Mjadala wa namna ya kukabiliana na kuvuja kwa nyumba, maoni ushauri njoo tujadiliane

Alvajumaa

JF-Expert Member
Jul 5, 2018
4,937
6,044
Wakuu kwema !

Kama maada inavyojieleza hapo juu, kuvuja kwa nyumba iwe ya kawaida(mfuto), ghorofa(storey), contemporary n.k.
Maoni, ushauri karibuni sana.

Kwanza niwe muwazi kabisa nyumba nyingi hua zinavuja ila hua zinatofautiana namna ya kuvuja, zipo ambazo zinadondosha matone tuu kiasi kwamba huwezi kuona, zipo ambazo zinavujisha maji mengi kiasi cha kudondosha gypsum yaan unaokota mapande ya Gypsum.

Katika uzoefu wangu mdogo wa miaka 8+ katika ujenzi nimeona majengo mengi yakivuja, tena mpaka ghorofa ambazo zinamwagwa zege iliyotengenezwa b. plant zinavuja.

Nyumba ambazo zimepauliwa kawaida bado zinavuja, nyumba ambazo ni contemporary pia hua zinavuja hivyo dhana kwamba nyumba ikijengwa contemporary lazima ivuje tuitoe maana zipo ambazo zimejengwa na hazivuji.

Sababu zinazopelekea kuvuja kwa ghorofa, nyumba (kawaida) & contemporary. Ghorofa - hizi case hutokea mara chache sana ila kwenye roofing wakati mwingine design inataka uweke wire mesh na Styrofoam ambayo hua inatunza maji hivyo baada ya muda huanza kuvuja kidgo kidgo, kuna project moja tulifanya Zanzibar ni hotel tulipata shida kutokana na design... ila tulirekebisha tatizo

Nyumba (kawaida) - nyumba za kawaida hua zinavuja sana ila taarifa zake hazisambai kama kwenye nyumba za contemporary , Mara nyingi hapa kwenye roofing Fundi anaweza kufanya makosa kama atagonga msumali kwenye mbao afu anakosa mbao, shimo linaachwa anagonga sehemu nyingine, sehemu iliyoachwa baadae inadondosha matone na kuleta mvujo.

Sababu nyingine mvujo wa mpepea yaan mvua ya upepo, mvua hizi zinapopiga kama Fundi hakufunika vizuri kwenye maungio ya bati au kwenye kona bati ujue nyumba itavuja tuu, ni muhimu ridge na valley zitumike vizuri kuziba maungio,

Contemporary house - hizi ni design ambazo zinaonekana ni za kisasa ila ni za muda sana, wengi wamekua wakipenda huu muundo katika kufunika bati, yaan unaziba bati isionekane, nyumba hizi moja ya sababu ya kuvuja ipo hapo juu yaan issue ya misumali mfano misumali yenye tread si mizuri katika kupaua hua inaacha eneo wazi.

Sababu nyingine ni namna wanavyoweka sehemu ya kutolea maji yaan Gutter, unakuta nyumba ni kubwa ila sehemu ya kutolea maji ipo moja, pia ni nyembamba kiasi cha kusababisha maji ya mvua yakija yanajazana kiasi cha kuanza kuvujisha kwa vile yamekaa mda mrefu, kumbuka zege zetu za mtaani hua hatutumii poker hivyo voids katika zege zinakua nyingi kiasi cha kutengeneza gap na maji kupitia humo.

Sababu nyingine ni bati zenyewe, baadhi ya bati hua zinakua na matobo ila kwa vile tunanunua kiwandani hua tunaamini zipo sawa pasipo kukagua, hili ni nadra kutokea ila ni muhimu unapoenda kununua bati dukani/ kiwandani kagua kabla ya kupakia (usafiri) ujiridhishe,

Nini cha kufanya pale nyumba yako inapovuja? Usipaniki na kuanza kutukana Fundi, mchoraji au Engineer, hayo Mambo ni kawaida hivyo muhimu ni kukabiliana na tatizo.

Ghorofa- kwenye ghorofa kama kuna kunavuja, muhimu kujua maeneo yanayopitisha maji, rejea kwenye design pia uangalie, Ikiwa zege ishamwagwa , chukua kishoka fanya kutindua (haking) eneo lote la slab ili kupata atleast 3mm then fanya sand floor screed, Baada ya hapo safisha pawe safi ondoa vumbi na uchafu, paka water proofing kama Moyal proofing, sypex, andika, layer water proofing n.k yaan tumia water proofing kuvunika eneo zima.

Wengine hujenga Tiles ila ni muhimu kuzingatia Tiles ziwe zile zinazohimili jua yaan hali ya joto, si Tiles zote ziko namna hiyo,
Ni muhimu pia kutengeneza njia ya maji kwa pembeni ili yashuke chini kupitia pipes zilizoko kwenye duct.

Nyumba ya kawaida- pale unapokutana na tatizo la kuvuja basi Fundi anaweza kutumia silicon, maloo/lami kuziba sehemu husika na itakua historia,

Contemporary house - ni muhimu gutter yako iwe atleast 450mm ili maji yawe na nafasi pana ya kupita, pia kama ikiwezekana basi Gutter ziwe nyingi kama nyumba ni kubwa basi maji gawanya sehemu kama 3 au 4 hivi, hii itapelekea maji yanakua machache kwenye gutter kwa vile yanapokelewa sehemu nyingi, pia kwenye bati rejea somo la hapo juu yaan silicon na maloo.

Wakuu , ushauri wangu tuache kukatisha tamaa wale wanaotaka kujenga contemporary kwamba zinavujisha wakati nyumba nyingi tuu ambazo hazipo muundo huo bado zinavuja.

Pia pale mtu anapojenga epuka sana Fundi mmoja kufanya kazi zote, yaan tofali yeye , plaster yeye , kupaua yeye, Tiles yeye .... hii sio nzuri, Fundi hua anabobea sehemu moja au mbili ni ngumu kufanya kazi zote kwa ufanisi.

Niwakaribishe katika mjadala huu, weka maoni yako, ushauri wako n.k pia najua wengine ni wazoefu kunizidi hivyo share nasi hapa
 
kuna style mmoja nimeona uganda hawapigi gypsum board wanamwaga ka floor ka cement kwenye mbao na kuna wavu speacil kwa kazi hyo alafu wanachora mauwa nyumba inakua poa sanaah ata kama juu pata vuja huwezi ona effect yoyote
 
kuna style mmoja nimeona uganda hawapigi gypsum board wanamwaga ka floor ka cement kwenye mbao na kuna wavu speacil kwa kazi hyo alafu wanachora mauwa nyumba inakua poa sanaah ata kama juu pata vuja huwezi ona effect yoyote
Ahsante kwa maoni yako mkuu
 
Pia pale mtu anapojenga epuka sana Fundi mmoja kufanya kazi zote, yaan tofali yeye , plaster yeye , kupaua yeye, Tiles yeye .... hii sio nzuri, Fundi hua anabobea sehemu moja au mbili ni ngumu kufanya kazi zote kwa ufanisi.
Point Kubwa na muhimu sana hii! Ushauri mzuri
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom