MwanaHaki
R I P
- Oct 17, 2006
- 2,401
- 707
Kwa kawaida, mimi si mwanzilishi wa thread kwenye jukwaa hili maridhawa, lakini leo nimelazimika kuwa mwanzilishi.
Nimesoma kwamba TANESCO itakabiliwa na ushindani baada ya sheria mpya ya umeme kupitishwa (The Electricity Bill) wakati wa mkutano ujao wa Bunge.
Ushindani utakaokuja utakuwa na mtazamo wa kibiashara, kumpatia mteja unafuu, wakati huo huo, kumrejeshea faida mwekezaji. Suala la nani atakayewekeza, kwa viwango gani, ni suala la kisheria.
Lakini tuangalie, je, mtazamo wa kuwa na wawekezaji binafsi utaisaidia Tanzania ama hautaisaidia? Je, ni kweli kwamba TANESCO imeshindwa kukabiliana na changamoto za wakati huu, kiasi kwamba inalazimika kushindanishwa na wawekezaji binafsi?
Kwa mtazamo wangu, kuendelea kutumia vyanzo vya uzalishaji nishati vinavyotokana na mafuta ya petroli au maji, ni mtazamo ambao utalifikisha taifa hili kwenye wakati mgumu zaidi. Ni wazi kwamba mafuta ya petroli ni nishati ambayo inatumika na kumalizika, hata kama visima vipya vinagunduliwa kwenye nchi kadhaa, ikiwemo Tanzania. Ni nishati ambayo, licha ya kuwa na madhara kwa dunia kimazingira, haisaidii walaji kuwa na 'uhuru' wa kiuchumi, kutokana na mfumo uliotawaliwa na uroho wa kupita kiasi, wa kupanga bei ya mafuta hayo ya petroli kwenye soko la dunia.
Tayari, ninavyoandika, teknolojia mbadala ambayo ni rahisi kutumia, ingawa gharama za awali za uundaji wa teknolojia hiyo bado ziko juu, inaweza kutumika kikamilifu, na kuwa teknolojia pekee ya uzalishaji wa nishati ya umeme. Hii ni teknolojia ya Stirling. Kwa maelezo zaidi, tafadhali nenda kasome
1) http://www.wisegeek.com/what-is-a-dish-Stirling-system.htm
2) http://www.sandia.gov/news-center/news-releases/2004/renew-energy-batt/Stirling.html
na
3) http://www.stirlingenergy.com/whatisastirlingengine.htm
Teknolojia hii ilibuniwa zamani sana, takriban miaka 200 iliyopita, na mbunifu Stirling, ambaye alitaka kuwa na injini ambayo ingeendelea kuzalisha nishati kwa kutumia malighafi ya joto pekee.
Huko Marekeni, Serikali imesaidia utafiti, ambao kwa sasa, injini ya Stirling inatumia king'amuzi kwa kukusanya joto la jua, ambalo linatumika kama nishati ya kuendeshea injini hiyo, ambayo kwa sasa inaweza kuzalisha wastani wa kiwango cha Mega Watt 1 kwa kila injini inayotumia king'amuzi (Dish Stirling Engine - DES).
Changamoto kubwa inayotukabili Watanzania ni kwamba, jitihada za kutumia vyanzo mbadala vya kuzalisha umeme vinakwamishwa na wafanyabiashara wa mafuta, ambao wanataka kuendelea kupata faida kwa kuuza mafuta yao, hivyo kuwa na ushawishi mkubwa wa kisiasa na kiutashi kwa watendaji wa Serikali yetu.
Kilichobakia ni sisi wenyewe kufanya utafiti zaidi, wa jinsi ambavyo tunaweza kuchukua fursa mpya za kibiashara zitakazojitokeza baada ya Sheria ya Umeme mpya itakayopitishwa, ili tuanze kuwa na vyanzo vingi vya umeme, ambavyo vitakuwa vinatumia nishati mbadala.
Natumai wito huu utaitikiwa na washika dau.
Napenda kuwasilisha.