TUSHIRIKISHANE Mjadala wa Mipango ya Maendeleo kwa Jimbo la Kigoma Mjini

KATIKA UTEKELEZAJI WA AHADI NAMBA 4 KIPENGELE CHA KUBORESHA MAZINGIRA YA ELIMU Mradi wa kuboresha elimu na kuinua taaluma ndani ya kata ya Rusimbi, hatimae leo tumepata Photocopy Mashine kwa Shule ya Msingi Rusimbi. Kifaa hicho ni sehemu ya vifaa vinavyohitajika kwa ajili ya kuchapisha mitihani ya kila wiki ambayo wanafunzi wa Shule nzima watakuwa wanafanya mitihani.

Natoa shukurani za dhati, tena za dhati kweli kwa wananchi wa Rusimbi, na wazazi wa wa wanafunzi wa S/M Rusimbi kwa ushirikiano wao ulofanikisha kupata mashine hiyo.

Pia shukurani za dhati nazitoa kwa Mtendaji wa Kata, Mratibu wa Elimu wa Kata, Afisa Maendeleo ya Jamii wa Kata, na watendaji wa mitaa ya TAIFA na Kawawa kwa kazi kubwa waloifanya kufanikisha upatikanaji wa mashine hiyo.

Pia natoa pongezi kwa Mkuu wa Shule ya msingi Rusimbi na Walimu wake kwa jitihada kubwa walofanya kupandisha taaluma za wanafunzi wa Shule hiyo. Natumai mashine hiyo itakuwa ni chachu ya kuzidisha juhudi za kimasomo ili kuboresha elimu katani.

Mungu ibariki Rusimbi.

BUTIJE (Diwani Rusimbi)
d991128977d7c5dd7134d5899c93a7b9.jpg
a172998f241ecd9d2b162c47535336f7.jpg
 
KATIKA KUSHUGHULIKIA UTATUZI WA MIGOGORO YA ARDHI KAMA AHADI NYONGEZA NAMBA 2 Leo tumekaa na pande mbili zenye mgogoro ktk eneo la Makaburi ya Katubuka ambapo BAKWATA inalalamikia Kanisa la Pentekoste FPCT Katubuka kuingia katika eneo la Makaburi na kujenga kabisa lao.

Tumekutana na pande mbili hizo. Baada ya kukutana na pande hizo kamati itakutana na wadau wengine kupata taarifa Zaidi kabla ya kufikia kutoa mapendekezo yake (Butije Hamis- Mwenyekiti kamati ya mipango miji)
44d9b4ce710b0ab0c1ebfa953e5f03b0.jpg
30bcbbe2020bb851e7ac7a6e576af416.jpg
009a812260784193d7a0bbb8a4dd1b61.jpg
74bb870387293fb97a16b137ba626566.jpg
 
Diwani kata ya Kigoma Ndg Hussein Kalyango akifafanua juu ya mradi wa sanamu la mgebuka ambao umesitishwa kwa muda kidogo hivyo ameutolea ufafanuzo na haya ndio machache aliozungumza kwa wananchi wake
 
Diwani kata ya Kibirizi Ndg Yunus Ruhomvya akifafanua juu ya swala la elimu bure na Shule ya Buronge ambayo inatoa elimu bure kwa kidato cha tano na sita katika shule iliopo kwenye kata yake hio. Pia Mheshimiwa Ruhomvya ni mwenyekiti wa kamati ya Elimu
 
. Meya wa manispaa ya Kigoma ujiji Ndg Hussein Ruhava akifafanua juu ya mradi wa Tushirikishane na namna ambavyo unaisaidia manispaa ya kigoma ujiji katika utendaji kazi kwa uwazi.
 
28 January 2017 nimekutana na kuzungumza na wananchi wa kata ya Bangwe kujadili madai ya fidia ya viwanja eneo lililoendelezwa kuwa hifadhi ya msitu mtaa wa katonga kupitia tasisi ya TACARE.
Pamoja na mambo ya msingi tuliyojadiliana bado changamoto inayojitokeza ni viongozi waliochaguliwa kama kamati ya ufuatiliji kutotoa taarifa ya kila hatua kwa wahusika.

Idadi kubwa ya majina ya wadai ikilinganishwa na ukubwa wa eneo husika, Hatahivyo maeneo mengi yaliyokuwa yanamilikiwa na wazazi ambao wamefariki, Maeneo hayo wengi wao wamesimama wanafamilia zaidi ya mmoja jambo ambalo linaweza kuongeza mgogoro.

Pamoja na baadhi ya wahusika wa maeneo hayo kutokuwepo kwenye orodha iliyowasilishwa kwa mkurugenzi na TACARE.

