Mjadala wa posho na kodi bado wawaka Bungeni; Lissu awawashia moto CCM

Unajua muungwana ukitaka kumtukana mtu kiiungwana unajifanya umesahau message inakuwa sent and delivered. Ndicho kitu alichokifanya Lissu. Amemtukana kiungwana tu Msingida mwenzake
 
LISSU kweli ni mwanasheria wa ukweli kawachachafwa kwa hoja wabunge wa CCM ambao hawana uzalendo na nchi hi wanapitisha vitu kwa wingi wao bila kuangalia maslahi ya TAIFA,tuichukie CCM,TUIOGOPE KAMA UKOMA.
 
Kumbukeni siku nchi ikiingia katika machafuko kutokana na uwekaji wa msingi mbovu, hapatakuwa na habari ya chama, kabila, rangi wala dini. Gose manzi ga nyanza!
 
Yes Nyalunda was on the receiving end! but he won it. Lissu ni Mwanaume... kwangu mimi ni bora X1000 ya mbowe
 
Mbowe anaingiaje hapo!!au ilimradi umeandika tu.Inaonekana Mbowe anakunyima sana usingizi na bado hadi mchambie mchanga mwaka huu.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Nyirandu got exactly what he wanted! Alinibore sana jinsi alivyojibu swali kwa nyodo na kujiona! Rxn ya Lissu was appropriate! Kuanzia statement yenyewe, "he was vaguely bumbling empty words" ukiachilia mbali kuitwa waziri mdogo!
 
Nimekukubali mkuu..huyo Nyalandu hastahili hicho cheo.

Nyalandu ni kafisadi kadogo .Kalibebwa na kanisa la kilutheri na mwaka jana askofu akataka kuka mwaga siju iliuwaje.Kana nyondo nakmbuka tulikutana Ujerumani kakaleta ubisho watu wakakatolea uvivu .
 
Kukatolea uvivu!Fafanua hapa.
 
Yaani alinipa raha sana; kwakweli pamoja na uchache wa wapinzani, wanawafunika kishenzi!

Lissu ni bonge la mjaja, yaani hapo alikuwa anamaanisha nyarandu ni mdogo katika hoja, nimependa alivyomsurpress maana hawa mawaziri utadhani sio watanzania.
N

Nimeiangalia hiyo drama mpaka nikapata raha. maana mpira ulikuwa unachezwa kwa pasi za ukweli ... hapa lissu, hapa Zitto na kijana Mnyika. Pamoja na kuwa wamechomoa hoja zote kwa wingi wao; ila joto la jiwe walionja.

Nilicheka pale AG alipolazimishwa kuomba msamaha na zitto baada ya kumpiga dongo lissu eti anataka kuonekana kwenye TV. Zitto akampiga dogo kuwa ametoka kuumwa; mzee mzima akanywea.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Poor! Nyalandu...leo imekuwa bahati mbaya ata mkeo Faraja Kotta ameshuhudia ukithbtsha uwezo wako mdogo wa kujbu maswali ya Msingi...ulitaka kuwaonyesha Wanasingida kuwa Msingda mwenzako Lissu s chochote...bt u fierced a finger in a molten Magma..it wasn't a Spongy!...muhimu n kuwa wewe ndo wazir uliye bado na kinga kubwa ya kuzuia kutetemeka...wenzako n waathirika wa kutetemeka hasa wakimuona Lissu
 
• ZITTO, MNYIKA NA LISSU WAITOA JASHO SERIKALI

BUNGE jana liligeuka sehemu ya majibizano na kurushiana vijembe baina ya wabunge wa upinzani hususan wale wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa upande mmoja na viongozi wa serikali wakiongozwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Aliyeanzisha moto wa ‘vijembe’ hivyo alikuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema, ambaye alisema Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (CHADEMA), anafanya mabishano bungeni kwa lengo la kutafuta umaarufu wa kuonekana katika runinga.

