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  ina manaa utajadiliwa sio? sidhani kama watauacha this period

   
 15. R

  Rayase Member

  #15
  Apr 21, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 82
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  MmmmH Thanks for good updates! kwa kweli me nitashangaa kama kuna watu kwa nia kabisa wanataka kutemper na muswada wakati mapendekezo ya tume yapo! This is too much! wanataka kumwaibisha rais tena asiini afu urudi bungeni
   
 16. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #16
  Apr 21, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Na kama ni kufungasha waache wafungashe. Hatishiwi mtu nyau hapa. Madini ni yetu.
   
 17. Mdau

  Mdau JF-Expert Member

  #17
  Apr 21, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,771
  Likes Received: 251
  Trophy Points: 180
  Muungwana hana neno na mtu...yeye kwake ndoto zilishatimia,so liwalo na liwe...
   
 18. L

  Lecturer New Member

  #18
  Apr 21, 2010
  Joined: Apr 17, 2008
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mining bill
   

  Attached Files:

 19. P

  PELE JF-Expert Member

  #19
  Apr 22, 2010
  Joined: Dec 23, 2009
  Messages: 229
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Muswada wa madini waitoa jasho serikali
  Wednesday, 21 April 2010 23:20

  [​IMG] Spika wa Bunge Samwel Sitta

  Habel Chidawali na Frederick Katulanda, Dodoma

  MUSWADA wa Sheria mpya ya madini unaendelea kuitoa jasho serikali baada ya jana kukwama kuwasilishwa bungeni kwa siku ya pili bila maelezo.Juzi Spika wa Bunge, Samuel Sitta aliwaeleza wabunge kuwa muswada huo ambao tayari umeleta mvutano mkubwa katika jamii ungewasilishwa jana baada ya kushindikana Jumatatu iliyopita lakini, tofauti na ahadi hiyo, haukuwamo kwenye ratiba ya shughuli za Bunge.

  “Niwaombe wabunge kuwa kesho (jana) tutajadili muswada wa sheria ya madini, niwaombe mkajiandae,” alisema Spika Sitta wakati wa matangazo ya mwisho kabla ya kuahirisha Bunge juzi.

  Lakini jana orodha ya shughuli za Bunge hazikuonyesha muswada huo na Spika baadaye aliwatangazia wajumbe wa Kamati ya Nishati na Madini mkutano baada ya kipindi cha maswali na majibu.

  Mbali na mkutano huo wa wajumbe wa Kamati ya Nishati na Madini, pia Spika Sitta alitangaza mkutano wa wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) baadaye jioni jana.

  “Leo muswada wa sheria ya madini hautawasilishwa kwa sababu hali bado ngumu sana, unaendelea kujadiliwa ili kuhakikisha ukiwasilisha haukumbani na upinzani na unapita kwa sababu hiki ni kipindi cha kuelekea uchaguzi,” alieleza mmoja wa wabunge ambaye hakupenda kuandikwa jina lake gazetini.

  Wabunge wengine waliozungumza na gazeti hili jana walisema kitendo cha serikali kushindwa kuwasilisha muswada huo ni dalili ya waziri mwenye dhamana kusoma alama za nyakati na kuugopa kukwama kuupitisha.

  "Waziri angelazimisha kuleta Muswada huo ni wazi kuwa angekutana na kiyama kama alichokutana nacho Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi ambaye wabunge walimgomea katika miswada yake miwili," mbunge mmoja ambaye hakutaka atajwe gazetini alisema.

  Wadau walianza kushikwa wasiwasi kuhusu muswada huo pale gazeti hili liliporipoti taarifa za ndani kwamba Rais Jakaya Kikwete ametoa maelekezo maalum kutaka muswada huo ujadiliwe kwa hati ya dharura.

  Mbali na wadau mbalimbali kupinga muswada huo waziwazi, Waziri na Kilimo, Chakula na Ushirika Stephen Wassira na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige waliupinga muswada huo hadharani wakati wa semina ya Kamati ya Madini iliyofanyika mjini hapa wiki iliyopita.

  Kitendo cha muswada huo kupingwa na viongozi wa dini na hata mawaziri kimeonekana kuistua serikali kiasi cha kusitisha kuwasilisha haraka hivyo kuamua kuutayarisha upya ili kukidhi mahitaji ya wengi.

  “Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini ya Bunge, Shelukindo anawatangazia wajumbe wote wa kamati hiyo kuelekea katika kikao cha kamati katika Ukumbi wa Pius Msekwa kuanzia majira ya saa 5 asubuhi,” alisema spika Sitta na kuongeza;

  “Nyaraka za sera za madini ziko tayari zimewekwa katika masanduku yenu, naomba mzichukue na kuzisoma kwa makini waheshimiwa wabunge.”