Kwa pamoja tumekubaliana kuwa 6 February kifanyike kikao cha tathmini ya majina halali ya wamiliki eneo hilo na kuchagua baadhi ya Viongozi watakaosaidia kufuatilia stahaki husika.
Bangwe nimoja ya wahanga wa Migogoro mingi ya ARIDHI ndani ya manispaa ya kigoma ujiji chanzo chake kikubwa ni upimaji na utwaaji wa ARIDHI kupitia ARIDHI mkoa. 1999 hadi 2004 bila kushirikisha wamiliki husika.
Tushirikiana Kwa pamoja tuweza kutatua changamoto zote.

HUSSEIN RUHAVA
MANISPAA KIGOMA UJIJI

54e48e70ef2bd1880814fab62edd710b.jpg
IMG-20170129-WA0003.jpg
IMG-20170129-WA0008.jpg
IMG-20170129-WA0009.jpg
IMG-20170129-WA0001.jpg
 
Diwani kata ya Mwanga Kaskazini Clayton Revocatus almaruufu kama BABALEVO amehakikisha kasimamia ahadi ya ufunguzi wa soko la usiku kwenye kata yake ili kukwamua kina mama toka kwenye janga la umaskini na kujishughulisha kwenye biashara. Pichani ni mabomba kwa ajili ya kuwekea taa za usiku ili kuhakikisha ufanyaji wa biashara kwa usalama na mwanga wa kuhakikisha biashara zinafanyika bila changamoto ya giza
27dfd7a7406478912e1ee53a46fcfa7f.jpg
d35e91e7792410b9ffe4d4cd02f96cb0.jpg
097a1439684a10d453699efb9d6ee716.jpg
b8d774a3e325cb939226240f4e24c6ea.jpg
 
Waheshimiwa madiwani wa manspaa ya ujiji/kigoma wajumbe wa kamati ya fedha walitembelea mradi wa MAJI Mgumile kata ya KAGERA nakuangalia ujenzi wa mradi utaoanza tarehe 01/02/2017 utaishia 30/07/2017 Gharama ya mradi 548,000,000 Mradi huu ukikamilika kero ya maji mgumile itakuwa ndoto.
Mstahiki Meya wa manspaa ya ujiji/ kigoma amewakikishia wakazi wa mgumile kata ya kagera kuwa mradi wa maji ni moja ya Ahadi ya mhe.Mbunge na Diwani nilazima utakwisha kwa haraka na wanachi watapata huduma ya maji safi na salama fedha zipo tayari na mkandarasi anaanza mara moja.
c427179ac4f281c29a9774e38c20fcd3.jpg
 
Madiwani wa manspaa ya ujiji/kigoma wa kamati ya fedha na uongozi wametembelea mradi wa ZAHANATI YA MGUMILE ulionza tarehe 20/04/2015 mpaka 20/09/2015 kwa gharama ya Tshs milion 83,000,000 lakini mpka jengo lipo hivyo limeghalimu milion 23,000,000 zimelipwa.
Mstahiki meya wa manspaa amezungumza na wananchi wa Mgumile kata ya KAGERA nakuwahaidi kuumaliza zahanati hiyo na Amesikiliza kilio cha wakazi wa mgumile nakwenda kushughulikia na ujenzi utaanza haraka sana.
Huduma ya Afya nimuhimu kwa wakazi wa kagera.
dbbafdc35cea701ccac9d3968fd9632c.jpg
54bae70114e7a411b750113dc2bc1426.jpg
1b170e5765a536c5a5509fd929821f60.jpg
d976547e7114fca3edff103094af8d70.jpg
 
Madiwani wa Manspaa ya ujiji/kigoma wajumbe wa kamati ya fedha wametembelea shule ya Buronge High school ilikuangalia ujenzi wa choo cha wanafunzi na walimu na kuangalia High school ilivyoanza kwa mara ya kwanza ktk shule ya Buronge.
Mstahiki meya na madiwani wamezungumza na wanafunzi na walimu kuwa wavumilivu manspaa inajenga miundombinu ya shule lakini kumaliza changamoto mbalimbali za shule,wanafunzi mnatakiwa kusoma kwa bidii na walimu kufundisha kwa bidii ilikufanya wanafunzi kufaulu wa juu.
Meya amewataka wanafunzi kusoma na kutambua manspaa itaendelea kuwasomesha bure kidato cha TANO na SITA BURE kama tulivyotoa Ahadi kwa wananchi natumeshawalipia wanafunzi Ada kilichobaki nikusoma tu.
Tumepanga kwenye manspaa kujenga High school 3 kwa kipndi cha miaka mitano ya utawala wetu- Ruhava Hussein(Meya Kigoma Ujiji)
ffe4bb4f84766f08cbedef17cd37aa04.jpg
42bb6b3c12e9bbcb1f2d632b7aebdefe.jpg
ab8fb87b0f31cda612a8430fe623ca00.jpg
d8530360445851d7f9f1933b54d38f7f.jpg
ad37d4d311b5f9273a2d85d09c726869.jpg
a64a35c8db8cc9c6ad2295fe9e4149fd.jpg
131038989d93ff27c11f6e910e12e55b.jpg
 
Back
Top Bottom