Lissu alikuwa akitoa hoja kwenye mjadala wa kupitia vifungu vya sheria na kupokea mapendekezo ya Muswada wa Sheria ya Fedha kwa mwaka wa fedha 2011 wakati Bunge lilipokaa kama kamati.
Baada ya kauli ya Werema, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (CHADEMA), aliomba mwongozo wa Spika kuhoji kwanini Werema amekuwa akitumia kauli za kuudhi bungeni wakati wabunge ni viongozi.
“Mheshimiwa Spika, ninachoamini ni kuwa wote tuliomo humu ndani ni viongozi na tumepigiwa kura na wananchi ili kuwawakilisha, kauli ya Werema ni ya kuudhi. Kauli ya kuwa mbunge aliyekuwa akitoa hoja anatumia runinga ili aonekane kwa wananchi na kujitafutia umaarufu ni ya kuudhi, sina hakika kama mwanasheria huyo ni mzima ama anaumwa, naomba mwongozo wako,’’ alisema.

Spika wa Bunge, Anne Makinda, alitoa mwongozo katika suala hilo ambapo alisema kauli za kuudhi bungeni hazitakiwi, kwa kuwa chombo hicho kinatawaliwa na kanuni na taratibu kilichojiwekea.
“Jamani humu ndani si sehemu ya kutoleana maneno ya kuudhi, namuomba Mwanasheria Mkuu wa Serikali afute usemi wake ndani ya Bunge ili liendelee,” alisema Makinda. Baada ya mwongozo huo, Werema alisimama na kusema yeye ni mzima kimwili na kiakili na haumwi kama alivyosema Zitto wakati akiomba mwongozo wa Spika. Werema baada ya kusema hivyo bado alionekana kutokubaliana na uamuzi wa Spika Makinda na badala yake akawa anaendelea kuzungumza lakini Makinda alimsisitizia afute kauli.
Mwanasheria Mkuu huyo, aliamua kutii agizo la Spika Makinda kwa kufuta usemi wake kuwa wapo baadhi ya wabunge ambao wanatumia Bunge kwa kujionyesha kwa wananchi kupitia katika runinga.

Baada ya Werema kufuta usemi huo ikafuatia zamu ya Zitto kufuta usemi wake kuwa Werema anaumwa kutokana na kutoa majibu ya kuudhi bungeni.
Awali Lissu alitaka kuondolewa kwa mamlaka anayopewa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ya kutoa misamaha ya kodi, ambapo alidai kuwa, mamlaka hayo hutumika kama mwanya wa rushwa. Wakati akijibu hoja hiyo, Werema alisema ni vema kamsema Lissu ili awe huru kwani amekuwa na tabia ya kusema mambo bila kufikiri, kwa sababu ya kutaka kuonekana kwenye runinga.
Lissu pia aliingia katika mzozo tena baada ya kutaka posho kubwa zinazotolewa kwa watumishi zikatwe kodi, lakini hoja hiyo ilipingwa na wabunge. Baadaye Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi, alisimama na kuunga mkono hoja ya Lissu na kueleza kuwa mshahara unaotolewa kwa wabunge ni mkubwa na akashauri kuwa hoja ya posho hizo iwasilishwe kwenye Tume ya Kanuni ili ipitie suala hilo.

Lissu pia aliingia katika mzozo na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Lazaro Nyalandu, pale aliposema kuwa anashangazwa na waziri mdogo (Nyalandu) kusema misamaha inayotolewa na serikali ina tija.
Alisema tume kadhaa zimekwisha kuundwa kuchunguza misamaha hiyo, hasa ile ya kampuni za madini na kubaini kuwa haina manufaa. Baada ya kauli hiyo, wabunge wa CCM walipiga kelele kudai kauli hiyo ya Lissu ni dharau na kumtaka aifute. Lissu alilazimika kuifuta kauli hiyo baada ya kusema kuwa amesahau kuwa hivi sasa waziri mdogo anaitwa Naibu Waziri.