  Jana ilikuwa siku ya pili kwa Kamati ya Nishati na Madini kukutana baada ya juzi kutwa nzima wajumbe wake kuendeleza majadiliano hayo hadi usiku jambo linaloonyesha kuwa bado ngoma ni nzito.

  Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini William Shelukindo jana alijifungia na kamati yake na kila alipopigiwa simu ya mkononi iliita bila mafanikio muda wote.

  Hata hivyo, Shelukindo aliwahi kukaririwa akisema kamati hiyo haitaweza na wala haithubutu kupitisha vitu ambavyo vinaopnekana wazi kuwa na utata na ambavyo havitakuwa na tija kwa Watanzania.

  Kwa mujibu wa ratiba ya Mkutano wa Bunge unaoendelea mjini hapa, sheria hiyo ilipaswa kuwasilishwa bungeni tangu siku ya Jumatatu ambapo ungejadiliwa kwa siku mbili hadi jana, lakini haikuweza kuwasilishwa.

  Mwishoni mwa wiki Wizara ya Nishati na Madini iliitisha semina katika Ukumbi wa Pius Msekwa ambapo wabunge pamoja na wadau wa madini walionyesha nia ya wazi kuwa walitaka kuukwamisha muswada huo.

  Katika semina hiyo, mawaziri wawili walionyesha wazi kuwa walikuwa wanapingana na serikali kuwa hawangekuwa tayari kuunga mkono muswada huo kwa kuwa ulikuwa ukiwakandamiza wananchi.

  Jana Waziri wa Kilimo na Chakula, Stephen Wasira aliliambia Mwananchi kuwa kupinga kwake muswada hakuwa akiikomoa serikali kama alivyoripotiwa katika katika vyombo vya habari bali ilikuwa ni makusudi mazima ya kumsaidia waziri mwenzake.

  “Mimi sikuwa napinga muswada hata kidogo kama watu wanavyosema, lakini nilikuwa na kila sababu kwa kuwa nilikuwa namsaidia Waziri mwenzangu pamoja na Watanzania wote ambao wanaguswa katika sekta hiyo,” alisema Wasira.

  Kuhusu baadhi ya watu kumtaka ajiuzulu wadhifa huo kutokana na mabishano hayo Wasira alisema “Sina cha kusema” hata alipotakiwa kuendelea kuzungumza zaidi aliondoka na kumuacha mwandishi.

  Hata hivyo, baadhi ya watu wanaonekana kuwatetea mawaziri hao wakisema kuwa ilikuwa ni haki yao na kwamba hawatakiwi kuhukumiwa kwani mabishano yao yalikuwa kwenye semina na sio ndani ya kikao halali.

  Kabla ya hapo walishakaa wabunge tena ambapo waliweza kulumbana bila ya mafanikio kwani taarifa za ndani ya kikoa hicho zilidai kuwa kulikuwa na malumbano makali jambo lililothibitishwa na mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe.

  “Ni kweli tulikuwa na malumbano makali sana, lakini ni ya kawaida tu wala sio jambo la kutisha maana kitu kinachogusa masilahi ya nchi hatuwezi kukipitisha hivi hivi tu,” alisema Ziito wakati akizungumza Mwananchi katika viwanja vya Bunge juzi.

  Hata hivyo, habari zilizolifikia Mwananchi kutoka kwa mmoja wa wabunge ambaye ni mdau wa kutoka katika maeneo yanayozalisha madini alisema kuwa muswada huo unatarajia kuwasilishwa siku ya Ijumaa jambo linaloonyesha kuwa wabunge watakuwa wamenyimwa nafasi ya kuchangia.

  Siku ya Ijumaa ilikuwa na ratiba za wabunge kupkiea Taarifa za kamati ya Miundombinu kuhusu Azimio la Bunge kuhusu Utendaji wa kazi usioridhisha wa kampuni ya Tanzania International Container Terminal Services (TICTS) pamoja na Uendeshaji usioriudhisha wa Shirika la Reli Tanzania uliofanywa na Kampuni ya RITES ya India


  Mambo mengine yaliyotarajia kuwasilihwa siku hiyo yaliwasilishwa jana ambayo ni pamoja na taarifa za Hesabu za serikali za Mitaa,Serikali Kuu pamoja na Hesabu za Mashirika ya Umma ambazo zote ziliwasilishwa jana
   
 20. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #20
  Apr 22, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,552
  Likes Received: 18,233
  Trophy Points: 280
  Update 8:00 am 22/04/10

  Sintofahamu hii, itamalizika rasmi Saa 5:00 asubuhi hii, baada ya kipindi cha maswali na majibu, Muswada huu utawasilishwa rasmi na Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Wiliam Ngeleja.
   
Loading...