Moto wa wabunge wa CHADEMA uliendelezwa baada ya Mbunge wa Ubungo, John Mnyika kusimama jana jioni na kupinga eneo moja katika muswada huo huo wa fedha lililokuwa likipendekeza wawekezaji kupewa nafuu ya kulipa kodi katika kipindi cha miaka mitano, huku yeye (Mnyika) akipendekeza iwe mitano.
Hoja hiyo ya Mnyika iliungwa mkono na Mbunge wa CCM, Simbachawene na kusababisha miguno ya kushangiliwa na wabunge kadhaa kwa makofi, kabla ya Naibu Waziri Nyalandu kusimama na kusisitiza kwamba pendekezo kwamba miaka 10 ilikuwa ni muhimu.

Mabishano hayo ambayo yaliibuka wakati Bunge lilipokaa kama Kamati ya Matumizi, yalimalizwa na Mwenyekiti Makinda ambaye alipoomba wabunge wajibu kwa kauli za ndiyo na siyo, alisema waliounga mkono pendekezo la serikali walikuwa wameshinda.
Uamuzi huo wa Makinda ulifuatiwa na sauti ya Zitto aliyesikika akimtaka mwenyekiti huyo kutumia utaratibu wa wabunge kupiga kura za kuhesabiwa ili kujua idadi kamili ya wabunge waliounga mkono hoja ama ya Mnyika au ile ya Nyalandu (serikali). Makinda aliendelea na vifungu vingine akionyesha ama kutosikia au kutotilia maanani ushauri huo.

Tanzania Daima
 
hizi si dharau jamani? kwa nini spika awe na nguvu hivi?
 
Wanahamishia mashambulizi kwenye mitandao sasa, maana kazi ya mitandao inashika kazi number one kwa uelimishaji katika kizazi kipya
 
• ZITTO, MNYIKA NA LISSU WAITOA JASHO SERIKALI

BUNGE jana liligeuka sehemu ya majibizano na kurushiana vijembe baina ya wabunge wa upinzani hususan wale wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa upande mmoja na viongozi wa serikali wakiongozwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Aliyeanzisha moto wa ‘vijembe' hivyo alikuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Frederick Werema, ambaye alisema Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (CHADEMA), anafanya mabishano bungeni kwa lengo la kutafuta umaarufu wa kuonekana katika runinga.

Lissu alikuwa akitoa hoja kwenye mjadala wa kupitia vifungu vya sheria na kupokea mapendekezo ya Muswada wa Sheria ya Fedha kwa mwaka wa fedha 2011 wakati Bunge lilipokaa kama kamati.
Baada ya kauli ya Werema, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (CHADEMA), aliomba mwongozo wa Spika kuhoji kwanini Werema amekuwa akitumia kauli za kuudhi bungeni wakati wabunge ni viongozi.
"Mheshimiwa Spika, ninachoamini ni kuwa wote tuliomo humu ndani ni viongozi na tumepigiwa kura na wananchi ili kuwawakilisha, kauli ya Werema ni ya kuudhi. Kauli ya kuwa mbunge aliyekuwa akitoa hoja anatumia runinga ili aonekane kwa wananchi na kujitafutia umaarufu ni ya kuudhi, sina hakika kama mwanasheria huyo ni mzima ama anaumwa, naomba mwongozo wako,'' alisema.

Spika wa Bunge, Anne Makinda, alitoa mwongozo katika suala hilo ambapo alisema kauli za kuudhi bungeni hazitakiwi, kwa kuwa chombo hicho kinatawaliwa na kanuni na taratibu kilichojiwekea.
"Jamani humu ndani si sehemu ya kutoleana maneno ya kuudhi, namuomba Mwanasheria Mkuu wa Serikali afute usemi wake ndani ya Bunge ili liendelee," alisema Makinda. Baada ya mwongozo huo, Werema alisimama na kusema yeye ni mzima kimwili na kiakili na haumwi kama alivyosema Zitto wakati akiomba mwongozo wa Spika. Werema baada ya kusema hivyo bado alionekana kutokubaliana na uamuzi wa Spika Makinda na badala yake akawa anaendelea kuzungumza lakini Makinda alimsisitizia afute kauli.
Mwanasheria Mkuu huyo, aliamua kutii agizo la Spika Makinda kwa kufuta usemi wake kuwa wapo baadhi ya wabunge ambao wanatumia Bunge kwa kujionyesha kwa wananchi kupitia katika runinga.

Baada ya Werema kufuta usemi huo ikafuatia zamu ya Zitto kufuta usemi wake kuwa Werema anaumwa kutokana na kutoa majibu ya kuudhi bungeni.
Awali Lissu alitaka kuondolewa kwa mamlaka anayopewa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ya kutoa misamaha ya kodi, ambapo alidai kuwa, mamlaka hayo hutumika kama mwanya wa rushwa. Wakati akijibu hoja hiyo, Werema alisema ni vema kamsema Lissu ili awe huru kwani amekuwa na tabia ya kusema mambo bila kufikiri, kwa sababu ya kutaka kuonekana kwenye runinga.
Lissu pia aliingia katika mzozo tena baada ya kutaka posho kubwa zinazotolewa kwa watumishi zikatwe kodi, lakini hoja hiyo ilipingwa na wabunge. Baadaye Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi, alisimama na kuunga mkono hoja ya Lissu na kueleza kuwa mshahara unaotolewa kwa wabunge ni mkubwa na akashauri kuwa hoja ya posho hizo iwasilishwe kwenye Tume ya Kanuni ili ipitie suala hilo.

Lissu pia aliingia katika mzozo na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Lazaro Nyalandu, pale aliposema kuwa anashangazwa na waziri mdogo (Nyalandu) kusema misamaha inayotolewa na serikali ina tija.
Alisema tume kadhaa zimekwisha kuundwa kuchunguza misamaha hiyo, hasa ile ya kampuni za madini na kubaini kuwa haina manufaa. Baada ya kauli hiyo, wabunge wa CCM walipiga kelele kudai kauli hiyo ya Lissu ni dharau na kumtaka aifute. Lissu alilazimika kuifuta kauli hiyo baada ya kusema kuwa amesahau kuwa hivi sasa waziri mdogo anaitwa Naibu Waziri.

Moto wa wabunge wa CHADEMA uliendelezwa baada ya Mbunge wa Ubungo, John Mnyika kusimama jana jioni na kupinga eneo moja katika muswada huo huo wa fedha lililokuwa likipendekeza wawekezaji kupewa nafuu ya kulipa kodi katika kipindi cha miaka mitano, huku yeye (Mnyika) akipendekeza iwe mitano.
Hoja hiyo ya Mnyika iliungwa mkono na Mbunge wa CCM, Simbachawene na kusababisha miguno ya kushangiliwa na wabunge kadhaa kwa makofi, kabla ya Naibu Waziri Nyalandu kusimama na kusisitiza kwamba pendekezo kwamba miaka 10 ilikuwa ni muhimu.

Mabishano hayo ambayo yaliibuka wakati Bunge lilipokaa kama Kamati ya Matumizi, yalimalizwa na Mwenyekiti Makinda ambaye alipoomba wabunge wajibu kwa kauli za ndiyo na siyo, alisema waliounga mkono pendekezo la serikali walikuwa wameshinda.
Uamuzi huo wa Makinda ulifuatiwa na sauti ya Zitto aliyesikika akimtaka mwenyekiti huyo kutumia utaratibu wa wabunge kupiga kura za kuhesabiwa ili kujua idadi kamili ya wabunge waliounga mkono hoja ama ya Mnyika au ile ya Nyalandu (serikali). Makinda aliendelea na vifungu vingine akionyesha ama kutosikia au kutotilia maanani ushauri huo.

Tanzania Daima

- Watumishi wote wa Serikali wakatwe kodi, ndio iliyokuwa hoja yangu ya msingi niliposema kufutwa vyama vyote vya siasa nchini thaanks mbunge kwa kunielewa!, sasa mfano uanzie kwa kilipia kodi mshahara wa Dr. Slaa na wengine watafuata tu!

Willie @ NYC, USA.
 
Back
Top Bottom